Sunday, June 30, 2013

JACK WOLPER ADAI KUWA ANAPENDA KUTEMBEA NA "SERENGETI BOYS" KWA SABABU WANAYAJUA MAPENZI UKILINGANISHA NA WATU WAZIMA WENYE PESA ZAO



Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu...

Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati  kwani mapenzi yao ni ya  chumbani tu...


" Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake , alafu mtu mzima, ni  lazmia  ukose  penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi ...


"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..

“Wanaume wengi wenye  pesa zao huniona  nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
 
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.

Wolper  anadai kuwa  kuna watu ambao huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine....
 
Jack Wolper anasema wao si malaika , wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
source:mpekuzi

No comments: