Saturday, December 29, 2012

KESI YA LWAKATARE: TUNDU LISU AMLAUMU "ISSA MICHUZI" NA " MWIGULU NCHEMBA"



Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki  (CHADEMA), Tundu Lissu akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu leo amefanya mkutano wa wanahabari. Katika mkutano huo, Lissu ameongea yafuatayo:

1. Atafungua kesi Mahakama kuu kuiomba iiamuru Mahakama ya Kisutu kuendelea kusikiliza kesi ya awali iliyofutwa na DPP katika kesi inayomhusu Lwakatare kwani DPP amevuka mipaka yake inayomruhusu kufuta kesi na isitoshe kesi aliyofungua ni ile ile hivyo Mahakama iamuru shauri la awali liendelee.


2. Kuhusu video iliyoonyeshwa kwenye mitandao Lissu anasema kuna mashaka makubwa sana kuhusiana na video ile na kisheria kesi hiyo ikifika mahakamani haitachukua hata nusu saa ataibuka mshindi.
Lissu anasema
- Hakuna mtu anayepanga mauaji katika hadhara mahali ambapo watu wanapitapita kama inavyoonekana kwenye video ile.


-Lwakatare kama alirekodiwa basi lazima ielezwe je ilikuwa ni kwa hiari yake kama si hivyo ni makosa


-Issa Michuzi Mpiga picha wa Rais alikuwa akipongezana na watu wa Ikulu wenzake kuwa TISS (Usalama wa Taifa) wamefanya kazi nzuri kwa kurekodi ile video. Kisheria usalama wa taifa hawatakiwi wala hawaruhusiwi kurekodi au kuvifanyia ushushu vyama vya siasa kwa maslahi ya Chama tawala.


-Ludovick baada ya kukutana na Lwakatale tarehe 28 Desemba mwaka jana saa 5 muda mfupi baadaye yaani saa 5:59 alimpigia simu Mwigulu Nchemba kwa kutumia namba ya simu ya Mwigulu ambayo ameiandikisha kwenye kumbukumbu na vitabu vya Bunge Lissu anadai wana rekodi ya mazungumzo yao.


-Siku iliyofuata tarehe 29 Desemba mwaka jana akiwa kwenye kipindi cha Tuongee asubuhi cha Star TV alidai ana mkanda wa video unaowaonyesha CHADEMA wakipanga mauaji.


-Pia amedai itabidi waambiwe video hiyo imerekodiwa studio gani, maneno gani yameondolewa na yapi yameongezwa.


Anamalizia kwa kusema walianza kwa kusema CHADEMA ni chama cha familia wakashindwa, wakasema ni chama cha wachaga wakashindwa, wakesema ni chama cha wakatoliki wakashindwa, wakasema ni chama cha wakristo wakashindwa, wakasema ni chama cha ukanda wakashindwa leo wanasema ni chama cha kigaidi WATASHINDWA.


(Picha / Habari na Kurugenzi Ya Habari Chadema)

MAELFU WAANDAMANA KUPINGA GESI KUTOLEWA MTWARA


MAELFU ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara jana waliandamana wakipinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka hapa kwenda Dar es Salaam.


Maandamano hayo ambayo yaliwashirikisha wananchi wa wilaya za mkoa huu zikiwamo Tandahimba na Newala, yalianzia katika Kijiji cha Mtawanya hadi Mtwara mjini kupitia barabara ya kwenda Msimbati eneo ambako gesi asilia inapatikana.

Waandamanaji hao waliotembea umbali wa kilomita sita, walitoa maazimio tisa mojawapo likihoji sababu za mitambo ya kuzalisha umeme kutojengwa Mtwara ambako ni jirani na inakochimbwa gesi hiyo.

Katika tamko hilo lenye kurasa mbili, waandamanaji hao wamesema Serikali haijaweka wazi namna gani wakazi wa Mtwara watanufaika na gesi hiyo, huku tayari Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshazindua ujenzi wa bomba kwenda Dar es Salaam. Wametaka ujenzi huo usitishwe.

