Sunday, April 14, 2013

Makahaba’ 51, ‘majambazi, na ‘matapeli’ kizimbani Dar


JESHI la Polisi linawashikilia watu wanne wa mtandao wa utapeli wa biashara ya madini bandia, huku mmoja wao akikutwa na kitambulisho bandia cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi nchini (JWTZ) chenye cheo cha Kapteni kikionesha kuwa aliwahi kushiriki vita ya Kagera na kupata medali ya vita. Polisi pia wanawashikilia watu wengine wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambao walikamatwa wakiwa na mirungi katika baa ya Muleba iliyoko Mabibo jijini Dar es Salaam wakiwa na bastola yenye uwezo wa kubeba risasi 12 pamoja na simu za mkononi. Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Charles Kenyela alisema jana kuwa mbali na watu hao, Jeshi la Polisi linawashikilia pia wanawake wanaofanya biashara ya …read more
Source: HabariLeo

No comments: