MWANAMKE MMOJA WAUME WATANO, WOTE NDUGU, KILA MMOJA ZAMU YAKE KWENYE CHUMBA KIMOJA
MWANAMKE, Rajo Verma, 21, mkazi wa mjini
Dehradun, India, anaishi na wanaume wake watano katika kibanda chenye
chumba kimoja ambapo hulala na mwanamme mmoja kila usiku. Mwanamke huyo
hana uhakika na baba wa mtoto wake mdogo wa kiume ambapo anasema:
“Mwanzoni niliona matatizo kuwahudumia wote katika kuwapa unyumba.
Lakini sasa nawahudumia wote bila upendeleo.” Mumewe mmoja aitwaye
Guddu, 21, ambaye alikuwa wa kwanza kumwoa anasisitiza: “Wote tunafanya
naye tendo la ndoa bila wivu.
Sisi sote ni familia moja yenye
furaha. Jamaa huyo alimwoa Rajo miaka minne katika ndoa ya mila za
Kihindu na ndiye mumewe halisi. Lakini mila kijijini kwake zilimlazimu
kuwachukua kaka za mumewe pia kama waume zake. Hao ni Bajju, 32, Sant
Ram, 28, Gopal, 26, na Dinesh – ambaye alimwoa kwa njia hiyo ya kimila
mwaka jana alipofikisha umri wa miaka 18. Bajju ambaye ndiye mkubwa
kuliko wote anasema: “Namchukulia kama mke wangu na ninalala naye kama
wanavyofanya ndugu zangu.”
Rajo anafanya kazi zote za nyumbani na
kumtunza mtoto wake aitwaye Jay, mwenye umri wa miezi 18, ambapo waume
zake huenda kufanya kazi kila siku mjini Dehradun. Mwanamke huyo anasema
mama yake pia aliwahi kuolewa na ndugu watatu wa kiume, hivyo hilo si
jambo la ajabu kwake. “Ninalala nao kwa zamu. Hatuna vitanda chumbani
bali tunatumia mablanketi yaliyotandikwa sakafuni. Watu hao hunijali na
kunipenda zaidi, jambo ambalo wanawake wengi zaidi hawalipati katika
ndoa zao,” anasema.
Chanzo: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment