Monday, June 3, 2013

TASWIRA MBALI MBALI KATIKA SHEREHE ZA UTAMADUNI WA WASUKUMA


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akibusu petu ya Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu la Mwanza,Yuda Thadei Ruwaichi wakati alipowasili kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila  la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako alizindua sherehe za utamaduni  wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo,  Juni 2, 2013.
 Baadhi ya watemi wa Kisukuma wakiingia kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako sherehe za  Utamaduni  wa wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo zilifanyika Juni 2, 2013.
  Baadhi ya washiriki wa sherehe za  umtamaduni wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia alipozindua sherehe hizo kwene uwanja wa Bujora Kisesa jijini , Mwanza  juni 2, 2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea fimbo ya Kitemi kutoka kwa  Antonia Mipamo maarufu kwa jina la Tonisiza ambaye pia ni Mtemi Chigoku Masa wa Simiu baada ya  kutawazwa muwa Mtemi wa Wasukuma wakati alipozindua sherehe za Utamaduni wa Wasukuma katika uwanja wa Bujora, Kisese jijini Mwanza Juni 2, 2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na baadhi ya watemi wa kabila la Wasukuma waliomkabidhi zawadi  mbalimbali  kabla ya kuzindua sherehe  za utamaduni wa kabila la Wasukumba kwenye uwanja wa Bujora, Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013. 
 Baadhi ya wapiga ngoma wakionyesha ufundi wao  katika sherehe za utamaduni wa Wasukuma zilizozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uwanja wa Bujora, Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu Mkuu wa jimbo Kuu la Mwanza, Yuda Thadei Riwaichi (kulia) wakifurahia ngoma ya wasukuma katika Sherehe za Utamaduni wa Wasukuma kwenye uwanja wa Kisesa jijini Mwanza Juni 2, 2013. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  ambaye hivi karibuni alitawazwa kuwa Mtemi Kishosha wa Dutwa, Bariadi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Mh. Lowassa aongoza harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Rukwa

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya kuchangia maendeleo ya Willaya mpya ya Nyasa iliopo Mkoani Ruvuma,katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre,Ilala jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi,Mh. John Komba akizungumza machache juu ya Wilaya hiyo mpya wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Willaya mpya ya Nyasa iliopo Mkoani Ruvuma,katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre,Ilala jijini Dar es Salaam.Mh. Komba ndio Mwenyeji wa harambee hiyo akishirikiana na Kamati ya Maendeleo ya Wilaya ya Nyasa.
Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk. Cyril Chami (katikati) akitoa ahadi yake ya kuchangia harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Prof. Mbele wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya mpya ya Nyasa.
Brigedia Jenerali Mstaafu,Julius Mbilinyi akitoa ahadi yake Mbele ya mgeni Rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi mchango wake kwa Mratibu wa harambee ya maendeleo ya Wilaya ya Nyasa iliyopo Mkoani Ruvuma ambapo yeye na marafiki zake walichangia kiasi cha Tsh.65 Millioni kwenye harambee iliyokusanya Zaidi ya Tsh. 300 milioni.
Madiwani wa Wilaya Mpya ya Nyasa wakizungumza na kutoa ahadi zao za michango.

No comments: