Wilaya
inapakana na Wilaya ya Bukoba upande wa Kaskazini, Magharibi inapakana
na Wilaya ya Karagwe, Kusini inapaka na Wilaya ya Biharamulo, Kusini
Mashariki inapakana na Wilaya ya Chato na Mashariki inapakana na Mkoa wa
Mwanza.
Wilaya ina eneo la kilomita za mraba
10,739 na kati ya hizo kilomita za mraba 3,444 ni nchi kavu na kilomita
za mraba 7,295 ni eneo la maji hususani Ziwa Victoria . Eneo la nchi
kavu linahusisha pia zaidi ya visiwa ishirini vilivyomo katika Ziwa
Victoria .
JIOGRAFIA YA WILAYA
Wilaya ya Muleba imetawaliwa na vilima,
mabonde na tambarale (plateaus). Wilaya ipo kati ya mwinuko wa mita
1,150 na 1,667 kutoka usawa wa bahari na sehemu ya juu kabisa ni
Karambi. Mto Ngono unakatisha wilaya kuanzia Kusini kuelekea Kaskazini
ambapo unaungana na Mto Kagera unaomwaga maji yake katika Ziwa Victoria.
Wilaya imegawanyika katika kanda kuu
nne za kilimo ambazo ni: Ukanda wa mwambao wa Ziwa na Visiwa katika Ziwa
Victoria, Ukanda wa juu, Ukanda wa chini Kusini na Ukanda wa Burigi.
Ukanda wa mwambao wa Ziwa na ukanda wa juu unapata kipindi kirefu cha
unyevunyevu (miezi 8 – 9) wakati ukanda wa chini na wa Burigi unapata
kipindi cha unyevunyevu cha miezi 3 – 4 tu kwa mwaka.
Mvua zinanyesha zaidi upande wa
Kaskazini – Mashariki yaani milimita 1800 wakati Kusini – Magharibi ni
pakame. Kwa kufuata viwango vya miinuko na mvua, Wilaya inakuwa na kanda
za kilimo tofauti zenye mazao mbali mbali yanayopandwa katika misimu
tofauti.
Hali ya rutuba ya udongo si ya
kuridhisha hasa kutokana na mvua nyingi zinazosababisha kuondolewa kwa
virutubisho udongoni. Hata hivyo maeneo ya mabonde ya upande wa Kusini –
Magharibi na miinuko tambarale (plateaus) yana rutuba ya kutosha wakati
maeneo ya mwambao wa ziwa hayana rutuba.
IDADI YA WATU
Kulingana na takwimu za sensa ya watu
na makazi za mwaka 2002 na ongezeko la watu la asilimia 2.5 kwa mwaka
wilaya kufikia mwaka huu wa 2008 inakadiriwa kuwa na jumla ya watu
wapatao 453,931 na kati ya hao watu 225,891 ni wanaume na watu 228,039
ni wanawake.
Msongamano wa watu kwa kilomita ya
mraba ni 110. Watu wenye uwezo wa kufanya kazi ni asilimia 24 ya watu
wote wakati watu wenye umri wa kwenda shule ni asilimia 30, zipo kaya
81,084 na wastani wa watu katika kaya ni 4.7.
Jedwali Na.1, 2 na 3 hapa chini vinachambua kwa kina takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002 kama ifuatavyo:-
Jedwali Na. 1 : Idadi ya watu kwa umri na jinsi
Umri
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
0 -1
|
29718
|
32219
|
61937
|
1 – 5
|
29860
|
30760
|
60620
|
6 – 14
|
31518
|
28519
|
60037
|
15 – 24
|
34951
|
33697
|
68648
|
25 – 44
|
29331
|
25584
|
54915
|
45 – 60
|
19971
|
22957
|
42928
|
60+
|
16903
|
20340
|
37243
|
Jedwali Na. 3: Mlinganisho wa jinsi katika Grafu
Jedwali Na. 3: Idadi ya watu Kitarafa.
Tarafa
|
Idadi ya Kata |
Idadi
ya vijiji
|
Idadi ya Mitaa
|
Me
|
Ke
|
Jumla
|
Muleba |
6
|
22
|
2
|
27354
|
27760
|
55114
|
Izigo |
6
|
25
|
|
9123
|
8893
|
18016
|
Kamachumu |
4
|
15
|
|
29988
|
30759
|
68648
|
Nshamba |
9
|
39
|
|
72769
|
73398
|
146167
|
Kimwani |
6
|
31
|
|
53018
|
53266
|
106284
|
Total |
31
|
132
|
2
|
192252
|
194076
|
386328
|
UTAWALA NA UONGOZI KISIASA
KIUTAWALA
Kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali Na.
hapo juu wilaya ya Muleba imegawanyika katika Tarafa tano (5) nazo ni
Izigo, Kamachumu, Muleba, Nshamba na Kimwani. Tarafa hizo tano nazo
zimegawanyika katika kata 31, vijiji 132, mitaa 2 na vitongoji 677.
KISIASA
Wilaya pia imegawanyika katika majimbo
mawili ya uchaguzi. Jimbo la Muleba Kusini linaongozwa na Mh. Anna
Tibaijuka (Mb) na Jimbo la Muleba Kaskazini linaongozwa na Mh. Mwijage
(MB), na wote wawili wanatoka Chama Tawala cha CCM.
Upande wa Kata, Kata zote 30 zinao
madiwani wa kuchaguliwa ambapo kata moja iko wazi baada ya diwani wake
kufariki dunia na Kata 2 madiwani wake ni wa kutoka kambi ya upinzani.
Madiwani hawa wote ni wanaume. Wapo pia madiwani 11 wanawake wa viti
maalum ambapo 8 ni wa kutoka chama cha CCM na 3 wanatoka kwenye vyama
vya TLP 1 na CUF 2.
|
No comments:
Post a Comment