Hali ya chuki dhidi ya CHADEMA inayoonyeshwa na mbunge wa Iramba Magharibi dhidi ya CHADEMA imesababisha wafuasi wa CHADEMA kote nchini kuungana kuhakikisha CHADEMA inamshinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu katika jimbo la Iramba 2015.
Mwigulu Nchemba anakabiliana na Msomi aliyebobea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Pia wafuasi wa CHADEMA wameapa kuhakikisha CHADEMA inazoa viti vyote vya udiwani Iramba Magharibi ili kumuonyesha ni nini maana ya nguvu ya umma.
Katika mahojiano na wafuasi kadhaa wa CHADEMA wa mikoa ya Mara,Kagera na Mwanza wameutaka uongozi wa CHADEMA kuanzisha Akaunti maalum ambayo itachangiwa na wanachama kuhakikisha Mwigulu harudi bungeni.
Wanachama hao wamesema chuki ya Mwigulu dhidi ya Chadema hailezeki na ameapa kutumia njia zozote kuiangamiza CHADEMA.Wamesema hata awapo bungeni hatetei chochote wanaIramba zaidi ya kutukana na kukashifu viongozi wa CHADEMA.
Hii itakuwa ni Operesheni Ondoa Mwigulu Iramba(OMI) walisema wafuasi hao wa Chadema.Pia walisema watajitolea kukaa Iramba kipindi chote cha Kampeni kuhakikisha Mgombea wa CHADEMA anapata ushindi wa 80%.
Kwa sasa Jimboni Iramba Dr Kitila Mkumbo anazungumzwa kila kona ya Jimbo hilo kama mwanasiasa makini,mpole na mtetezi wa dhati wa wananchi.Mzee mmoja katika kata ya Ndago Iramba aliwahi kusema mwaka jana kuwa kwa kawaida watu wa Iramba ni wanyenyekevu na wenye kupima maneno kabla ya kuzungumza mfano wa Dr Kitila.Mzee huyo alisema hawakuwahi kujua kama kuna siku wangekuwa na mbunge mwenye kuhamasisha chuki ndani ya jamii kiasi cha kuhatarisha amani ya nchi.
CREDIT:Apex Bnews
No comments:
Post a Comment