Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Akitoa Damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa mlipuko wa bomu Leo jijini Arusha.
Nassari Akitoa damu kwa Majeruhi Mlipuko wa BomuMbunge wa Arumeru Mashariki,
Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde
amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na
bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya
kuwawekea majeruhi.Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi
wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya
kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la
Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.Kutokana watu wengi kupoteza damu na
kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo
wameueleza mtandao wa Habarimasai.com kwamba hivi sasa wana wakati mgumu
katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia
manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na
dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.Lema na Nassari wameonekana
wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo. Endelea
kusoma habarimasai.com kwa taarifa mbalimbali zaidi.
No comments:
Post a Comment