Hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani
Ulinzi umeimarishwa kila kona
Hali
ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete. Soko Kuu,
kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.
Usafiri wa
Pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo
makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo
kawaida.
Polisi wakiwa kwenye magari
wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na wengine kuweka makambi
madogo katika maeneo yanayoaminika kuwa na msongamano wa watu katika
siku za kawaida.
Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.
Mwandishi wetu ameshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya
Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na gari la kumwaga maji ya kuwasha,
Magomeni, Skoya na Majengo.
MADUKA YA BIMA YOTE CLOSED:
JUCTION YA BIMA HAINA WATU KABISA, HATA NMB IMEFUNGWA:
KWA MBALI UTALIONA GARI YA ASKARI IKIRANDARANDA...KOKOBICHI, KIMYA KABISA
Hata
hivyo hadi kufikia saa 7 mchana hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa
amani, makundi ya vijana walionekana wakijadiliana mambo katika maeneo
mengi ya mji.
Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi
na ujumbe wa simu za mkononi na watu wasiojulikana ukiwataka
wafanyabishara kusimamisha shughuli za biashara kwa siku ya leo
ili kutoa fursa kwa wananchi hao kusikiliza bajeti ya Nishati na Madini
iliyotarajiwa kuwasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma.
Hata hivyo bajeti
hiyo itawasilishwa Bungeni Mei, 22, mwaka huu.Sehemu ya kipeperushi hicho
kilichopambwa na picha ya mtoto aliyeshikia kombora kinasomeka
“Wote
kwa pamoja siku ya tarehe17.05.2013 (Ijumaa saa 3 asubuhi) tusikilize
bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (Bungeni) ili kujua mustakabali
mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio, msimamo wetu kwa serikali wa
kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini, siku hiyo huduma zote za jamii
zisimamishwe”
Licha ya polisi mkoani
hapa kuwasihi wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa
jeshi hilo litaimarisha ulinzi bado wananchi wameonesha kutokubaliana na
wito huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Mtwara, Linus Sinzumwa ameliambia amesema kuwa hali ni shwari na
kwamba jeshi lake limeimarisha ulinzi.
“Hali
ni shwari, wapo madereva Bodaboda wanaendelea na kazi zao, wananchi
wanatembea kama kawaida, ispokuwa baada ya maduka yamefungwa” alisema
Sinzumwa
No comments:
Post a Comment