Tuesday, May 14, 2013

"MKITUKAZA KUNYWA VIROBA TUTAANZA KUNYWA GONGO"....WANANCHI WALIJIBU BUNGE



Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara, wakiangalia uzalishaji walipotembelea kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Dar es Salaam hivi karibuni.

Baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hoja iliyozuka bungeni wiki hii kwamba kinywaji cha Konyagi aina ya Kiroba kipigwe marufuku nchini.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao, walisema endapo serikali itachukua uamuzi wa kupiga marufuku kinywaji hicho, watarudia kunywa pombe aina ya gongo ambayo ni hatari kwa afya zao.


Mkazi wa Mbagala, Faustine Mwiruka aliyekutwa kwenye baa ya Kisuma, aliiasa Serikali kutothubutu kukubali kinywaji hicho kupigwa marufuku, kwani ikifanya hivyo wengi wa wananchi wenye kipato cha chini wataanza tena kunywa gongo na pombe za kienyeji.

Itabidi tufanye kama Zambia  ambao wamezuia viroba, lakini nchi nzima imejaa viroba vya Malawi, Zaire na Burundi, lazima tuiadhibu serikali ikose kodi kote kote, bia hatunywi, viroba vya nje tutakunywa, pamoja na gongo.

Alisema haingii akilini kukihusisha kinywaji hicho na ajali za magari, akidai kuwa hata kabla ya viroba kuingia sokoni ajali zilikuwepo nyingi.


“Sisi tuna imani na viroba kwa vile vina ubora wa uhakika tofauti na pombe ya gongo ambayo inapikwa bila kupimwa ubora hivyo ni hatari kwa usalama wa afya zetu.” amesema Mwiruka.


Naye Ali Hassan mkazi wa Kinondoni kwa Manyanya, alisema, wanaotaka viroba vipigwe marufuku hawawatendei haki wananchi wa kawaida ambao kwa asilimia kubwa hawana uwezo wa kununua bia ambazo bei yake ni kubwa.

Mwandishi wetu aliyetembelea maeneo ya Ilala Kota Mchikichini alifanikiwakuhojiana na wakazi wa eneo hilo ambao wengi wao walisema kuwa jambo hilo lililozushwa wiki iliyopita wanaamini ni njama za wafanya biashara toka nchi jirani ambao hawaitakii mema Tanzania  kwa kuwa pombe hiyo kuwepo kwake pia kunakuza pato la Taifa.

Juma Pingu amesema kuwa haoni sababu ya kupiga marufuku viroba kwakuwa ni pombe ya wanyonge na kuwataka wabunge kuthamini bidhaa za nyumbani kwanza.


Akizungumza na waandishi wa habari mwanzoni mwa wiki hii, Mkurungenzi Mkuu wa Konyagi, David Mgwassa amesema kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwa na mchezo mchafu wa kuharibiana jina sokoni kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini, kampeni inayoendeshwa na makampuni yenye uhusiano na makampuni makubwa ya pombe duniani yasiyo penda, nchi za afrika zizalishe pombe zake, bali ziendeleee kununua kutoka Ireland, wales. Kenya  and uingereza.


Wadau hao wa Pombe nchini walifikia uamuzi wa kutoa maoni hayo baada ya kuona kuwa kinywaji chao Kiroba kinapigwa vita lukuki kwenye magazeti. Huwezi ukahusisha viroba na piki piki, kwani nchi hii ina piki piki laki tatu, na wananchi million 43, uhusiano wake uko wapi, kwanza hata leseni hamuwapi?

No comments: