Sunday, September 29, 2013

MAAJABU YA MDALASINI NA ASALI

          Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na
magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama
itachanganywa na mdalasini wa kawaida.
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa
yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.
Kama ifuatayo:


1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali
pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua
sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya
asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko Copenhagen, madaktari waliwapa
wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa kijiko kimoja *cha chai* cha asali na kimoja cha mdalasini kila
asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu kubwa ya maumivu yao na _
ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea na kutembea vyema.

2. kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo
maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu
unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai} vya mdalasini na kijiko kimoja
{cha chai} cha asali huondoa bacteria kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya
maji ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.

5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini kwenye chai ya raspberry
nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu makali ya canker sores.

7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio} kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu mwilini.
Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric Vogelmann. Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.

      8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini, mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba koo.

9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili wanashauriwa kunywa anglao vijiko
viwili {vya mezani} kila siku kabla ya muda wa kulala {usiku}. Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi
ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.
Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya mgando {paste} ambao hupakwa
kwenye fizi za meno na kunyonywa na kuingia mwilini taratibu.
Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na kupata mapacha wa kike
baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.

10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na
kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

l l . Esi di / Gesi -Co2.  Hco3.  Hcl .
Kula asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi/acid kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko India na Japan.

12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}
Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye
mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa. Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko kimoja {cha mezani} cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja ulionyesha
.
13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}
Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na kizunguzungu
yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali ilyochanganywa na mdalasini. Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha
ukawaida na wote 137 waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya wiki chache za tiba hii ya ajabu.

14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini   kwa pamoja - wataalamu wanasema.
Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya vitamini{vivurutubisho}na madini pamoja na
michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za  damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na {bacteria}.

15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}
Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.
Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana, watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa na dunia yakusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.

16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula chakula} huondoa kiungulia na
wataalamu wanasema kwamba asali husaidia kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.

17.Flu {INFLTJENZA}
Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia ya ajabu ambayo huharibu
vairasi {vimelea} waletayo Flu.

18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila
siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko
vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo
kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.

19.Chunusi {PIMPLES}
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.

20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} wenye sumu
Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwahso
unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe vinatoweka.

21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}
Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.

22. Kupungua kwa uzito
Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na kupunguza uzito wa mwili
ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu. Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala. Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.

23.Sarakani {CANCER}
Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa asali ina uwezo mkubwa
katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya kutibu sarakani.
Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa sarakani ya
mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya kawaida".

24.Uchovu {FATIGUE}
Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo wa kuongeza nishati
mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji,
nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri
wakati nishati {nguvu}inapoanza kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa. "katika wiki moja hii
itajionyesha".

25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}
Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu} nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila asubuhi halafu nawisha nyayo kwenye maji baridi na vaa viatu.

26.Harufu mbaya kutoka mdomoni
Waamerica wa kusini wanasukutua kwa kutumia asali na mdalasini pamoja na vuguvugu kila asubuhi
ili kufanya harufu toka mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya kusini mashariki, watu hula kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni {halitosis}. Wataalamu wanaamini kwamba uwezo wa kuua bacteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni.

27.Kupungua kwa usikivu {HEARING LOSS}
Dozi za kila siku za asali na mdalasini hufanya hali ya usikivu kuwa makini kama ilivyogunduliwa na
Wagiriki wa zamani.
MDALASINI NA ASALI vinaweza kukufanya uonekane kama picha yenye afya nzuri kama ile ya
mwonyeshaji mitindo ya mavazi na muigizaji sinema Jocqol Bell.
Imeandikwa na BEATRICE DEXTER kukopiwa na BENCOS
Mwandishi
{INTERNET}
{"Ni mchanganyiko Mama asilia wenye uwezo mkubwa wa kuponya"}.

MISAADA YA KIMAENDELEO JIMBONI KALENGA YAMNYIMA USINGIZI WAZIRI DR MGIMWA


Dr Wiliam Mgimwa
KUELEKEA uchaguzi  mkuu  mwaka 2015 mbunge  wa  jimbo la kalenga na waziri fedha na uchumi Dr Wiliam Mgimwa ameanza kuingia na hofu ya kupata  upinzani mkali katika jimbo lake  la  uchaguzi na  kuwataka wapiga  kura  kuwapuuze wadau wa maendeleo  wanaofika  kusaidia kutatua  kero za  wananchi.
 
Katika  kile kinachoonyesha  kuwa  waziri Dr Mgimwa ameanza kuingiwa na hofu ya  kushindwa katika  uchaguzi  mkuu mwaka 2015  hata kabla ya wana CCM  wanaotaka  kuwania ubunge kujitangaza hadharani ,Dr Mgimwa ameponda misaada  hiyo   na kuwataka  wananchi kuwapuuza wadau  wanaojitolea  kusaidia matatizo ya  wananchi jimboni kwake.

Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,John  Adam   na  Sarah Sanga  wakazi wa kata ya Nzihi walisema  kuwa  hawakutarajia   kusikia mbunge  wao  akionyesha kuwabeza  watoto  wao  wanaofika  katika vijiji  vyao  walivyozaliwa  kusaidia matatizo ya wananchi.

Alisema  Adam kuwa  ni  vema  wabunge na madiwani kuendelea  kuwa na mshikamano  wa  kweli kwa  wadau mbali mbali  wa maendeleo  wanaofika kusaidia shughuli za maendeleo  katika maeneo yao badala ya  kuendelea  kuingizwa misaada  hiyo katika sura ya  kisiasa .

Kwani  alisema  kuwa  hatua  ya  mbunge Dr Mgimwa  kuwataka  wananchi  wa  jimbo  hilo la Kalenga  kuwapuuza  watu mbali mbali  wanaofika  kusaidia  shughuli za kimaendeleo  katika  jimbo  hilo ni kauli isiyo na faida kwa  maendeleo ya  wana kalenga .

"  Hivi  kweli  siasa itugawe  wananchi na familia zetu ...leo mtoto  wetu anapokuja  kutusaidia  misaada  ya kimaendeleo  tukatae kwa  sasa  mbunge wetu  hapendi  watu hao kutusaidia sasa  nini maana ya maendeleo"

Huku Bi Sanga  akimtaka  mbunge Dr Mgimwa  kuachana na  hofu ya kisiasa na kuwa  wanaoweza  kufanya mabadiliko  ya mbunge ama chama kipi kitawale  jimbo la Kalenga ni  wananchi ambao  mwisho  wa  siku  wanapima kazi iliyofanywa na mbunge  ama  diwani  husika na kama  hakuna  jipya  hawataangalia mtu  wala chama wanatoa hukumu .

Mbunge  Mgimwa katika moja kati  ya mikutano yake  aliyoifanya katika jimbo la Kalenga  alipata  kutoa kauli iliyonukuliwa na gazeti la Majira  la Jumamosi tarehe 28/9/2013  kauli inayoonyesha  wazi  kuwa ameanza  kupata  hofu ya  kisiasa  jimboni  baada ya kutamka  wazi  kuwa  wapo  watu  wanazunguka kutoa misaada vikiwemo  vitanda  katika Hospital ya Ipamba .huku zikiwa ni siku  chache  kupita toka mkazi wa Nyamihuu Jackson Kiswaga  kukabidhi  msaada  huo wa vitanda  katika  Hospital  hiyo kama fadhila  yake kwa Hospital kutokana na kulazwa  hapo na kuhudumiwa  vema ,msaada ambao hata  hivyo mbunge  huyo anadaiwa  kuwa na taarifa  nao.

SERIKALI YAYAFUNGIA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA KWA UCHOCHEZI

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeyafunga magazeti ya Mwananchi na Mtanzania kwa madai kuwa  yanaandika habari za uchochezi na uhasama.

Imeelezwa kuwa kutokana na habari ambazo zinachapishwa na magazeti hayo zinasababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), ni kwamba Gazeti la Mwananchi limefungiwa kutochapishwa kwa siku 14,  kuanzia Septemba 27, 2013.

"Adhabu hii imetangazwa kwa tangazo la Serikali namba 333 la Septemba 27, 2013.
Gazeti la Mwananchi limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi na uvunjifu wa amani.

"Mfano Julai 17, 2013 katika toleo namba 4774 ilichapisha habari isemayo "MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013" kwa kuchapisha waraka uliozuiwa kwa matumizi ya vyombo vya habari. Waraka huo ulikuwa wa siri kwani haukupaswa kuchapishwa magazetini," ilisema taarifa hiyo.

Aidha, katika toleo la Agosti 17, 2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho "Waislamu wasali chini ya ulinzi mkali" habari hiyo ilikolezwa na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

"Habari na picha hiyo ilitoa tafsiri  kuwa Jeshi la Polisi lilipeleka mbwa katika maeneo ya ibada ya waumini wa dini ya Kiislamu. Jambo ambalo halikuwa la  ukweli," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Jeshi la Polisi katika doria yake siku hiyo halikupeleka mbwa katika maeneo ya misikiti na kwamba Serikali na Jeshi la Polisi linaheshimu na kuzingatia maadili ya dini ya Kiislamu.

Kwa mazingira hayo, taarifa hiyo ilisema jeshi haliwezi kupitisha au kuingiza mbwa katika maeneo ya ibada, hivyo gazeti hilo kuchapisha habari iliyokolezwa na picha ya mbwa ni uchochezi wa kulichonganisha Jeshi la Polisi na waumini wa dini ya Kiislamu kwani mbwa ni najisi kwa sababu hapaswi kuingia katika maeneo ya ibada.

Wakati Gazeti la Mtanzania limefungiwa kutochapishwa kwa siku 90, kuanzia Septemba 27, 2013 kwa kuchapisha habari zenye uchochezi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Serikali ni kwamba gazeti hilo limeonywa mara nyingi lirekebishe mtindo wake wa uandishi wa kichochezi na lizingatie maadili na sheria na kanuni za fani ya habari.

Pamoja na kuonywa gazeti hilo halikuonesha kuzingatia maelekezo ya Msajili wa Magazeti kwani katika toleo namba 7262 la Machi 20, 2013 liliandika habari yenye kichwa kisemacho "URAIS WA DAMU".

