CHAMA CHA KUTETEA HAKI ZA WANAUME TANZANIA (TAMRA)
 KATIBU WA UHAMASISHAJI WA TAMRA TAIFA BWANA HATIBU MGEJA AKIWA NA MWEKA HAZINA WA TAMRA TAIFA BWANA JUMA KOMBO
TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION
Equal treatments for all
UTANGULIZI
TAMRA ni Asasi ya kiraia iliyoanzishwa na wanaume wa Tanzania kwa lengo 
la kutoa msaada wa Kisheria pamoja na Elimu ya Haki na Wajibu katika 
mahusiano ya kindoa kati ya mwanamke na mwanaume.
Kuanzishwa kwa asasi hii 
kumekuja katika kipindi hiki baada ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa 
wapo wanaume  wengi wanaofanyiwa vitendo vya ukatili katika masuala ya 
ndoa kwa kunyimwa haki zao za kindoa kutupiwa virago pindi mwanamke 
anapoamua kumchoka mwanamme kufuatana na kukosa kipato, kupungukiwa 
nguvu za kiume na mambo kama hayo , jambo ambalo limeonekana kuwa ni 
chanzo cha migogoro katika ndoa inayosababisha ongezeko la watoto 
wanaoishi bila wazazi wa pande zote mbili yaani  [ Baba na Mama] huku 
hali hii ikiigharimu jamii na wanandoa kupigana na kusababisha majeraha 
na mauaji katika jamii.
Si hivyo tu Mwanamme wa 
Tanzania amekuwa ni mvumilivu kwa vile amekuwa akitendewa mambo yote 
haya bila kuwa na chombo cha kukemea vitendo hivi jambo lililotoa 
ushawishi kwa waanzilishi wa chama hiki kupata uchungu na hatimaye 
kuamua kuanzisha Asasi hii.
Muda mrefu mwanaume wa 
Tanzania hakupata wapi  pa kwenda kupata msaada wa kisheria, imefika 
wakati wanaume kuwa na  chama cha kuwatetea dhidi ya unyanyasaji kutoka 
kwa wake zao katika nyanja mbali mbali ikiwemo mambo ya ndoa,urithi wa 
mali kwa wagane, pamoja na ulezi wa watoto.
TAMRA kinaenda mbali katika kuelimisha wanaume juu ya haki zao za msingi
 pamoja na kuwaelimisha juu ya wajibu wao kama baba katika kuitunza 
familia yake,kuondoa mfumo dume na mfumo jike, kupiga vita unyanyasaji 
kwa mke na watoto,urithi wa mali kwa wajane na wagane pamoja na kulea 
watoto kabla na baada ya kufariki kwa wanandoa.
Jina la asasi: Asasi hii itajulikana kuwa ni Chama cha kutetea haki za 
wanaume Tanzania/Tanzania Men’s Rights Association kwa kifupi TAMRA
(1) Kuanzishwa kwa TAMRA:
Asasi  ya TAMRA ilianzishwa 01/05/2012
(2) Makao Makuu.
Makao makuu ya TAMRA 
yatakuwa katika Mtaa wa Mpakani ‘A”Kijito Nyama Jijini Dar Es Salaam 
kituo cha Afrika sana Nyumba Block namba 45.
vile vile kutakuwa na ofisi ndogo ya Makao Makuu Jijini MWANZA
(3)  Anuani ya Chama ni. Chama Cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania.
    S.L.P 60065
   Dar Es Salaam - Tanzania
    Simu: Mwenyekiti TAMRA TAIFA +255 784 203 556
             Katibu Mkuu TAMRA TAIFA +255 787 565 533
    Blog:   yetu ni  www.tamratanzania.blogspot.
TAFSIRI
“TAMRA” itamaanisha ni TANZANIA MEN’S RIGHTS ASSOCIATION.
       KUTAKUWA NA VIONGOZI WAFUATAO WA TAMRA
·         Kutakuwa na Mwenyekiti wa TAMRA Taifa.
·         Katibu mkuu wa TAMRA Taifa.
·         Mweka Hazina wa TAMRA Taifa.
·         Katibu wa Uhamasishaji wa TAMRA Taifa.
·         Wajumbe wa Bodi ya TAMRA 
KAZI ZA TAMRA.
TAMRA itakuwa na kazi zifuafuatazo:
(1)  Kutetea wanaume dhidi ya unyanyaswaji katika ndoa.
(2) Kutoa elimu juu haki za Wanamme
(3) Kuwaelimisha wanamme kuondokana na mfumo dume/jike.
(4) Kuelimisha
 wanaume kuhusu haki na usawa kati ya mwanamme na  mwanamke katika kutoa
 maamuzi kwa mambo mbalimbali ya kifamilia, kisiasa na kiuchumi.
(5) Umiliki wa mali katika familia.
(6) Haki ya kushiriki na kufurahia ndoa.
(7) Kuelimisha jamii juu ya Haki ya kumiliki mali kwa pamoja kabla na baada ya kifo cha mmoja wa wanandoa.
(8) Kuelimisha
 wanandoa kuhusu Haki na wajibu wa kuheshimiwa na kupendwa kwa 
kila  mwanandoa kama ilivyo katika maandiko matakatifu bila kuathiri 
itikadi za dini.
(9) Kuhakikisha
 kwamba TAMRA inashirikiana na  taasisi za kutetea haki za wanawake ili 
kuondoa imani potofu dhidi ya mwanamme ili kujenga mahusiano mazuri 
katika familia badala ya kuchochea uhasama kwa kumkandamiza mwanamme 
kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ndani ya familia.
10.kuhakikisha kuwa kuna 
usawa na uhuru wa kujieleza pindi mashauri ya ndoa yanapopelekwa katika 
vituo vya Polisi kwa uchunguzi na hatimaye hatua ya kupelekwa  katika 
vyombo vya maamuzi.
11.Kuhakikisha kuwa wapo 
Mawakili wa kutosha panapotokea mashauri katika Mahakama watakaotetea 
Haki za Wanaume   ili kuhakikisha Haki inatendeka
MALENGO YA TAMRA.
TAMRA itakuwa na malengo kama ifuatavyo:-
(1)  Kupigania Haki za mwanaume katika masuala mbalimbali ikiwamemo kulinda na kudumisha ndoa.
(2) Kulinda Haki ya mwanaume ngazi ya familia ,kitaifa na kimataifa.
(3) Kuelimisha waathirika wa unyanyasaji
(4) Kutoa msaada wa kisheria Bure kwa kutumia mawakili wa TAMRA.
(5) Kutoa
 elimu ya Afya na malezi ya mtoto wa kiume ili akue katika maadili 
yanayozingatia haki sawa kwa wote kuondoa dhana ya mfumo dume.
(6) Kutoa elimu juu ya magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa yasiyokuwa na tiba ikiwamo Ukimwi (HIV/AIDS).
(7) Kutoa elimu na mafunzo kwa wanamme ili kuwafundisha ujasiria mali kuondoa  utegemezi .
(8) Kufanya upatanishi na usuluhishi kwa wanandoa kwa kuzingatia mila,Desturi,Dini pamoja na sheria za Nchi.
(9) Kutoa elimu kwa wanaume kukubali mabadiliko ya mwili kufuatana na umri kuwa mkubwa kati ya mwanamme na mwanamke.
10   Kulinda Haki za kila raia bila kujali itikadi za dini, rangi, kabila jinsia na taifa.
      11  Kutoa Elimu ya uraia.
11    Kushirikiana
 na serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa katika maadhimisho 
ya  siku ya mwanamme Duniani ikiwemo kuandaa sherehe  hizo kitaifa 
kufuatana na kalenda ya kimataifa kila mwaka.
12   Kutoa
 misaada kwa makundi ya wasiojiweza  yatima, wazee,wagonjwa ,wakimbizi 
majeruhi wa ajari, majanga kama njaa,mafuriko, shule au kujenga majengo 
ya kutoa huduma za afya na elimu kulinda na kutunza mazingira kuangalia 
chaguzi ndani na nje ya Tanzania.
 
 
No comments:
Post a Comment