Mulugo aliliambia NIPASHE kuwa wizara
inasubiri Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imalize kufanya
kazi yake, ndipo itatoa uamuzi nini kifanyike juu ya wanafunzi hao.
“Kwa
sasa siwezi nikasema chochote kwani tume imeundwa ili kulifanyia kazi
jambo hilo, hivyo tunasubiri wamalize kufanya kazi yao ndipo tutatoa
kauli ya nini kifanye juu ya wanafunzi walio feli kama ni kurudia tena
mtihani au la,” alisema Mulugo.
Alitoa ufafanuzi
huo baada ya kuulizwa wizara yake inazungumziaje juu ya mpango wa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca
Msambatavangu kuandaa mafunzo ya kozi ya muda mfupi kwa vijana wote
waliofeli mkoani humo ili kuwapima kama wapo wanaaoweza kusaidiwa
kuendelea na elimu ya cheti.
Msambatavangu alitoa
uamuzi huo baada ya makubaliano yake na baadhi ya vyuo vikuu kama Chuo
Kikuu cha Tumaini (IUCO) na Chuo kikuu cha Ruaha (Ruco) na kukubaliana
kutoa mafunzo hayo yatakayo anza Machi mwaka huu.
Mulogo
alisema kuwa ni wazo lenye mpango mzuri wa kuwasaidia vijana wengi
ambao ni kama wamekumbwa na tatizo kwa sasa, hivyo anacho kifanya
Mwenyekiti huyo hakina madhara yoyote na anafanya kama raia mwema
aliyeguswa na matokeo hayo
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment