MWANAFUNZI ALIYEMALIZA KIDATO CHA NNE AKAMATWA AKIIBA FEDHA KATIKA ATM YA NMB
POLISI
wilayani Rungwe, mkoani Mbeya, limewanasa watu wanne akiwamo mwanafunzi
aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, wilayani Bunda, mkoani Mara,
baada ya kukutwa wakiiba fedha Benki ya NMB tawi la Tukuyu kupitia
mashine za kutolea fedha (ATM).
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku.
Meela aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mkazi wa mjini Tukuyu, Mfanyabishara wa Mbozi, mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana wilayani Bunda na mkazi wa Msasani Tukuyu.
Meela aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mkazi wa mjini Tukuyu, Mfanyabishara wa Mbozi, mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana wilayani Bunda na mkazi wa Msasani Tukuyu.
Alisema akiwa nyumbani kwake usiku, alipigiwa simu na msamaria
mwema na kuambiwa taarifa za kuwapo watu wakiwa kwenye mashine hizo za
kutolea fedha, huku wakiwa wanatoa fedha mfululizo na aliwatilia shaka.
“Jana usiku saa 2:30 nilipigiwa simu na msamaria mwema na
kuniambia kuwa, kuna watu wapo Benki ya NMB wanatoa fedha ATM tena
mfululilo huko wakiwa na kadi nyingi za ATM,” alisema Meela na
kuongeza:“Baada ya kuambiwa hivyo nilimpigia simu OCD (Mkuu wa polisi
wilaya), akatuma timu ya makachero eneo ta tukio na wakabahatika
kuwakuta na kuwatia nguvuni.”
Meela alisema watuhumiwa walikutwa wakiwa na kadi bandia za ATM
150 za watu tofautitofauti na kwamba, hadi wanatiwa mbaroni tayari
walikuwa na Sh20.5 milioni mkononi. Alisema kadi zote ni za NMB na
kwamba, zilikuwa zinaonyesha wateja wote ni walimu kutoka wilayani
Mbozi.
Alisema baada ya watuhumiwa kuhojiwa walidai ni wafanyabiashara
wanajihusisha na kukopesha fedha walimu, hivyo katika kuzirejea fedha
hizo walimu waliwapatia kadi zao ili waende kutoa benki.
“Kinachotupa hofu hapa ni kwamba, kadi zote hizi zinaonyesha
wateja kutoka wilayani Mbozi, sasa swali kwa nini waje kutolea fedha
hizo wilayani kwetu?” alihoji Meela.
Alisema watuhumiwa wote wapo Kituo cha Polisi Tukuyu kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alikiri kupata taarifa hizo, lakini alikataa kulitolea ufafanuzi kwa sababu wanaendelea na uchunguzi.
Chanzo: mwananchi.co.tz
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alikiri kupata taarifa hizo, lakini alikataa kulitolea ufafanuzi kwa sababu wanaendelea na uchunguzi.
Chanzo: mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment