BAADA ya mumewe kipenzi, Jafar Ally
kufariki dunia hivi karibuni, Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa
amefunguka kuwa kwa sasa anaishi maisha magumu sana.
Marehemu Jafar Ally enzi za uhai wake.
Akizungumza nasi hivi karibuni,
mwanamama huyo alisema hali hiyo inatokana na kukosa msaada aliokuwa
akiupata kutoka kwa mumewe huyo ambaye alikuwa na nafasi kubwa katika
maisha yake.
“Hakika naishi maisha magumu sana
hivi sasa, sina hata nguvu ya kufanya chochote ila namshukuru Mungu kwa
yote, mume wangu alikuwa ndiyo msaada mkubwa kwangu, nikienda kwenye
shoo ananipeleka sasa nimebaki mpweke, siwezi kumsahau mume wangu
milele,” alisema Khadija.
Kwa upande mwingine, Khadija alisema
hana mpango wa kuolewa tena kwa sasa kutokana na jinsi alivyokuwa
akimpenda mumewe japokuwa hawezi kujua kwa siku zijazo kwani Mungu ndiye
mpangaji wa kila jambo.
No comments:
Post a Comment