Pia Juni 12,  2013, toleo namba 7344 lilichapisha makala isemayo "mapinduzi hayaepukiki". Aidha, Septemba18, 2013 katika toleo namba 73414 ukurasa wa mbele lilichapisha kichwa cha habari kisemacho "Serikali yanuka damu".

Serikali ilisema taarifa hiyo ilikolezwa na picha zilizounganishwa kwa ustadi mkubwa kwa kutumia kompyuta kutapakaza rangi nyekundu mithili ya damu nyingi kumwagika .

"Katika habari hiyo gazeti hilo limedai bila uthibitisho kuwa Jeshi la Polisi linahusika na wahanga waliumizwa na watu wasiojulikana kwa kumwagiwa tindikali na waliovamiwa na kujeruhiwa vibaya.

"Vile vile gazeti hilo limeishtumu Serikali kuwa goigoi katika kushughulikia matukio yenye sura ya kigaidi. Kwa ujumla wake habari hiyo ni ya kichochezi ina lengo la kuwafanya wananchi wavichukie vyombo vya ulinzi na usalama wavione kuwa haviwasaidii.

"Kutokana na makosa yalitajwa hapo juu Serikali imelifungia Gazeti la Mtanzania  kutochapishwa kwa muda wa siku 90 kwa tangazo la Serikali namba 332 la  Septemba 27, 2013," ilisema taarifa hiyo.

Pia ilifafanua kuwa Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kwa ujumla kuwa makini, kuzingatia weledi, miiko na madili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Serikali inawataka wamiliki na hasa wahariri kuhakikisha habari wanazoandika na vipindi wanavyoviandaa vinazingatia taaluma, kuweka mbele maslahi ya taifa na uzalendo wa hali ya juu.

Pia inavionya vyombo vya habari vinavyotumia uhuru wa habari bila wajibu kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali ikiwemo kuvifungia. Serikali haitakubali kuona vyombo vya habari vikiwa chanzo cha uvunjifu wa amani nchini.

Wednesday, September 18, 2013

WALIOLIPUA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA JIJINI ARUSHA WAKAMATWA...!!



 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo. 

WATUHUMIWA walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenyemkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema hayo jana katika mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti.
 
“Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani."
 
Mulongo alisema kwa sasa Polisi iko katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo.
 
Malengo mengine kwa mujibu wa Mulongo ni kuwafahamu watu wote waliopewa zabuni ya kuingiza mabomu hayo, ili hatua za kisheria zifuate.
 
Mulongo aliomba wananchi waendelee kutulia wakisubiri matokeo ya Serikali na hata wakitajwa wahusika waiachie Polisi ifanye kazi yake. Mabomu hayo yalirushwa Mei 5 kanisani Olasiti na Juni 15 uwanja wa Soweto, wakati wa hitimisho la kampeni za udiwani za Chadema mkoani hapa.
 
Kanisani Mlipuko huo ulitokea muda mfupi baada ya kuanza kwa ibada ya uzinduzi wa Parokia hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini na Mjumbe wa Baba Mtakatifu, Askofu Fransisco Mantecillo Padilla.
 
Mbali na Askofu Padilla, pia alikuwapo mwenyeji wake Askofu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha na waumini zaidi ya 2,000.
 
Wakati mgeni rasmi akitoka nje ya Kanisa akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi, mtu alirusha kitu chenye ukubwa wa ngumi, kwenda eneo lenye mkusanyiko wa watu na baada ya kutua, kulitokea kishindo na mlipuko mkubwa uliosababisha taharuki miongoni mwa waumini na kusababisha watu kukimbia ovyo.
 
Katika tukio hilo, watu wawili walifariki dunia, akiwamo Regina Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariki dunia siku ya tukio wakati akipewa matibabu katika hospitali ya Mount Meru na majeruhi mwingine James Gabriel (16) alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 6.
 
Bomu hilo lililipuka Juni 15, katika Uwanja wa Soweto wakati wanachama na wapenzi wa Chadema wakiwa wamekusanyika kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani humo.
 
Mlipuaji alilipua bomu hilo dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kumaliza kuhutubia mkutano huo na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kisha kuacha maswali mengi.
 
Mulongo alitaja waliopoteza maisha kuwa ni Judith Mushi (46) ambaye alikuwa Katibu Kata wa Chadema, Kata ya Sokoni One na mkazi wa eneo hilo aliyemtaja kwa jina moja la Justine (16) wa Sombetini ambaye alifariki dunia katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru.
 
Siasa Akizungumza katika mkutano huo wa kukaribisha wawekezaji jana, Mulongo alisisitiza Serikali inahitaji siasa zenye tija na anapotokea mwanasiasa mwenye kupinga maendeleo, atashughulikiwa.
 
“Kila mwanasiasa awe wa kuchaguliwa au kuteuliwa, aliposimama kuomba nafasi hiyo wote waliahidi maendeleo kwa wananchi, hivyo tufanye hivyo,” alisema.
 
Mulongo alisisitiza kuwa kutokana na umakini wa vyombo vya usalama, wanaomba wawekezaji wasiwe na hofu, wajitokeze kuwekeza maeneo ya mkoani hapo, bila hofu.
 
Alisema mkoa huo unatangaza fursa za uwekezaji kwa sababu ya kuongeza kipato na ajira kwa wakazi wa Jiji hilo pamoja na kupanua wigo wa masoko na bidhaa zinazozalishwa hapa.

-Habari leo

DOKTA NIWE NAMLETA MARA NGAPI KWA WIKI?


Harusi ilishapita mwezi, bwana na bibi harusi wakawa wanataka kupata mtoto lakini hawajui tendo gani wafanye ili mimba itokee. Wakaenda kwa daktari kumueleza tatizo lao, akawatafutia kitabu cha watoto wadogo chenye maelezo rahisi baada ya siku mbili wakarudi na kulalamika kuwa hawajaelewa kitu, akawapa picha waangalie, wakadai hawaelewi, akawatafutia video zenye shughuli hiyo 'live' bado wakadai hawaelewi, daktari sasa akakasirika akamuita jamaa na mkewe kwenye ofisi yake, walipofika tu daktari akamshughulikia mke wa jamaa mbele yake ili jamaa aone kinachofanyika, alipomaliza wakati anavaa na mke yuko hoi;
DAKTARI: Umeona sasa kazi inayotakiwa kufanywa?
MUME: Dah asante sana dokta pole kwa kazi, sasa niwe namleta mara ngapi kwa wiki?

Historia ya kuacha kunywa pombe na kulewa


Nilipokuwa mnywaji niliamini kuwa siwezi kuacha pombe kwa kuwa kabila langu linadai mwanaume wa ukweli lazima anywe na pombe ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu. then mijini tunaambiwa kuwa wajanja ni wale wanaokunywa.

nilipokuwa naelekea kulewa, nilijiona naeda kufanya jambo la busara, wakati nalewa nilijiuliza uko wapi utamu na faida za pombe? ebwana utamu wa bia baridi uko pale kwenye kuimeza pale kwenye koo wakati inakaribia kushuka tumboni, basi! kilchobaki ni mzigo

then wakati nimelewa nilijiuliza sasa ninafaida gani? mbona nashindwa kutembea, naongea hovyo, kila mwanamke ni mzuri, nanuka pombe nk?

ngoma kesho yake sasa, mning'inio (hangover), mateso mpaka ugonjwa, walevi wenzangu walinishauri kunywa tena eti nazimua! kuna siku nilikunywa matapu matapu yale yatokayo arusha na siku nyingine nikanywa gongo ya kihaya (kaliiinya), nililewa siku mbili na ugonjwa juu!

nilijiona siwezi kuacha pombe, nakumbuka rafiki yangu mmoja wa kipare aliniambia kuwa ninaweza na akanihakikishia kuwa naweza akasema kama nabishi, basi nijaribu kuacha pombe! nikajaribu siku hiyo (maana nilikuwa nakunywa kila siku), ikapita, wiki, then mwezi.

nikajisemea kuwa kumbe nikijidhibiti itakuwa poa kwa hiyo ninywe kidogo kidogo, baadae nikaona kama bado ni utumwa maana mbele ya pombe, maji, soda na juice, nilichakua pombe, nikaona bado innanitesa, nikasema sasa basi kwenda mbali.

changamoto ni maneno ya watu wanaoisifia pombe na kutudharau tusiokunywa, eti inakuletea marafiki, inapunguza mawazo, sijui vinywaji vingine ni vya watoto wadogo etc. kwa ufupi pombe ni addiction ndio maana matangazo yote ya vilevi hayakwambii kunywa bali yanakwambia onja, wanajua ukionja hutorudi nyuma ila kuacha inawezekana kabsi utakapo acha kuitukuza!

visa na mikasa ya wahamihaji haramu KAGERA


misako mikali inaendelea mkoani kagera, magari ya polisi yaliyosheheni
FFU, JWTZ na mofisa waliovalia kiraia (UWT, PCCB etc) yanaonekana
yakikimbia kama vile yanaendeshwa na vichaa wasiojali uhai wao.

hufika mahala wengine wakasombwa kibahati mbaya. nikiwa maeneo ya
ibwera, nakutana na jamaa mwenye asili ya Rwanda, hali halali,
anasimama milimani akiona gari la binafsi linakuja nduki anakimbilia
porini na kujificha pangoni

jamaa huyu amezaliwa hapa miaka ya sabini, babayake na mama
walimtelekeza na kurudi rwanda na hana mawasiliano nao tangu 1994.

ila sasa imengia siasa pia, nimekutana na bwana mmoja anapanga
kugombea udiwani uchaguzi mkuu ujao, huyu bwana anataka kuchuana
kwenye kata ya meya wa sasa, kapelekeshwa, anasema amelala Lupango ya
uhamiaji kwa siku 7 bila kupelekwa mahakamani, akawa mbogo na
kwalazimisha wampeleke mahakamani

ndo kaachiwa kwa sharti kuwa ajaze mafuta kwenye gari la
polisi/usalama, then awapeleke maofisa kijijini kwao izimbya na
kuwaonyesha makaburi matano ya babu zake ili kuuthibitisha uraia wake!

inasemekana hawa jamaa wakikutilia shaka wanataka vitambulisho,
usipokuwa navyo unaammbiwa imba wimbo wa taifa, ikishindikana basi
imba ile tanzania tanzania nakupenda.........

raia wenye asili za kigeni wote hapa matumbo yao ni ya moto hapa na
wengine wanatamani kuhama mkoa. swali kujiuliza ni je, kwa nini watu
kutoka rwanda, burundi, Uganda etc wanapenda kukimbilia na kujichimbia
hapa nchini lakni hawaombi uraia wala kuwa na nyaraka halali kwe wengi
wao?

Njia KUMI rahisi za kupunguza Uzito





Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.

NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:
1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.
2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.
3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.
4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.
5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.
6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.
7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).
8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.
9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.
10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia kupunguza uzito. Mazoezi ya kunyanyua vitu vyenye uzito ni mazuri zaidi kwa kuwa huchoma Kalori iliyopo mwilini.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/njia-kumi-rahisi-za-kupunguza-uzito/#sthash.UzJf98Qv.dpuf

Njia KUMI rahisi za kupunguza Uzito





Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.

NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:
1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.
2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.
3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.
4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.
5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.
6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.
7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).
8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.
9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.
10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia kupunguza uzito. Mazoezi ya kunyanyua vitu vyenye uzito ni mazuri zaidi kwa kuwa huchoma Kalori iliyopo mwilini.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/njia-kumi-rahisi-za-kupunguza-uzito/#sthash.UzJf98Qv.dpuf

Njia KUMI rahisi za kupunguza Uzito





Kabla ya kukimbilia kujinyima vyakula ili kupunguza uzito, inabidi uamue ni uzito gani unaouhitaji. Wataalamu hawashauri kushusha uzito ghafla kwa zaidi ya kilo 22 ndani ya wiki.

NJIA ZA ASILI ZA KUKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO:
1. Tambua Mahitaji ya Karoli(Nguvu)
Kabla hujaamua jinsi ya kula, unapaswa kufahamu ni Kalori(Nguvu) kiasi gani unahitaji kwa siku. Hii inaweza kupatikana kwa kikokotozi maalumu cha Kalori (Nguvu) kinachotumia kimo, uzito, umri na shughuli za mhusika.
2. Jifunze Kutumia Matunda na Mboga za Majani
Unahitaji walau vipande vitano vya matunda na mboga za majani. Kufanya hivi kutaweka mwili wako vizuri kwa kuwa matunda na mboga za majani vina nyuzi muhimu(valuable fibres) na vitamini muhimu. Pia vinajaza tumbo lako na hufanya usihitaji kula vyakula vya Kalori(Nguvu) sana.
3. Angalia Kiwango cha Chakula unachotumia
Jizuie kula vyakula vyenye Kalori(Nguvu) sana mfano maharage ya soya, mafuta ya samaki, soseji, karanga n.k na ukilazimika kula kwa kiwango kidogo sana. Dondoo ya muhimu ni kutafuna chakula chako taratibu na kwa muda unaofaa ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula na hii itakusaidia kula kidogo.
4. Usiruke Mlo!
Wengi wanaotaka kushusha uzito huona kujinyima milo mfano kuacha kula mchana au asubuhi au usiku ndio njia sahihi wakati sio sahihi, kula chakula kidogo kutafanya mwili uwe na afya. Unaweza hata kugawa ile milo mitatu mikubwa katika vijisehemu vitano au sita vya muda mfupi.
5. Matunda na Mboga Safi ya Asili ndio sahihi zaidi
Vyakula vilivyosindikwa viwandani vina sodiamu na mafuta kwa wingi. Unatarajiwa sana kushusha uzito ukitumia vyakula asili.
6. Usidhibiti sana Matumizi ya Vyakula
Unaweza kuendelea kula vyakula unavyopenda kama vipande vya keki lakini hakikisha unatumia kwa tahadhari kubwa vitu hivyo vyenye sukari ili visiwe vipingamizi vya kushusha uzito wako.
7. Usiamini kila kitu Kilichoandikwa kwenye Lebo za Vyakula
Lebo zinazosema haina mafuta haimaanishi kuwa kuna kiwango kidogo cha Kalori(Nguvu). Ni sawa na zile lebo zinazosema kiwango kidogo cha sukari(low sugar).
8. Dhibiti kiwango cha Vinywaji vya Sukari unavyokunywa
Unywaji wa soda na juisi za viwandani huongeza utendaji wa kimetaboliki wa mwili na kufanya uzito kuongezeka. Jitahidi kunywa glasi 8 za maji safi na salama ambayo yatasaidia kutoa sumu na uchafu
mwilini.
9. Ainisha vyakula utakavyokula
Kuandika mpangilio wa vyakula utakavyokula kutakulinda na kuhakikisha vyakula vya kutia nguvu unavyokula ni sahihi na pia ni kikumbusho cha kila wakati juu ya ni vyakula gani unahitaji.
10. Kumbuka kufanya mazoezi siku hadi siku
Dakika 30-60 za mazoezi kila siku zitalinda afya yako na kukusaidia kupunguza uzito. Mazoezi ya kunyanyua vitu vyenye uzito ni mazuri zaidi kwa kuwa huchoma Kalori iliyopo mwilini.
- See more at: http://www.fikrapevu.com/njia-kumi-rahisi-za-kupunguza-uzito/#sthash.UzJf98Qv.dpuf

Tuesday, September 17, 2013

Jinsi ya Kupunguza Uzito (1)


Ni matumaini yangu kuwa hamjambo wasikilizaji wapenzi na karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Kama mnakumbuka katika vipindi viwili vilivyopita tulizungumzia unene wa kupindukia na pia katika kipindi chetu hiki tunaendelea kujadili suala hilo ambapo leo tutajadili namna ya kujua kiwango cha kalori za chakula zinazohitajika kuliwa kwa siku ili kudhibiti unene. Karibuni mjumuike nami hadi mwisho wa kipindi.
&&&&&&
Inaonekana kuwa watu wengi hawajui ni kiasi gani cha kalori za chakula tunachotakiwa kula kwa siku. Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya Taarifa ya Chakula umeonesha kuwa, nchini Marekani raia wengi wa nchi hiyo hawafahamu vipimo vya kalori katika vyakula, ambapo katika kundi lililochunguzwa, asilimia 12 tu ndio walifahamu kiwango cha kalori wanachotakiwa kula kwa siku. Asilimia 43 hawakufahamu na 35 walikosea kiwango hicho. Kuna umuhimu mkubwa kufahamu kuwa, tunatakiwa kula kiasi cha kalori sawa na kalori zinazotumiwa na miili yetu ili kudhibiti uzito na kujiepusha na unene. Hata hivyo kuna mambo mengi yanayoathiri kiwango cha kalori kinachotakiwa kuliwa kwa siku kama vile jinsia, umri, uzito, urefu na aina ya kazi na shughuli za mwili. Lakini kabla sijaendelea mbele pengine ningechukua fursa hii kuwafahamisha wasikilizaji wetu maana ya neno kalori. Maana ya kalori kwa mujibu wa fizikia, ni kiasi cha nishati zinazohitajika kuongeza joto la gramu moja ya maji kwa celcius moja. Lakini tukiitafsiri kalori kwa mujibu wa lishe na chakula, ni kiwango cha nishati ya chakula au nguvu inayopatikana kutokana na chakula tunachokula. Kwa msingi huo kwa mfano tunaposema kuwa, mkate una kalori 55, tunamaanisha kwamba, kiasi cha nguvu kinachotokana na mkate ni kalori 55. Kujua maana ya kalori na kiasi cha kalori tunachokula hutusaidia kufahamu ni kiasi gani cha nishati miili yetu inahitajia kwa siku kwa ajili ya mahitaji yake na hivyo kuweza kudhibiti uzito wa miili yetu kwa kutoipatia kalori nyingi zaidi ya mahitaji yake. Suala hilo pia mbali na kuimarisha afya zetu vilevile huzuia unene wa kupindukia tatizo ambalo linazidi kuongezeka kila siku duniani kote.
&&&&&
Wanasayansi wanatuambia kuwa, ratili moja ya mafuta (ambayo ni sawa na karibu nusu kilo)  ni sawa na kalori 3,500, kwa hivyo iwapo mtu atapunguza kalori 500 kwa siku, kwa wiki anaweza kupunguza ratili moja na hivyo kupunguza uzito. Ni vigumu kujua kiasi cha kalori kinachotakiwa kwa siku, kwa sababu kila mtu ana sifa tofauti za kimwili na pia kiwango cha kazi na namna anavyoushughulisha mwili wake. Wataalamu wa masuala ya afya wanatushauri kuwa, ni bora wanawake wale kalori 1,400 na wanaume kalori 1,800 kwa siku. Pia ni bora tusile kalori zinazopungua 1,000 kwa siku, na tuzingatie kazi tunazofanya kwa siku na jinsi tunavyoishughulisha miili yetu. Hii inamaanisha kuwa, ikiwa mtu anafanya kazi ya kukaa chini muda mrefu isiyo nzito na kutoushughulisha sana mwili kama vile kazi za maofisini, ni wazi kuwa kiwango cha kalori anachohitaji kwa siku ni kidogo. Tofauti na watu wanaofanya kazi zinazohitaji nguvu kubwa na zilizo ngumu kama vile kilimo, ujenzi, ukuli na kadhalila ambazo huufanya mwili utumie nishati nyingi. Hivyo watu wenye kufanya shughuli hizo ni wazi kuwa wanahitaji kula kiasi kingi zaidi cha kalori kwa siku. Vilevile ili kudhibiti uzito wa mwili na kujiepusha na unene wa kupindukia mazoezi yanapaswa kuzingatiwa. Hii ni kwa sababu wakati tunapofanya mazoezi miili yetu huchoma kalori za ziada mwilini na hupunguza unene na kuudhibiti.  Hata hivyo, hatupaswi kula kalori chache kuliko mahitaji ya miili yetu na ni bora kutopunguza kalori zaidi ya 500 kwa siku. Hii ni kwa sababu iwapo kiwango cha kalori kitakuwa kidogo kuliko hitajio la mwili, ufanisi wa mwili hupungua na kiwango cha misuli hupungua suala linaloweza kusababisha utapiamlo na matatizo mengine ya kiafya.
&&&&&
Iliyopo hewani ni idhaa ya Kiswahili sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kipindi kilichopo hewani ni Ijuwe Afya Yako. Wasikilizaji wapenzi kwa kuwa baadhi ya wasikilizaji wetu wametuandikia na kutaka kujua namna ya kupunguza unene, tumeamua kuelezea moja ya njia za kupunguza nene au diet plan. Kuna njia nyingi sana ambazo hutumiwa na watu ili kupunguza mwili na tumbo, lakini baadhi huwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanayoishi watu, hivyo watu wengi hushindwa njiani. Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa, chai ya kupunguza uzito na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu na hata baadhi ya wakati huwa na madhara. Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka uzito wa mwili. Tutatoa mfano wa kupunguza uzito kwa muda wa siku 7. Mambo muhimu ya kuzingatia ni kwamba, kupungua uzito kunategemea kiwango cha mafuta mwilini (body fat), uzito wa mtu, kalori anazohitaji kwa siku, BMI yake pamoja na lengo la mtu kutaka kupunguza uzito. Maswali muhimu ya kujiiuliza ni kuwa, je, vyakula ninavyokula hunipa nguvu na uwezo wa kumudu majukumu yangu ya kila siku? Nahitaji kupunguza kiwango cha mafuta mwilini kwa kiasi gani? Kwa mfano wengine wanahitaji kupunguza asilimia 10, 20 au 25 ya kiwango cha mafuta mwilini. Kwa maana hiyo, si kila diet plan humfaa kila mtu, inaweza ikawafaa baadhi na isiwafae wengine.
Jambo lingine la kuzingatia ili kupungua uzito ni kufuata ushauri wa wataalamu wa lishe, madaktari, wataalamu wa mazoezi na kadhalika. Ufuatao ni mfano wa njia ya kupunguza unene au diet plan. Kila siku unahitaji kunywa kikombe kimoja cha kahawa, na ni vizuri kubadilisha unywaji wa kahawa kwa chai, yaani kama leo utakunywa kahawa kesho kunywa chai na kadhalika. Kwa wale wenye ugonjwa wa shinikizo la damu, ugonjwa wa wasiwasi na kadhalika, wanashauriwa kuepuka kahawa kabisa na hivyo wanywe chai. Wagonjwa wa kisukari wanaweza kunywa chai au kahawa kwa kukamulia ndimu au limao ndani yake na hivyo kuongeza ladha.
&&&&&
Siku ya kwanza:
Tembea kwa muda wa dakika 30 asubuhi au jioni kabla ya kula chakula chochote. Kwa wale wenye mashine ya kutembelea ya tredmill wanaweza kutembea kwa muda wa dakika 30 kwa kuanza na kasi ndogo. Unaweza pia kukimbia kwa muda wa nusu saa au kukimbia kwenye mashine ya tredmill kwa muda wa nusu saa. Anza kukimbia kwa kasi ndogo halafu ongeza kasi. Au unaweza kukimbia kwa kasi ya juu kama 8 kwa muda wa dakika 5 na kisha kupunguza hadi 5. Hii inaitwa interval training, yenye lengo la kukupa uwezo wa kufikisha dakika 30, kuchoma mafuta mwilini na kupunguza mapigo ya moyo ili yarudi kwenye kiwango cha kawaida. Hii ni kwa sababu wakati unapofanya mazoezi mapigo ya moyo huongezeka sana na pia kuupa moyo wako uwezo wa kufanya kazi vizuri. Wale wenye matatizo ya kiafya ya mapigo ya moyo au wale ambao walishawahi kuugua hapo awali matatizo ya moyo na wagonjwa wa pumu, ni vyema wafanye mazoezi chini ya uangalizi wa wataalamu wa mazoezi pamoja na kushauriana na daktari. Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) mara 15-20. Ikiona ni vigumu kwako unaweza kuanza hata kwa mara 10 na utakuwa unaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na tumbo. Unaweza kutumia benchi au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups, kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati mmoja. Unaweza ukawa unakunywa huku ukiendelea na mambo mengine mpaka bilauri 4 ziishe. Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini.Mlo wa asubuhi (Breakfast):Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka kijiko kimoja kidogo cha sukari. Yai moja la kuchemsha na kipande kimoja cha mkate wa kawawia au ngano isiyokobolewa (brown bread). Usithubutu kuweka siagi wala kitu kingine chenye mafuta na sukari nyingi. Kula matunda kadri unavyoweza lakini epuka ndizi tamu.Chakula cha mchana (Lunch):Kula robo kuku wa kuchoma au wa kuchemsha na si vinginevyo. Saladiau kachumbari ya mboga mboga tofauti lakini isiwe na sosi ya mayonnaise. Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks au asusa kama vile malai (ice cream) chokoleti, biskuti na kadhalika. Jizoeshe kula matunda kwa wingi kila unapohisi njaa. Jioni tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa pamoja na kufanya mazoezi ya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku. Chakula cha usiku (Dinner):Kulasupu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha. Unaweza kutumia karoti, nyanya au tungule, brokoli,cauliflower, pilipili boga na za kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na thomu na kadhalika epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.
Naam wapenzi wasikilizaji tunaishia hapa kwa leo kwani muda wa kipindi chetu umetutupa mkono. Hadi wiki ijayo kwaherini.

