Thursday, November 14, 2013

Hali ni Mbaya : Rais Museveni wa Uganda AMSALITI Rais Kagame wa Rwanda na kumpa ushauri ule ule uliomkosanisha na Rais Kikwete


WAKATI hatima ya kutiwa saini mkataba wa amani kati ya Serikali ya DRC na waasi waliosambaratishwa wa M23 ikiwa haijulikana, uhusiano wa maswahiba wawili wa eneo la Maziwa Makuu, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda umetikisika baada ya Museveni kumtaka mwenzake huyo azungumze na waasi.

Ni ushauri kama huo aliopewa Kagame Mei mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete ukilenga kuleta na kuimarisha amani Mashariki mwa Congo ndio ulioyumbisha uhusiano kati ya Tanzania na Rwanda, kabla ya Kikwete kuifafanua na kisha kukutana na Kagame jijini Kampala, Uganda Agosti mwaka huu.
  

Kwa mujibu wa mtandao wa AfroAmerica Network, Museveni, baada ya kurejea kutoka kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za SADC na zile za Maziwa Makuu (IGGLR) huko Pretoria, Afrika Kusini wiki iliyopita, alimpigia simu Kagame na kumwambia: “Huenda sasa ni wakati muafaka wa kuzungumza na wapinzani wako wenye silaha.”

Chanzo cha habari cha mtandao huo kimemnukuu mmoja kati ya viongozi wa juu wa Jeshi la Rwanda (RDF), akisema Museveni alimwomba Kagame kuzungumza na waasi hao haraka kabla muda haujapita mara tu Rais huyo wa Uganda aliporejea Kampala Alhamisi iliyopita. 

Mkutano wa pamoja wa wakuu wa nchi za SADC na ICGLR uliofanyika kuanzia Jumatatu wiki iliyopita chini ya uenyekiti wa marais watatu, Joyce Banda (Malawi, SADC), Museveni (Uganda, ICGLR) na wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ulitoa wito kwa M23 kuweka silaha chini. Siku mbili baadaye waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, walishindwa vita na kutangaza kuacha uasi.

Kagame hakuhudhuria mkutano huo, badala yake aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo.

“Ni ushauri tu. Nimerejea kutoka kwenye mkutano na SADC uliojadili amani eneo la Maziwa Makuu. Bahati mbaya inaonekana kwamba karibu viongozi wote wanaamini kikwazo kikubwa cha amani ni kuwapo kwa waasi wa Kinyarwanda mashariki mwa DRC. 

“Hakika suala hili linapaswa kuzungumzwa kwa njia moja au nyingine. Na viongozi hao wanaamini kwamba hili halitatatuliwa bila serikali ya Rwanda kukaa kwenye meza ya usuluhishi na wapinzani wake wenye silaha. Hata mimi ninaamini hivyo, huenda wakati umefika kwako kuzungumza nao,” alinukuliwa Museveni akimwambia Kagame katika mazungumzo ya simu yaliyodumu kwa takriban dakika 15.

Kagame alijibu: “Sitozungumza na FDLR, washiriki wa mauaji ya kimbari. Never, … , ever. Sitozungumza kamwe na wahalifu.”

Hata hivyo, inadaiwa Museveni alimkumbusha Kagame kuwa si waasi wote wa Rwanda walioko DRC ni wanachama wa FDLR au wahalifu  na kwamba wapo anaoweza kuzungumza nao kwa kuanzia.

Baada ya mazungumzo hayo, Kagame aliitisha mkutano wa dharura na washauri wake wakuu na kuwaeleza walichozungumza na Museveni na kuongeza:

Nimekuwa nikiwaambia mara kwa mara kuwa tuko peke yetu. Hata Yoweri, tuliyemwamini kama rafiki yetu na mwenzetu anatugeuka! Leo anatuambia hiki, kesho anakwenda kukutana na viongozi wengine na kutubadilikia.

Baadaye akawataka washauri hao kuja na mpango mkakati wa nini cha kufanya wakati huu Rwanda ikizidi kutengwa na nchi za Afrika na hata za nje ya Afrika.

Mwanzoni mwa mwezi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na mwenzake wa Uingereza walimwonya Kagame kuachana mara moja na ushiriki wake kwenye machafuko ya mashariki mwa DRC, ikiwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja kwa wakubwa hao kutoa onyo kama hilo. 