Pia wamesema uamuzi wa kupeleka gesi Dar es Salaam unapingana na tamko la Rais Kikwete alilolitoa kwenye ziara yake mkoani hapa mwaka 2009 kwamba ujiandae kuwa ukanda wa viwanda.

Aidha, wanataka vinu vya kuzalishia gesi vijengwe Mtwara kwa kuwa wanayo maeneo ya kutosha ya ujenzi huo tofauti na Dar es Salaam.

“Tunahitaji viwanda vikubwa vijengwe Mtwara ili kuleta ajira kwa wakazi wa Mtwara na mikoa ya jirani, tuna hofu kutokana na ilivyokuwa kwa wakazi wa Songongo (Lindi) kubaki maskini wakati gesi inazalishwa hapo, yasije yakatukuta sisi, hivyo ni lazima tusimamie rasilimali hii ili iweze kuleta maendeleo,” walisema katika azimio lao.

Wamesema pia kwamba Serikali haijaeleza athari zitakazopatikana kutokana na uchimbaji wa gesi katika eneo hilo na namna itakavyoweza kusaidia kuziondoa, huku wakitaka gharama za uunganishaji wa umeme wa nyumbani zisizidi Sh50,000 ili kila mwananchi aone ananufaika na gesi hiyo.

Waandamanaji hao wamesema gharama za mradi huo wa kusafirisha gesi hadi Dar sa Salaam ni kubwa, hivyo wakashauri Serikali ichimbe gesi ya Dar es Salaam katika kisima namba 7 ili kuepuka hasara.

Katika azimio lao la mwisho, wamemwomba Rais Kikwete kumwondoa madarakani Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia kwa madai kwamba amewakashifu kutokana na madai yao ya kupinga gesi kwenda Dar es Salaam.

Ilielezwa kuwa, awali Simbakalia aliombwa kuwa mgeni rasmi katika maandamano hayo, lakini alikataa na badala yake yalipokewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Siasa, Hussein Mussa Amiri.

Desemba 21, mwaka huu katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara (RCC), kilichoketi kwenye Ukumbi wa Boma, Simbakalia alisema hawezi kushiriki katika maandamano hayo.

Maandamano hayo yaliratibiwa na vyama vya siasa vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Sau, TLP, APPT Maendeleo, ADC, UDP na DP, yakiwa na kaulimbiu ya ‘gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu.’ Kutokana na maandamano hayo, Soko Kuu la Mtwara lilifungwa kwa muda kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kushiriki na barabara kadhaa zilifungwa kwa muda.

Mbali ya watu kujitokeza kwa wingi, pia walibeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.

“Bandari Bagamoyo, Viwanda Bagamoyo, Gesi Bagamoyo, Mtwara wapuuzi?.... Gesi haitoki hata kama hatujasoma.... Gesi kwanza vyama baadaye, hapa hakitoki kitu.... Kusini tumedharauliwa vya kutosha sasa basi.”

Akisoma tamko la vyama hivyo, Katibu wa umoja huo, Seleman Litope alisema kwa muda mrefu Kusini imekuwa ikiondolewa fursa mbalimbali za maendeleo.

Alitoa mfano wa kung’olewa kwa reli, ukosefu wa usimamizi mzuri wa zao la korosho, ukosefu wa miundombinu ya barabara, kuondolewa kwa Mradi wa Maendeleo ya Ukanda wa Mtwara (Mtwara coridor) na hilo la gesi.

Alisema hali hiyo imesababisha mikoa ya Kusini kuwa nyuma kimaendeleo na kwamba umoja wao unalenga kuhakikisha rasilimali yao hiyo haitoki kwenda kokote kabla ya kuwanufaisha.

TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU-ASILIMIA 90% YA VIONGO...

: TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU-ASILIMIA 90% YA VIONGO...: TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKUTANO MKUU WA NNE WA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA (TCF) TAMKO RASMI “ATUKUZWE MUNGU JUU MBINGUNI,...

Wajenzi wa Dunia: SIKU YA JUMUIYA SAUT - Mtwara

Wajenzi wa Dunia: SIKU YA JUMUIYA SAUT - Mtwara: Sehemu ya kwaya ikiongoza maandamano ili kuanza ibada. Naam waimbaji walipendeza hasa!

MPAMANO WA MH.MBILINYI NA MH.MLUGO

SAKATA LA NAIBU WAZIRI WA ELIMU KUWA NA ELIMU FEKI PAMOJA NA JINA FEKI LACHUKUA SURA MPYA.....!!!




NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw. Philipo Mulugo, amesema yupo tayari kumthibitishia Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bw. Joseph Mbilinyi, maarufu 'Sugu', juu ya elimu aliyonayo kama alivyodai mbunge huyo.

Bw. Mulugo aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na Majira kuhusu madai ya Bw. Mbilinyi ambayo ameyatoa katika vyombo vya habari kuwa, Waziri huyo ana elimu ya kuunga unga na jina lake kamili ni Amim.

Alisema kauli ya Bw. Mbilinyi haina ukweli wowote bali yeye ni msomi na yupo tayari kuthibitisha ukweli huo kwa umma.

“Mimi na Bw. Mbilinyi tuna vilema vingi, akitaka tuumbuane yatabainika mengi hasa katika upande wake, namfahamu muda  mrefu kwa sababu nimesoma naye shule moja, nafahamu mambo yake mengi lakini kutokana na hekima zangu sihitaji malumbano na yeye,” alisema Bw. Mulugo.

Alidai kumshangaa Bw. Mbilinyi, kuzungumzia jambo ambalo halifahamu lakini kwa kumsaidia ili asielendelee kuonekana mwanasiasa muongo, aitishe mkutano na waandishi wa habari na yeye atakuwa tayari kuthibitisha elimu yake kwa umma.

Bw. Mulugo aliongeza kuwa, ni kweli wakati anasoma alikuwa akitumia jina la Amim na baada ya kufika elimu ya juu alianza kutumia jina la Philipo ambalo ni la ukoo ambapo Bw. Mbilinyi kama angekuwa makini, angefuatilia kwenye ukoo wake ili kujua jina hilo linamuhusu au la.

Aliongeza kuwa, dhamira yake ni kuhakikisha kuwa Jimbo la Mbeya Mjini ambalo hivi sasa linashikiliwa na Bw. Mbilinyi, mwaka 2015 linarudi CCM na ukweli huo utathibitika katika uchaguzi.

Mimi ni Waziri kutoka CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu NEC, hivyo Bw. Mbilinyi, asifikiri kuzua maneno hayo yatanitisha hadi nishindwe kutekeleza sera za chama changu,” alisema.

Alisema ibara ya 5 ya Katiba ya CCM, inamwongoza kuhakikisha chama chake kinashinda uchaguzi wa dola wa ngazi zote pamoja na kulirudisha jimbo la Mbeya Mjini kutoka upinzani.

“Katika Uchaguzi Mkuu ujao, nitatumia nguvu zote kuhakikisha jimbo la Mbeya Mjini linarudi CCM, ninachoweza kumshauri Bw. Mbilinyi,  ajifunze kutokana na makosa kwani ameanza kunitafuta siku nyingi lakini mimi sikuwa na muda wa kumjibu bali niliendelea kutekeleza majukumu niliyonayo,” alisema.

Alisema Mbunge huyo na chama chake walijibiwa na wananchi wa Saza katika mkutano wa CHADEMA uliofanyika katika Wilaya ya Chunya na kusahau kilichowapeleka ni kampeni hatimaye wakaanza kunadi elimu ya Mulugo badala yake waliambulia kufukuzwa.

