VURUGU kubwa Nchini kenya ambayo zinaaminika kufanywa na vijana ambao ni wafuasi wa chama cha ODM nchini kenya pale walipoamua kuchoma makazi na kuharibu makao ya Raia Nchini humo.....
Katika Vurugu hizo watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na makazi yao kuchomwa moto kwa kile kinachosadikika kuwa ni Kutokubaliana na uamuzi wa mahakama nchini humo kuubariki Ushindi wa Rais mteule UHURU KENYATTA kama mshindi halali wa kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu uliofanyika mapema mwezi uliopita.
Askari wa kutuliza Ghasia walilazimika kutumia mabomu ya kutoa Machozi na silaha nyinginezo kuwatawanya vijana hao ambao awali walionekana kutishia hali ya amani Nchini humo...
Hata hivyo maeneo ambayo yaliathirika na Vurugu hizo ni pamoja na KISUMU na maeneo ya Kenya ya kusini.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/03/vurugu-vijana-wachoma-moto-makazi-ya.html#ixzz2PGk8sul4
No comments:
Post a Comment