Tuesday, April 2, 2013

MATUKIO YA TAMASHA LA PASAKA

 

Pamoja na Mvua Kubwa iliyonyesha jana katika jiji la Dar-es-Salaam Maelfu Ya Wakazi wa Jiji la Dar wamejitokeza katika Tamasha la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa.

Tamasha Pasaka ni Tamasha linalofanyika Kila Mwaka mara moja katika Msimu wa Pasaka ambapo wanamuziki wa nje na ndani ya Tanzania wanakuwa na muda wa pamoja wa Kusifu na Kumwabudu Mungu.
 
Mwaka 2013 Kauli Mbiu ya Tamasha ni Amani na Utulivu ambapo fedha zitakazopatikana ni maalum kwa ajili ya kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Katika siku ya leo Mgeni rasmi alikuwa ni Mhe. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye mara kadhaa alipata shuruba ya kupigiwa makelele mara kwa mara kutokana na kukatika katika kwa umeme mara kwa mara.
 
Mwanamuzi Mwalikwa wa Mwaka huu Kutoka Africa ya Kusini ni Sipho Makabane ambaye jioni ya leo amefanya Performance ya nyimbo 10 Mfululizo ndani ya uwanja huo na Kukonga nyoyo za watu waliohudhuria Tamasha la leo. Malkia wa Muziki wa Injili Tanzania Rose Muhando alifanya kile ambacho kilitarajiwa na Wakazi wa Jiji kwa Kuimba wimbo wa Utamu wa Yesu ulioombwa na Mhe. Mgeni rasmi.
 
Wanamuziki Wengine waliokuwepo siku ya jana ni Christ Ambassadors kutoka Rwanda, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, John Lisu, Faraja Mtabobwa na Glorious Worship Team.

Waimbaji Wa Christ Ambassadors kutoka Rwanda walishuka Kutoka Jukwaani na kugusa wanakazi wa jiji la dar na wimbo wao "Kwetu Pazuri" 



Mwanamuziki Wa Injili wa Tanzania Upendo Kilahiro akienda sawa Siku Ya Leo



Upendo Nkone akiwa Jukwaaani


Anastazia Mukabwa kutoka Kenya akiwa na Rose Muhando ambao kwa pamoja wameimba wimbo wa "Kiatu Kivue"

 Christ Ambassadors Choir wakiwa tayari kwa ajili ya Kazi. 


Solomoni Mukubwa akiwa anapadna Stejini tayari kwa ajili ya Kuimba siku ya leo



Ephrahim Sekeleti Mwuimbaji Kutoka Zambia akiwa George Mpella na Hudson Kamoga


Glorious Worship Team wakienda Sawa siku Ya Leo


Malkia wa Muziki wa Injili Rose Muhando akiwa Kikazi Zaidi




Ephrahim Sekeleti akienda Sawa Siku Ya leo


Sipho Makabane akiwa kikazi Zaidi siku Ya leo


Sehemu Ya Umati Wa Watu


Rose akiendelea na Kazi huku Waandishi na Walinzi wakiwa wamemzunguka


Sipho akijiandaa kuingia Jukwaani


Pole Pole akisogelea Umati Wa watu


Koti Likawa Zito


Kikazi Zaidi


Hapa wakitengeneza Tangazo la Chomoza


Bon Mwaitege akiwa mbele ya Camera Man Ray wa Clouds Tv.


Sipho akienda Sawa na Wananchi siku ya leo


Watu Nyomiiiii


Wakati Sipho akiimba ni kama ilikuwa Mchaka Mchaka Kulia ni Anastazia, Rose Muhando Upendo Nkone na Solomon Yakima Support Sipho.


John  Lisu


Credit to Sam sasali.

No comments: