LICHOKISEMA DJ CHOKA KWA WALIOFELI KIDATO CHA 4
Baada ya matokeo ya kidatocha nne kutoka vibaya, watu wameongea mengi sana, na mmoja wa watu walioongelea matokeo hayo ni DJ maarufu tanzania DJ CHOKA. Na alichokieongelea mi nimeona ni cha muhimu sana, na ndo maana nimeamua kushare nanyi. DJ HOKA kasema " Naulizwa maswali mengi wanataka kujua nilivyokuwa form 4 nilipata division ngapi? sasa jibu ni hili nilivyomaliza darasa la 7 mwaka 1998 pale MUGABE Primary Sinza nilifeli tena nilifeli haswa. Nilipofika form 4 mwaka 2003 nilipata division 4 ambayo ningefeli somo la computer ningepata 0 so somo la computer ndio lilininyanyua. Kwahiyo wadogo zangu wa form 4 kufeli masomo sio kufeli maisha, kama unaweza rudia yale masomo uliyofeli au kama vipi nenda kasomee vitu unavyovipenda kuliko kukaa na kukata tamaa ukizani maisha ndio yamekupiga picha". |
No comments:
Post a Comment