Friday, September 13, 2013

SEMINA YA KAMATA FURSA TWENDZETU KWA VIJANA YAFANYIKA LEO MKOANI DODOMA.


Msanii mahiri wa Kughani Mashairi kwa mtindo wa kisasa kabisa,Mrisho mpoto akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake waliojitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya kamata Fursa twendzetu,iliofanyika ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma. Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Sehemu ya washiriki wa semina hiyo ilipokuwa ikiendelea mapema leo asubuhi.

 Wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo ya kamata fursa twendzetu,mapema leo asubuhi mkoani Dodoma.

 Mwakilishi wa NSSF-Makao Makuu,Salim Khalfan akifafanua masuala mbalimbali yatokanayo na faida za kujiunga na shirika hilo la NSS,ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu iliofanyika mapema leo kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
  Sehemu ya ya watu wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri kwenye semina hiyo.
 Meneja wa  NSSF mkoani Dodoma,Bwa.Kirondera Nyabuyenze akizungumza fursa mbalimbali zitokanazo na shirika la NSSF,Nyabuyenze amewataka watu mbalimbali wajitokeze kwa wingi kujiunga na NSSF,ili kujipatia fursa mbalimbali zikiwemo mikopo,matibabu na mambo mengiyo mbalimbali.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Maxmalipo,Renard Munuri akizungumza kwenye semina ya Kamata Fursa Twenzetu kwa vijana,kuhusiana na masuala mbalimbali yanayofanywa na kampuni yake katika kusaidia huduma za jamii,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya  Africans dream,iliyoko nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Mmoja wa Watangazaji mahiri wa Clouds FM,akizungumzia fursa mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyozifanyia kati na kujipatia sehemu ya  mafanikio katika kupambana na maisha.Semina ya Kamata Fursa twendzetu inayoratibiwa na Clouds Media Group,imekwishafanyika mikoa zaidi ya mitano ikiwemo  Kigoma,Tabora,Singida,Mtwara,Mbeya,Iringa sambamba na leo ndani ya Dodoma,ambo semina hizo zote zimeonesha mafanikio makubwa kwa vijana kwali walikuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye ushiriki.
 Baadhi ya wasanii ambao wamenufaika mara baada ya kujiunga na Shirika la NSSF,shoto ni Queen Doreen na Mwasiti wakijadiliana jambo na mdau Phillipon mapema leo,wakati semina ya Kamata fursa twendzetu ilipokuwa ikiendelea.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kwenye semina ya fursa kwa vijana
 Sehemu ya meza kuu ya watoaji mada wakishangilia jambo.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM.

Sunday, September 1, 2013

MMH:HUYU NDIO MWANAMKE ALIYE WEKA AHADI YA KUFANYA MAPENZI NA WANAUME LAKI MOJA DUNIANI KOTE

...


Mwanamke mmoja raia wa Poland ameripotiwa kuweka nadhiri ya kusafiri katika kila mji duniani katika uchunguzi usio wa kawaida kulala na wanaume 100,000.

Ania Lisewska kutoka mjini Warsaw ameingia katika mpango huo usio wa kawaida kwenye mji aliozaliwa mwezi uliopita na mpaka sasa amefanikiwa kuongeza idadi hiyo kufikia 284, kwa mujibu wa gazeti la Huffington Post.

Lakini wakati rafiki yake wa kiume wa muda mrefu mwenye umri wa miaka 21 akimsamehe zaidi kuliko wote - hajamtosa pamoja na yote hayo - anaeleweka kwamba 'hajasisimuliwa' na wazo hilo.

Ania alisema kwamba rafiki yake huyo amelazimika 'kukubaliana na wazo hilo'.

Alilieleza gazeti la Austrian Times: "Nataka wanaume kutoka Poland, Europe na duniani kote. Ninapenda ngono, kufurahi na wanaume.

"Nchini Poland somo la ngono bado ni haramu na yeyote anayetaka kukidhi matakwa yao ya ngono huchukuliwa kama aliyepotoka, au mgonjwa wa akili."

Ania anasema kwamba atalenga tu kumaliza jukumu lake wakati wa siku za mwishoni mwa wiki na ameanzisha ukurasa wa Facebook na tovuti kusawiri mawazo ya wachimbaji kurasa wake ambao ni kidogo kuliko rafiki yake wa kiume anayevutiwa anaweza asipende kuwasevu kama watu wake muhimu.

Anaongeza kwamba anatarajia kutumia takribani dakika 20 na kila mpenzi mmoja.

Lakini taarifa za tamaa yake ya sasa ya kutaka makuu imeibua mashaka katika uhalalishwaji wake, huku ripoti kadhaa zikisema kwamba inaweza kuwa mzaha.

Kwa mujibu wa ripoti, kufanya ngono na watu wengi kiasi hicho kwa dakika 20 kwa wakati mmoja kunaweza kumchukua Ania miaka mitatu na miezi nane kumaliza kama hakutakuwa na mapumziko kwa ajili ya chakula au kulala.

Akionekana kanakwamba anapanga kuchukua nafasi ya siku za Jumamosi na Jumapili, jukumu hilo litamchukua miaka 20 mfululizo.

Ikichukuliwa anaishi hadi umri wa miaka 81, kufikisha 100,000 Ania atakuwa na hadi kiasi takribani wanaume 16 katika siku zote za mwishoni mwa wiki.