Wakati hayo yakiendelea, zipo taarifa kwamba Rais Museveni amepanga kutuma ujumbe nchini kuja kuzungumzia mustakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaambia Watanzania kwamba Tanzania haijakiuka chochote katika makubaliano ya msingi, ila wenzetu hao ndio huenda wana ajenda yao.

Kauli ya Kikwete ilihitimisha hali ya wasiwasi wa Tanzania kujitoa EAC na iwapo ujumbe wa Uganda utakuja, itakuwa ni mwendelezo wa kilichofanywa mwishoni mwa wiki na Kenya waliomtuma Waziri wa Mambo ya Nje kuja Dar es Salaam kuweka mambo sawa.

>>>Hali nchini Kenya

Mapema wiki hii, aliyekuwa Mwanasheria wa Serikali ya Kenya, Amos Wako ambaye pia ni Seneta wa Bisia alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha kuwa EAC haisambaratiki, akidai kuwa watakaoumia zaidi ni Wakenya.

Wako aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara pamoja na Mbunge wa Budalangi, Ababu Namwumba, alisema wakati jumuiya ya awali ilipovunjika mwaka 1977, Wakenya wengi waliokuwa wakifanyakazi nje ya nchi ndio walioathirika zaidi.

“Wapo watu mashuhuri kama Raila Odinga na Kalonzo Musyoka wanaokubalika ndani na nje ya nchi ambao kama Uhuru anataka wanaweza kumsaidia kuzungumza na Rais Kikwete wa Tanzania. Hatutaki jumuiya hii ivunjike, si busara hata kidogo,” alisema Wako.

-Mtanzania

NAOLEWA TU SABABU YA MIMBA YAKE ILA SIMPENDI HATA KIDOGO...!!

 
Nipo chat room ya one of social media.........nimemeet na binti mmoja rafiki yangu sana wa enz izo za kombolela kijijini

bint ni mjamzito sasa na mipango ya ndoa inaendelea.........katka kumdodosa anadai hakumpenda jamaa ila tu anaolewa kwa ajili ya ujauzito wake aliobeba na kutunza heshima yake na familia........what a looser

nimejaribu kumshauri ni bora akapange nyumba aishi na mwanae rather than comitting such a serious comitment with a fake heart..kagoma katakata


vikao vinaendelea pale msimbazi center vya sendoff August.....mfike bila kukosa Jumapili saa tisa unusu na michango yenu....mwisho wa mwezi huu..
 

Sunday, November 3, 2013

MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA UCHI HUKU AKIWA AMESHIKA KOPO LENYE MAVI NA DAWA HUKO BUNDA....


(Picha  ya  Maktaba.)

JESHI la Polisi wilayani Bunda, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wenye hasira kali waliotaka kumuua mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Cha Nyerere katika mamalaka ya mji mdogo wa Bunda.
 
Mwenyekiti wa mtaa huo, Maxmilian Bwire, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 10 usiku nyumbani kwa mwanamke huyo, Sarafina Nyamboko, maarufu kama mama Nyamboko.
Alisema kuwa siku ya tukio mama huyo alikutwa na mpangaji wake, Robert Msilimu, akiwa uchi wa mnyama na kopo tupu la amboni lita tano, lililodaiwa kuwa na dawa ambayo alikuwa ameimwaga katika kila mlango wa wapangaji wake.
 
“Baada ya kumhoji alisema alikuwa anawamwagia dawa ya baraka wapangaji wake kwani kila tarehe moja huwa anafanya hivyo ili waweze kupata baraka kwa Mwenyezi Mungu.
 
“Dawa hiyo inaonekana ilikuwa imechanganyikana na kinyesi maana mji mzima ulikuwa unanuka kinyesi,” alisema mpangaji huyo ambaye alimkuta mwenyenyumba wake akifanya mchezo huo.
 
Alifafanua kuwa kitendo hicho kilimshtua sana ndipo alipowaamsha wapangaji wenzake ambao waliamua kupiga yowe na majirani walifika na silaha mbalimbali za jadi na kuanza kumshambulia.
 
Alisema kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa huo, walipiga simu polisi ambao walikuja na baada ya kukuta hali ni mbaya, waliamua kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao na kumchukua mama huyo kwenda naye kituo cha polisi.
 
