Sunday, October 27, 2013

KINACHOENDELEA KWENYE MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU...MATUKIO KATIKA PICHA


 Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu.



 Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi.


Kajala Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia) wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori jijini Dar.



Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema.



 Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito.


Wema Sepetu akibubujikwa na machozi baada ya kuondokewa na baba yake mzazi.
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu, bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.
  Maudakuextra BLOG  inatoa pole kwa familia yote ya marehemu Sepetu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!

UCHAGUZI UNAOENDELEA WA TFF HALI TETE WAANDISHI WA HABARI WAFUKUZWA UKUMBINI,WASEMA HAWATAANDIKA CHOCHOTE


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa hakuna Mwandishi yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa madai kwamba Waandishi hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu lao ni kusubiria kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo liezua tafrani kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama (Polisi) walipowataka Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto amewataka Waandishi wa Habari kuachana na Uchaguzi huo na kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni dharau kubwa kwa waandishi wa Habari na watanzania wote nchini wanaopenda Michezo.CHANZO MICHUZI JR BLOG

UCHAGUZI TFF WAENDELEA MCHANA HUU WATER FRONT - MALINZI AU NYAMLANI???


UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unafanyika mchana huu kwenye Ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Mchuano mkali unaelezwa upo katika nafasi ya rais, ambapo wagombea Athuman Nyamlani na Jamal Malinzi wanachuana vikali kumrithi rais wa sasa wa TFF, Leodegar Tenga anayemaliza muda wake.
Wagombea wengine katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo; Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais).
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6- Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na Mbeya).
James Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
Wawakilishi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi ambaye ni Ofisa Maendeleo wa kanda hii, Magdi Shams El Din ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ni miongoni mwa wageni watakaohudhuria mkutano huo.

Source:Shafii Dauda

JUST IN: WEMA SEPETU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI, MZEE BALOZI ABRAHAM ISAAC SEPETU


Pichani ni Waziri wa Mambo ya Ndani, DR. William Nchimbi, akimpa pole Balozi Isaac Sepetu alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake September 21, 2013.
Wema (kulia) akiwa na baba yake (kati), kushoto ni meneja wake anayejulikana kwa jina la Petitman.
Balozi Abraham Isaac Sepetu amefariki dunia mapema leo akiwa katika hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi alioupata hivi karibuni mjini Zanzibar. Balozi Sepetu, ambaye pia ni baba mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu, hadi anapatwa na ugonjwa na hatimaye mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar. PICHA: Maktaba/GPL

Msanii wa Injili toka Nigeria ajianika UCHI


     
Mwimbaji wa nyibo za injili toka nchini Nigeria  ajulikanaye  kwa  jina  la  Maheeda  amejikuta  akitengwa  na  kanisa  baada  ya  picha  zake  za  uchi  kuvuja….

Taarifa  zinadai  kwamba kabla  ya  kuanza  kuimba  nyimbo  za  dini, mrembo  huyo  alikuwa  akijihusisha  na  mziki  wa  kidunia ambao  kwa  tanzania  unajulikana  kwa  jina  la  Bongo Fleva

Mhudumu wa baa iliyopo maeneo ya posta jijini Dar anaswa akimnyonya maziwa mteja wake


mhudumu wa baa
Muhudumu wa kiume wa baa moja maarufu iliyopo Posta Jijini Dar hivi karibuni alinaswa akifanya ufuska kwa kumnyonya maziwa hadharani mteja wake wa kike.
 
Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa pia na wahudumu wa baa hiyo  lilitendwa  na  jamaa  huyu  kwa  mrembo  ambaye  alionekana  kunywa  pombe  kupita kiasi , hali  iliyomfanya  asijitambue
 
 1
Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Chambuso alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya menejaa wake kufika na kushuhudia tukio hilo, hali  iliyomlazimu  meneja  huyo  kuchukua   uamuzi  mgumu  wa  kumtimua  kazini

TAZAMA PICHA ZAIDI YA 50 ZA KILA KITU KILICHOJIRI JANA FIESTA DAR, NOMA SANAAA


 
Linah akikatika sambamba na Amin ndani ya Serengeti Fiesta 2013. 

Rachel akilishambulia jukwaa la Fiesta 2013. 
Peter Msechu akifanya vitu vyake stejini. 

Snura 'Mamaa Majanga' akionyesha mbwembwe zake jukwaani. 
Mwanadada Ray C akiwapa raha mashabiki wa Fiesta 2013 waliokuwa 'wamemmis' kwa muda mrefu. 

Msanii Linah akifanya yake jukwaani. 
Umati wa watu ukifuatilia shoo ya Fiesta 2013. 
Mwanadada akitoa burudani kwa maelfu ya mashabiki waliohudhuria Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Leaders Club. 
Msanii Menina akinyanyuliwa juu na wacheza shoo wake. 
Wasanii mbalimbali wakiupamba usiku wa Serengeti Fiesta ndani ya Viwanja vya LeadERS 

 
Angalia baadhi ya picha jinsi moto ulivyowaka Serengeti Fiesta Dar es salaam Jana katika Viwanja vya Leaders 



 





 




 



 

 



 


Friday, October 18, 2013