KIJANA ambaye amekuwa ‘akiwaliza’ watu wakiwemo viongozi serikalini kwa kutumia jina la Waziri William Lukuvi aliyejulikana kwa jina moja la Jonathan amenaswa na polisi.
Kijana huyo alipita mbele na MC wa shughuli hiyo alimpa kipaza sauti ambapo alianza kwa kujitambulisha jina na kuongeza yeye ni mtoto wa Lukuvi.
Alisema mara kwa mara amekuwa akimpigia simu Lowassa ili azungumze naye akitaka msaada ambao hakuutaja ukumbini hapo.
Huku Mheshimiwa Lowassa akiwa amesimama wima na kumsikiliza kwa umakini, Jonathan alimwambia siku za nyuma katika mkutano wa mheshimiwa huyo uliofanyika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam alizungumza naye kuhusu shida yake kwa hiyo siku hiyo alitaka atekelezewe.
Kufuatia utambulisho huo, baadhi ya watu waliowahi kutapeliwa na kijana huyo, akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Teresia Mahongo waliguna, hali iliyosababisha polisi kujitokeza na kumtia mbaroni kijana huyo ambaye ilionekana alikuwa akiweka mtego wa kumtapeli Lowassa na viongozi wengine katika hafla hiyo.
Kada wa CCM mkoani Iringa, Godfrey Malenga Lukuvi alisema kijana huyo amekuwa akitumia jina la waziri kuliza watu. Alisema wengi wameshalalamika kuhusu utapeli unaofanywa na Jonathan na kuna wakati alikamatwa na polisi lakini akaachiwa.
Kwa upande wake, Katibu wa Mbunge Jimbo la Isimani ambaye pia ni familia ya mheshimiwa Lukuvi, Thom Malenga Lukuvi alisema amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali ambao wamelizwa na Jonathan na ameshaweka mitego ya kumnasa lakini hakuwahi kufanikiwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Mahongo alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa Jonathan aliwahi kufika ofisini kwake kwa lengo la kumtapeli lakini alimshtukia na kumpigia simu Waziri Lukuvi ambapo alisema kijana huyo ni tapeli.
Mwandishi wetu alimtafuta Lukuvi kwa simu na alipopatikana alimkana kijana huyo kwamba hamtambui wala hana undugu na ukoo wake.
“Huyu kijana simtambui na wala si ndugu yangu, ila amekuwa akitumia jina langu kutapeli watu na tayari amekamatwa na polisi kwa utapeli huo,” alisema Lukuvi.
No comments:
Post a Comment