Hata hivyo, baadhi ya majirani walidai kuwa hii ni mara ya tatu sasa kwa mama huyo kukutwa anafanya mchezo huo na kwamba hata kwenye mikutano ya hadhara ya mtaa huo, ameshaonywa mara kwa mara lakini alikuwa hajaacha.
 
Polisi walisema kuwa wanaendelea kumhoji kwa kina kuhusu kitendo hicho cha kukutwa uchi na pia kufahamu ukweli wa dawa hiyo aliyokutwa nayo.
 
Kama ikithibitika kuwa kuna kosa ndani yake watamfikisha kwenye mkondo wa sheria.
-Tanzania  Daima

HATARI KWA DIAMOND AUTIBUA MSAFARA WA RAIS!!

Stori:IMELDA MTEMA
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,

Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.

Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham Sepetu.

DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.

AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu.

MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein.

Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke ndipo waombolezaji wengine watawanyike.

“Jamani naomba sana itifaki izingatiwe, asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo.

DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.

Lakini kabla Rais Shein hajaanza kusimama, Diamond alinyanyuka na kuzua kasheshe kwa sababu baadhi ya watu, hasa wa umri wake walianza kumkimbilia huku wakikanyagana na kusababisha hali ya taharuki.

MC AWATULIZA WATU
Baada ya watu kuanza kukimbizana hovyo muongozaji wa msiba huo aliwaomba watulie na kusema kuwa wasiogope ila kuna staa ambaye anapita ndiyo maana watu wamemkimbilia.

“Naomba utulivu huyo ni staa f’lani kapita huko ndiyo maana watu wanamkimbilia hivyo tulieni kwanza viongozi wetu waondoke,” alisema.

USALAMA WA TAIFA NUSURA WAMKAMATE
Baada ya kuona watu wakikimbia hovyo baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa walitaka kumkamata msanii huyo wakisema alisimama kwa makusudi licha ya kusikia tangazo la kiitifaki.

WATU WAMSHANGAA DIAMOMD
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walionekana kushangazwa na kitendo cha Diamond na kusema kuwa ni vyema angesubiri viongozi wote waondoke ndipo na yeye atimke lakini kufanya vile si sahihi.

“Huyu Diamond kwani ana nini? Nakumbuka kwenye msiba wa Kanumba kule Dar pia aliingia kipindi ambacho ilitangazwa kuna kiongozi anakwenda, utaratibu ukatibuka, watu wakawa wanamshangilia yeye,” alisema mtu mmoja aliyetoka Dar kwenda Zanzibar kumzika

Friday, November 1, 2013

Busy - Masanja Mkandamizaji

http://www.youtube.com/v/CE_GLCA4ceQ?autohide=1&version=3&feature=share&autohide=1&showinfo=1&attribution_tag=CQ7as_725UM5MeWAQMF7Kg&autoplay=1

PICHA,RAHA YA UTOTO,MTOTO AKALIA KITI CHA PAPA NA KUGOMA KUONDOKA

Mtoto wa kiume aliyepata utambulisho wa nguo aliyokuwa amevaa ‘the boy in yellow’ alijikuta anachukua ‘attention’ ya waumini wote waliohudhuria siku ya familia St Peter’s Square huko Vatican baada ya kuvamia jukwaani na kukaa na papa Francis kwa muda wa dakika kadhaa.
Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis alikuwa akizungumza mbele ya umati mkubwa wa familia mbalimbali zilizohudhuria sherehe za siku ya familia. Baada ya mtoto huyo kupanda jukwaani alienda mbele ya papa na kumtazama na kuzunguka hapa na pale japo hakufanya fujo ya aina yoyote.
 
Makadinali walijaribu kutumia njia za kumshawishi kutoka kama kumpatia pipi, lakini mtoto huyo aligoma kuondoka. Papa alimgusa kichwani na kutabasam akamwacha na kuendelea na alichokuwa akikifanya.
Kuna wakati papa akiwa amesimama anazungumza mtoto huyo alimkumbatia miguu lakini papa alimwacha.
Baadaye Vatican walishare moja ya picha za tukio hilo katika akaunti yao ya Instagram ikimwonesha mtoto huyo akiwa amekalia kiti cha papa na kuandika ‘A special guest with #popefrancis.
Source: Mail Online

MAMBO 4 MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA KUFANYA TENDO LA NDOA!!!! YATAMBUE HAPA SI YA KUKOSA HII.....


Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia.
 Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi.  Nawakaribisha sana
 
Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia. 
Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa.
 Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.

Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.
Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.

Kuoga pamoja
 
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.

Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha? 
Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.

Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.

Kusifiana
 
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako. 

Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.

Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.
Kuelekezana
 
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika.

Zungumzieni maisha
 
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla.

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa. 
Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu.

MAONESHO YA WAJASILIAMALI MTWARA

Maonesho ya WajasiriaMali Mtwara

Maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiria mali kutoka pande mbalimbali za nchi na  nchi jirani yamenza mjini Mtwara. Maonesho hayo yaliyoandaliwa na SIDO na wadau wenzi, yanalenga kuonesha bidhaa anuwai zitengenezwazo na wabunifu na pia kutafuta masoko toka kwa wadau. Mkoa wa Mtwara, ambao umesikika masikioni mwa wadau wengi hivi karibu kufuatia kugunduliwa kwa gesi asilia, unaanza kuwa moja ya masoko makubwa tarajiwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Maonesho haya ambayo yamefunguliwa rasmi na ndugu mwenye dhamana ya viwanda vya Tanzania, ni fursa nzuri ya kuweza kuonesha bidhaa na mwanzo mzuri ya viwanda vyetu wenyewe kuanzia hatua za mwanzo kabisa. Kupitia wadau hawa wa bidhaa hizo ndogo, Taifa linaweza siku za usoni, kama tutaweka mkazo wa kutosha, kuwa na viwanda vyake lenyewe. Ili tuweze kufikia ndoto na lengo hilo ni muhimu kutengeneza mazingira ya kuwawezesha wajarisiliamali wetu kutengeneza bidhaa zao kwa gharama nafuu. Gharama za uzalishaji ikiwa ni pamoja na mali ghafi zikiwa  na bei ya chini, itawezesha wadau wengi kujiajiri na bidhaa zao zitakuwa na bei ya chini.

Nasema hivyo kwa kuwa baadhi ya bidhaa nilizoziona zinauzwa kwa bei kumbwa mno ukilinganisha na ubora wake. Bidhaa  nyingi ni za asili kabisa na hivyo kuwa imara ukilinganisha na zitangenezwazo na makanjanja mjini, japokuwa ubora wake unahitaji kuongezwa zaidi ili zivutie wanunuzi wengi zaidi. Nilipohoji juu ya bei mmoja wabunifu wa bidhaa alisema: "nalazimika kuuza kwa bei ya juu kwa sababu nalipia kodi na  ushuru mbalimbali na pia kwa kuwa hakuna watazamaji wengi nauza bei ya juu ili kupitia mauzo haya nijikimu hapa mjini". Baadhi ya wadau hawa wa bidhaa asilia waliomba waandalizi wa maonesho haya wafikilie kuwalipia baadhi ya gharama ili kumudu vyema zaidi maonesho hayo. (Mwandishi hakupata fursa kuongea na timu ya maandalizi juu ya suala hili)

Wakazi wa mjini Mtwara, hawajahamasika vya kutosha kutembelea maonesho hayo, jambo ambalo lingewezesha wajasiriamali kuuza bidhaa zao na kumudu kujikimu kupitia mauzo hayo. Hata hivyo ni fursa kwa wenyeji wa mkoa huo kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na maisha na utawala wa mazingira ya binadamu.

Kwa wajasiria mali, napenda kuwapongeza kwa kazi nzuri wanazozifanya, ila nawashauri pia waweke vitambulisho vya nchi zao wanakotoka ili kutambulisha bidhaa zao na pia kuzitambulisha nchi zao kibiashara zaidi. Hili linajumuisha kundika kwenye bidhaa jina la nchi bidhaa ilikozalishwa, kundika anuani  ama utambulisho uliojitosheleza ili mdau husika apatikane kwa wepesi kokote duniani. Ni muhimu kufanya hivyo kwani dunia imekuwa ndogo mno kupitia mapinduzi ya mawasiliano ulimwenguni.
SOURCE:Wajenga nchi by Martin Mandalu