MREMBO Brandina Barthon (24), Jumatatu iliyopita alihukumiwa kwenda
jela miezi 6 baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi ya ukahaba
iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar.
Brandina alisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
William Mutaki ambaye alisema kutokana na ushahidi uliothibitika,
mahakama hiyo inamhukumu kwenda jela miezi 6, ili liwe fundisho kwa
wengine.
Hukumu hiyo ilimfanya mrembo huyo kuchanganyikiwa na kuangua kilio
lakini mheshimiwa hakimu aliamua kukazia hukumu yake bila ya kupepesa
macho.
Wakati mwanamke huyo akiangua kilio, afande wa Jeshi la
Magereza alimfikia na kumchukua kwa ajili ya kumpeleka kwenye
Karandinga kuelekea Gereza la Segerea kuanza maisha ya jela.
Mbali na Brandina, mwanaume aliyedaiwa kuwa ni MUME wa mtuhumiwa
huyo aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo naye alimwaga machozi baada ya
kutolewa hukumu hiyo.
Credit:JIJI LETU
No comments:
Post a Comment