Aliongeza kuwa, Bw. Mbilinyi alipaswa kulisema na hilo kama walifukuzwa na wananchi wa Saza ambao walimwambia wao, wanamfahamu viziri Bw. Mulugo na wamemsomesha wenyewe kwa pesa zao baada ya kuthibitika ni yatima.

Alisema wananchi hao walidai kuchoshwa na matusi ya Bw. Mbilinyi dhidi yake na kumtungia uongo lakini yeye hana
muda wa kulumbana naye bali atamjibu kwa ushahidi.

Kauli ya Bw. Mulugo imekuja siku chache baada ya Bw. Mbilinyi kudai kuwa, elimu ya Waziri huyo ni ya kuunga unga kwani alisoma naye Sekondari ya Mbeya Day, wakati huo akiitwa Amim si Philipo Mulugo hivyo kuanzia sasa ataendelea kumuita jina lake halisi na kusisitiza hana uwezo wa kumng'oa jimboni kwake.
UGOMVI ULIANZIA KWENYE HII HOTUBA

Acky: TUTAKUFA KAMA IFUATAVYO .. UKIMWI NI HATARI

Acky: TUTAKUFA KAMA IFUATAVYO .. UKIMWI NI HATARI: KINACHOONEKANA kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa ...

WANASOCIOLOGIA STEMMUCO

 Wanachuo wa Stella Maris Mtwara Universty College wakiwa katika hospital ya mkoa Mtwara Ligula walipoenda kufanya usafi na kutoa baadhi ya zawadi kwa wagonjwa

 

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA




HAWA NI WANANCHI WA MTWARA WAPO KATIKA KIBARUA CHA KUTAFUTA MAISHA BORA LAKINI ASLIMIA KUBWA YAO NI WANAWAKE.HII INATUONESHA KUWA WANAUME WENGI WA MIKOA YA KUSINI HAWAJISHUGHULISHI NA KAZI NGUMU WANAWAACHIA WAKE ZAO.





Utafiti: Nguo za ndani zachangia ugumba

Utafiti: Nguo za ndani zachangia ugumba: TAFITI za kisayansi zimebaini kuwa nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbe...

Hii ndo treni itayokuwa na wapenzi wa clouds FM kw...

 Hii ndo treni itayokuwa na wapenzi wa clouds FM kw...: Kuwa sehem ya safari kwenda Moro tiket zinapatika kwa Shs 70,000 kwa kaaida na 100,000 kwa V.I.P nI Kesho tarehe 29 Dec 2012 .. hYO NI...

MAAJABU YA DUNIA

MAAJABU YA DUNIA NYATI AZAA BINADAMU


KATIKA hali ya kustaajabisha, nyati anayefugwa na raia mmoja anayeishi nje kidogo ya Jiji la Bangkok nchini Thailand amezaa kiumbe kinachofanana na binadamu kwa asilimia 80.
Mashuhuda walisema kiumbe hicho kilichozaliwa hivi karibuni, kuanzia kichwani kwenda hadi tumboni ni mwonekano wa kibinadamu.
Hata hivyo, miguu na mikono yake ina kwato kama za mama yake ambaye ni nyati lakini kichwani hakuna  pembe.
Tangu kusikika kwa tukio hilo, umati kutoka sehemu mbalimbali za jiji hilo umekuwa ukifika nyumbani kwa mfugaji huyo ambaye hakutajwa jina kwa lengo la kutaka kushuhudia ‘laivu’ tukio hilo la ajabu na hivyo kuzua taharuki.
“Kutokana na wingi wa watu kufurika, polisi waliitwa ili kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu na watu walitawanywa huku wakisema mfugaji huyo ndiye pekee anayejua kilichosababisha mnyama huyo kuzaa kiumbe kinachofanana na binadamu,” alisema shuhuda mmoja. Taarifa zinasema, kiumbe hicho mara baada ya kuzaliwa hakikuchukua muda mrefu kikafa. Hili ni moja ya tukio la ajabu linalotajwa kutokea duniani.