Msanii mkongwe na maarufu
nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo
cha kutimuliwa jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen
inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview.
Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya
mahojiano mafupi ya mwanzo mtangazaji alisema watarejea baada ya
mapumziko mafupi na ndipo Nature hakuonekana tena.
Kilichotokea kwa mujibu wa
Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi
hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu
ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa
kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo kupitia ukurasa wake wa
facebook....
"hivi
kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano
na kuvaa kaoshi ni tatizo....
kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na
hivi kama kweri we nimuandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria
kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia
ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview"
No comments:
Post a Comment