Mwanaharakati mashuhuri wa
kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja, amekamatwa nchini Zambia kwa
kuonekana kwenye televisheni akitaka uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja
kutofanywa kuwa hatia.
Paul Kasonkomona alishatakiwa kwa kosa la
''kuwachochea watu kushiriki vitendo visivyokubalika,'' alisema mkuu wa
polisi Solomon Jere.
Paul alikamatwa alipokuwa anaondoka nje ya studio hizo za kampuni ya kibinafsi ya Muvi.
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, ni haramu nchini Zambia.
Wadadisi wanasema kuwa watu wengi, wanaamini kuwa ni kinyume na imani zao
Duru katika stesheni hiyo, mjini Lusaka zilisema
kuwa polisi walijaribu kukatiza mahojiano lakini wakuu wa stesheni hiyo
walikataa.
Katika ombi lililotolewa kwa rais wa Zambia
Michael Sata, kundi moja la wanaharakati nchini Afrika Kusini Ndifuna
Ukwazi, lilitaka kuachiliwa mara moja kwa bwana Kasonkomona.
Kundi hilo pia lilisema linataka serikali ya
Zambia kuanzisha mara moja mpango wa kutofanya vitendo hivyo kuwa
kinyume na sheria ikiwa itakuwa kati ya watu wazima licha ya jinsia yao.
Vitendo kama ulawiti na uhusiano wa mapenzi kati ya wanawake, vina adhabu ya miaka 15 au kufungwa maisha jela.
Wiki jana kikundi cha wapenzi wa jinsia moja
kilijaribu kujisajili kama wanandoa lakini wakakatazwa na serikali
ikaamuru kukamatwa kwa yeyote atakayepatikana akihusika na vitendo vya
mapenzi ya jinsia moja.
Muungano wa ulaya mwezi jana ulitoa msaada wa
kifedha kwa mashirika yaliyotaka kuhamasisha kuhusu haki za wapenzi wa
jinsia moja nchini Zambia.
Mnamo mwaka 2011, Marekani na Uingereza zilionya
kuwa zitatumia msaada wa kigeni kama kikwazo cha kutoa ufadhili kwa
nchi za kiafrika ili kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Afrika Kusini ni mojawapo ya nchi chache barani Afrika zilizohalalisha mapenzi ya jinia moja.
bbc
No comments:
Post a Comment