Saturday, July 13, 2013

AUNT EZEKIEL AANIKA KUHUSU UBEBAJI WA MIMBA

STAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel juzikati alifunguka na kuweka wazi juu ya mipangilio yake ya ndoa kuwa anatarajia kubeba ujauzito siku chache zijazo kwani ana kiu kubwa ya kuitwa mama.
Akichonga na paparazi wetu Julai 9, mwaka huu nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, Aunt alisema kuwa anajutia sana kukaa kwa muda wote bila kuiruhusu mimba iingie ila siku si nyingi mambo yatakuwa yametiki.
Nina mpango wa kubeba mimba na nizae siku chache zijazo kwani sina sababu tena ya kunifanya nisipate mtoto kwa wakati huu ambao niko ndani ya ndoa na naamini itaimarika zaidi nikiitwa mama huku pembeni akiwepo baba wa mtoto wangu,” alisema Aunt Ezekiel.

 Kishymba

No comments: