Thursday, May 9, 2013

APANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUBAKA NA KUMNAJISI MTOTO WA MIAKA 7....!!

MKAZI wa Sinza B, Dar es Salaam, Jesse Malewo, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka saba. Akisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Hilder Lyatuu, Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali, Amani Mghamba, alidai tukio hilo lilitokea Machi 3, mwaka huu, eneo la Sinza Madukani.

Alidai mshitakiwa baada ya kutenda kosa hilo aliamua kumuingilia msichana huyo kinyume na maumbile, kitendo kilichomsababishia maumivu makali.

“Ulifanya kosa hilo kwa makusudi wakati unajua ni kinyume cha sheria za nchi,” alidai Mghamba.

Mshitakiwa alikana kosa na upelelezi bado unaendelea, ambapo Hakimu Lyatuu aliamuru mtuhumiwa kuleta wadhamini wawili walioajiriwa wakiwa na barua za waajiri wao.

Hata hivyo, mtuhumiwa hakutimiza masharti ya dhamana hivyo alirudishwa mahabusu hadi Mei 22, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

No comments: