Yameandikwa
mengi kuhusu hali ya ukosefu wa staha na heshima na matumizi ya maneno
ya kukera inayoendelea kwa baadhi ya wabunge katika vikao vinavyoendelea
bungeni ("Mjengoni") Dodoma. Mwanazuoni Machunde Mauma
amejaribu kupitia vyanzo mbalimbali vya habari na kukusanya hatimaye
kuorodhesha baadhi ya nukuu ya maneno ya kukera zinazotumiwa na baadhi
ya wabunge hao....
1. ‘‘Kuna
wabunge ambao wana mimba sizizotarajiwa bungeni...”
-Mbunge wa Mtera (CCM),Livingstone Lusinde
2. "Sugu
naomba unyamaze. Mimi ndiye nazungumza. Mimi siongei na mbwa,naongea
na
mwenye mbwa"
-Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM),Juma Nkamia
3.“UDOM (Chuo
Kikuu cha Dodoma) kuna udini wa hali ya juu, wanafunzi wa dini tofauti hawalali
chumba kimoja.”
-Mbunge wa Rombo (CHADEMA),Joseph Selasini
4."Kwa
kuwa wanaume wengi wanabaka, kifunguliwe kituo wafundishwe kutongoza.”
-Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Leticia Nyerere
5.“Serikali
iruhusu raia wa Tanzania walime bangi wapate fedha za kigeni.”
-Mbunge wa Nkasi (CCM), Ally Kesi
6.‘‘Mambo mengi
nchi hii hayaendi kutokana na serikali pumbavu, hatuwezi kuwa na waziri wa
elimu boya...”
-Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi
7. "Siwezi
kuikubali taarifa hiyo. Nadhani huyu mtu bado amechanganyikiwa na uchaguzi wa
kenya. Mimi sijaitaja Chadema bali nimesema kuna chama kimoja cha siasa, SIJUI
YEYE ANAWASHWA NINI..!!
-Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde
8.
"Serikali ina tatizo kwa kuwa kuna akili ndogo inatawala vichwa vikubwa.”
-Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA),Mchungaji Peter Msingwa
9. "Mbowe
kaja hapa anajambajamba tu" ..."Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au
mchungaji wa nguruwe?
-Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Saidi Haji
10.
"Wanaume wanapoongea,watoto wa kiume wakae chini"
-Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) Mwigulu Nchemba
Kama hali hii imefikia hapa kwa mhimili huu muhimu wa dola ni dhahiri kuwa tunakoelekea si kwema asilani!
No comments:
Post a Comment