Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu
katika chumba namba 107 kwenye gesti iitwayo Jamboz iliyopo Kinondoni
jijini Dar.
Habari za uhakika zilieleza kuwa tukio hilo lilikuwa ni mtego baada
ya walezi wa denti huyo kunasa mawasiliano ya mfanyabiashara huyo
akimrubuni binti yao.
Katika mawasiliano hayo, Tajiri alimtaka denti huyo wa sekondari moja
iliyopo Kibamba, Dar (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum za weledi wa
uandishi wa habari), wakutane kwenye gesti hiyo kwa ajili ya
kuimomonyoa amri ya sita.
Baada ya walezi hao
kuufuma ujumbe kwenye simu ya binti yao, walimuwekea doria bila mwenyewe
kujijua na ulipokaribia muda waliokubaliana kukutana gesti, denti huyo
aliaga anakwenda ‘tuisheni’.
Huku mwandishi wetu wakiwa ‘stendibai’,
kitendo cha binti huyo kuaga muda huo kilianza kuonesha dalili za mtego
wa walezi kukaribia kukamilika.
Waandishi wetu ndiyo
waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kujibanza wakiwa na picha za
wawili hao ambapo walimshuhudia mfanyabiashara huyo akifika kaunta na
kuagiza maji makubwa na kuyanywa hadi yakaisha kisha kuelekea kwenye
dirisha la mapokezi ya gesti hiyo.
Ilidaiwa kuwa yale maji aliyokunywa chupa nzima alilenga kuwa fiti kwa ajili ya ‘gemu’ na ‘kadenti hako’.
Mmoja wa waandishi wetu naye alijisogeza kwenye dirisha hilo akijifanya kutaka chumba na kumsikia mhudumu akimpa Tajiri chumba namba 107 na kumuonesha kilipo.
Ghafla binti huyo naye alifika mapokezi akiwa na
sare za shule ambapo alimkuta paparazi wetu akiendelea kuzuga kwa kutaka
kukagua chumba kizuri kabla ya kulipia.
Dakika chache baada ya
Tajiri na denti huyo kuingia chumbani, mwanausalama mmoja alitangulia
akifuatwa na mwandishi wetu na ndugu wa denti huyo ambapo waliomba
kukagua chumba hicho kwa kuwa kulikuwa na binti yao.
Waliporuhusiwa
waliingia na kugonga chumba ambapo jamaa huyo alifungua, wote wakakutwa
wakiwa watupu huku mfanyabiashara huyo akiwa kwenye harakati za kuvaa
‘kinga’ au ‘dawa ya penzi’ baada ya kumchezea mtoto wa watu.
Tukio
hilo lilivuta hisia za jazba kwa umati uliofurika ghafla kwenye eneo
hilo huku kila mtu akilaani kitendo cha jamaa huyo kumkatishia denti
huyo masomo na kumpeleka gesti kwa ajili ya ngono.
“Fikiria wewe kama mzazi unalipa ada
mtoto wako asome halafu mtu mwingine kwa makusudi anamwachisha masomo
na kumpeleka gesti wakafanye ngono! Kweli inauma sana, kila mzazi
anatokwa na machozi,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo baada ya
kuibuka kwa varangati gesti hapo.
Kwa upande wake, dada mlezi wa anayemsomesha denti huyo (jina tunalo) alijikuta akimnasa makofi mfanyabishara huyo na kuzua timbwili zito kutokana na kupandwa na hasira ya ajabu.
Katika vuta nikuvute, ghafla jamaa
huyo alifanikiwa kuwachoropoka na kuingia mitaani akitimua mbio hivyo
kutoa kazi nyingine ya kuanza kumsaka upya ili afikishwe kwenye mkono wa
sheria.
GLOBAL.NET
GLOBAL.NET
No comments:
Post a Comment