DONDOO MUHIMU KUHUSU KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU KILICHOENDESHWA NA WAZIRI MKUU HUKO MTWARA
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya
Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu
mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013
------------------
Waziri
Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya
wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na
dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia.
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake...
Taarifa mpya zitawekwa hapa punde
zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha
Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika
kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau.
Sikiliza Mtwara na Waziri Mkuu - PRIDE FM
--------------
UPDATES/TAARIFA MPYA za ziara ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana
na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara
vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya
Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho.Dondoo muhimu:
- Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar
- Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye
- Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa.
- Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
- Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar
- Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu
- Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa)
- Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa
- Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu
No comments:
Post a Comment