Mwl.
Salome Makanza wa Shule ya msingi Oysterbay akisoma risala kwa niaba ya
Mwl. Mkuu Msaidizi Janeth Mdingi ambapo ameishukuru Hoteli ya
DoubleTree by Hilton kwa kubuni kampeni kama hiyo ya kugawa taa
zinazotumia Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Darasa la Saba ambao
wanakabiliwa na Mitihani kwani zitawasaidia hata Umeme utakapokatika
majumbani mwao.
Mwl.
Salome Makanza akikabidhi risala yake kwa Mgeni rasmi Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mh.Dkt.
Terezya Huvisa. Kulia ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by
Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann. Kuhsoto ni Kushoto ni Afisa
Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl.Mkuu
Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili
kushoto).
Meza Kuu katika Halfa ya Uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua
zilizotolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Jijini Dar es Salaam
kwa shule za msingi za Mikoa ya Dar es Salaam ambapo leo wamezindua
kampeni hiyo kwa kuanzia shule ya Msingi Oysterbay jijini.
Mkurugenzi
wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd
Lehmann akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya kugawa taa zinazotumia
Nishati ya Jua kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi za Mkoa wa Dar es
Salaam ambapo amesema lengo lao ni kutaka wanafunzi hao wawe na ufahamu
kuhusiana na Nishati mbadala ya Umeme ambayo ni rafiki wa Mazingira.
Hivyo taa hizo zitawasaidia hata kunapokuwa hakuna Umeme wa Tanesco kujisomea majumbani bila kipangamizi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Mh. Dkt. Terezya Huvisa akitoa hotuba kuzindua kampeni ya ugawaji taa
zinazotumia Nishati ya Jua iliyobuniwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton
jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli
hiyo kwa kubuni mradi kama huo kwani taa hizo kwa kuwa zinatumia Nishati
ya jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata
Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa.
Baadhi ya Wanfunzi wa Darasa la Saba wa Shule ya Msingi Oysterbay wakimsikiliza mgeni rasmi.
Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa hoteli ya DoubleTree by Hilton ya jijini Dar wakati wa uzinduzi huo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Mh. Dk. Terezya Huvisa akiendesha maswali ya masuala ya mazingira kupima
upeo wa uelewa kwa Wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es
Salaa wakati akizindua kampeni ya kugawa taa zenye kutumia Nishati ya
jua kwa shule za msingi za mkoa wa Dar iliyodhaminiwa na Hotel ya
Doubletree by Hilton ya jijini Dar.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais
Mh.Dkt. Terezya Huvisa akimtunza Mwanafunzi Neema Njau shilingi Elfu
taslim baada ya kujibu vyema maswali yanahusiana na Mazingira wakati wa
hafla ya uzinduzi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizogaiwa kwa
wanafunzi wa Darasa la saba wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikata utepe kuashiria uzinduzi
rasmi wa taa zinazotumia Nishati ya Jua zilizotolewa na Hotel ya
Doubletree by Hitlon kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi wa shule tofauti
za msingi mkoa wa Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo Mkurugenzi wa
Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd
Lehmann aliyeambatana na Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof
(mwenye tai ya Orange) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoulbeTree by
Hilton Florenso Kirambata (nyuma ya Waziri). Kushoto (mwenye kipaza
sauti ) ni Afisa Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na
Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa
tatu kushoto).
Mgeni
rasmi Mh. Dkt. Terezya Huvisa akihamasisha wanafunzi kutumia vizuri taa
hizo hasa nyakati za kujisomea ya kukabidhi rasmi. Mkurugenzi wa kanda
wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (wa
tatu kulia), Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof (wa pili
kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoulbeTree by Hilton Florenso
Kirambata (kulia) na Wa kwanza Kushoto ni Afisa Elimu Msaidizi wa
Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl Mkuu Msaidizi wa Shule ya
Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili kushoto).
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akikabidhi rasmi taa inayotumia
Nishati ya jua kwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo John Maganga.
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree
by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (kulia) na Kushoto ni Afisa
Elimu Msaidizi wa Wilaya ya Kinondoni Faustin Kikove na Mwl Mkuu
Msaidizi wa Shule ya Msingi Oysterbay Bi. Janeth Mdingi (wa pili
kushoto).
Mkurugenzi
wa kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd
Lehmann akikabidhi moja ya taa hizo kwa mwanafunzi wa darasa la saba
Rebecca Andrew.
Mkurugenzi
wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akifanya
vivyo hivyo kwa mmoja wa wanafunzi wa shule msingi Oysterbay.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiwa kwenye picha ya pamoja na
Uongozi wa Hoteli ya DoubleTree By Hilton, Uongozi pamoja na baadhi ya
wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay baada ya kukabidhi taa hizo.
MC wa shughuli hiyo Taji Liundi akifurahi jambo na Meza kuu.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiteta jambo na Mkurugenzi wa
kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann
wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mwl. Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo
Janeth Mdingi.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Oysterbay ya Jijini Dar es Salaam wakipozi na taa
zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by
Hilton. Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo
zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani
hivyo kuongeza uwezo wao kielimu.
Na.Mwandishi wetu
Hoteli
ya DoubleTree by Hilton jijini Dar es Salaam imezindua rasmi kampeni ya
matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili
katika shule za mkoa wa Dar es Salaam.
Katika
kampeni hiyo Hoteli ya DoubleTree by Hilton itakuwa ikigawa taa 200 za
mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa
shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi
juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa
kupitia mafunzo katika madarasa yao.
Akizindua
rasmi kampeni hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira)
Mh. Dkt. Terezya Huvisa ameupongeza uongozi wa hoteli hiyo kwa kubuni
kampeni ambayo itawasaidia wanafunzi kutambua umuhimu wa nishati ya jua
na kufaidika na taa wao na familia zao.
Mh.
Huvisa amegawa awamu ya kwanza ya taa 200 za mezani zinazotumia nishati
ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya msingi Oysterbay
na kuwataka wazitunze na kuzitumia kujisomea.
Naye
Mkuu wa hiyo amtoa shukrani kwa Hoteli ya DoubleTree by Hilton akisema
kampeni hiyo inazo faida nyingi kwa upande wa afya, elimu, uchumi wa
nyumbani na mazingira kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment