1. Jana Julai 10, 2013 Mbumge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) alirudi Jimboni kwake tokea Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa
matibabu kufuatia kipigo alichopata wakati wa uchaguzi wa diwani Kata ya Makuyuni.
2. Ratiba ya kurejea kwake ilihusiha mapokezi ya ndugu, jamaa, marafiki
na watu wa Chadema kuanzia uwanja wa mdogo wandege Arusha na baadae
kufanya mkutano wa hadhara Jimboni kwake eneo la Liganga - Usa River.
3. Bahati mbaya raiba hiyo haikuweza kukamilika baada ya Jeshi la
Polisi luweka zuio la kutokuwako mkutano wana shamrashamra za mapokezi
kwa mtu yeyete kwasababu za kuwako kwa chaguzi za udiwani Arusha Mjini
keshokutwa Jumapili Julai 14, 2013.
4. Maandalizi ya zuio la
Jeshi la Polisi yalianza asubuhi kwa kuweka utepe kuzunguka eneo
walilotenga katika uwanja wa ndege Arusha na skari wenye silaha
wakilinda na pia kusambaza gari la majii ya kuwasha na askari wengi
kulinda viwanja vya wazi Usa River wakiwa na mabomu, bunduki, mbwa na
farasi.
5. Kwa kiasi kikubwa zuio hilo la Polisi lilipokelewa
vyema na maelfu ya watu wa Chadema waliokuwa wameshajpanga kwa wingi
kumpokea Mbunge Nassari na kuhudhuria mkutano wake wa Arumeru Mashariki.
6. Mh Nassari aliwasili uwanja wa ndege Arusha majira ya mchana na
kupokelewa na watu walionea gari mbili tu zilizoruhusiwa na Jeshi la
Polisi, saloon moja na Jeep ya wazi iliyombeba nassari.
7.
Msafara wa gari hizo mbili za Nassari ulisindikizwa kwa ulinzi mkali na
magari (Landcruiser) za Jeshi la Polisi kwa nyuma na mbele zikiwa
zimesheheni askari wenye silaha kali hadi ofisi kuu za Chadema zilizopo
Ngarenaro Arusha. Nassari akaingia ofisini askari wakapaki pembeni
kuendelea kulinda walichoagizwa kulinda.
8. Njiani kulikuwa na
wananchi baadhi wenye magari na bodaboda waliotaka kuunga msafara lakini
kabali ya Polisi iliwafanya wasiweze kuunga msafara huo.
9.
Katika ofisi za Chadema walikuwepo wanachama kiasi na viongozi wa Chama
ngazi ya Mkoa na Kanda, sambamba na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Lema na
waandishi wa habari, wote wakimsubiri Nassari wampokelee ofisini hapo
baada ya kuzuiwa uwanja wa ndege. Pia walikuwapo wagombea udiwani wa
Kata za Kaloleni na Elerai ambao walitangazwa na watu wa CCM kuwa
wamejitoa ili kuwahadaa.
Press Conference
10. Mh
Nassari aliongea na waandishi wa habari ofisini hapo na kueleza kwa
ufupi maumivu yake na kipigo alichopata na kudai kuwa aliumia zaidi uti
wa mgongo.
11. Nassari akasema kwa sasa yuko salama na mzima wa
faya na atashiriki kwa ukamilifu katika chaguzi za udiwani na ataongoza
kikosi maalumu kwa Kata mojawapo kulinda kura za Chadema isiibiwe hata
moja kama sheria zinavyoagiza ili haki itendeke.
12. Nassari
alishangazwa na kulaani uamuzi wa Jeshi la Polisi kumfuatiliatangia
uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kisha kumzuia kabisa asionane na
watu wake ilhali wanajua Arumeru kwake ni Mamlaka tofauti na Arusha
Mjini na yeye ni mbunge wa kuchaguliwa na watu hao na ametoka katika
matibabu.
13. Baadae Mbunge wa Arusha Mjini akapewa nafasi ya
kuzungumza na kuanika bayana mtego waliokuwa wameemtegea Mwigulu Nchemba
kwa kili kilichoelezwa mnamo Juni 12, 2013 alifanya mpango wa kumrubuni
mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Mpinga kujitoa kwa kumdanganya
kuwa yeye Mwigulu alikuwa ametumwa na Rais Kikwete na kwamba angekubali
angepewa Ukuu wa Wilaya au cheo chochote ambacho angetaka. Lema anasema
mtego huo ni kama Mwigulu aliushitukia na kwamba kama angeingia kwenye
18 angefanywa kitu mbaya.
14. Lema aksema Chadema kama chadema
wanarudisha Kata zote nne na wamejipanga kwa kila hila kuhakkisha hakuna
dhuluma itakayofanikiwa, ikiwemo zoezi alilodai linafanywa na maofisa
wa Tume ya Uchaguzi walioko Jijini Arusha kujaribu kubadilisha majina ya
daftari la wapiga kura.
15. Mh Lema alitanabaisha kuwa nae
ataongoza kiksoi maalumu kwa usalama wa kura za chadema kwa Kata
mojawapo na kwamba kuna baadhi ya wabunge wa Chadema watakuja Arusha
kuapishwa kama mawakala na watashiriki uchaguzi huo kuhakikisha hakuna
haki yao itakayodhulumiwa. Pia makamanda wao waliokuwa mikoani kama Ally
Banaga na Alphonce Mawazo na wengine watarudi kuungana na wengine
kuongeza nguvu ya ulinzi.Watakaofanya vurugu wapewe kichapo
16.
Lema akatahadharisha kuwa kuna watu wameandaliwa kufanya vurugu
wakivalishwa alama za Chadema ili ionekane ni Chadema. Lema akasema
yeyote atakaefanya vurugu sio mtu wa Chadema na atashushiwa kipigo bila
kujali amevaa magwanda ama kitu gani na kwamba watu wa Chadema
watatambua na alama wanazozijua siku hiyo. Amewataka watu wote wa
Chadema kuwa wapole lakini jasiri ili wasiwape mwanya CCM kutimiza hila
zao.
Eng Mpinga akanusha kuhamia CCM, amdharau Mwigulu Nchemba
17. Mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Jeremiah Mpinga akajitokeza
mbele ya kamera za waandishi wa habari na kukanusha propaganda za
Mwigulu Nchemba akimtumia kijana aliyefukuzwa Chadema, Mtela Mwampamba
kupitia mitandao ya kijamii (facebook na Jamii Forum) wakidai yeye
Mpinga amkubaliana nao kuhamia CCM.Eng Mpinga akasema amemdharau sana
Mwigulu Nchemba na akasema hakuwahi dhani ni mpuuzi kiasi hicho
kwasababu Mwigulu aliomba kuonana ane Mpinga mapema mwezi Juni, kwanza
kwa kupitia viongozi wa Wilaya Arusha na baadae mawasiliano
yalivyoendelea ndipo Mwigulu mwenyewe akajitokeza kwa namba yake 0714
008888 kuomba waonane akidai ana maagizo ya Kikwete.
Mzee
Mpinga akasema Mwigulu ni kama ndugu yake kwasababu wanatoka maeneo
jirani huko Singida na wanafahamiana. Alipomuomba kuonana nae
alimkubalia kama ndugu na alikataa kukutana maeneo mengine zaidi ya
nyumbani kwake.
Eng Mpinga akatanabaisha kuwa japo aliona ngumu
kwenda nyumbani kwake, alilazimika kufika siku ya Juni 12, 2013 akiwa
ameambatana na Mtela Mwampamba. Mzee Mpinga kwa kujihami kiusalama
alibaki sebuleni kwake na red brigade mmoja na alikuwa nae sebuleni.
Mwigulu alipofika akahoji huyo ni nani na kutaka aondolewe aliambiwa na
mtoto wa familia na hapo ni kwake ahawezi kuondoka.
Ndipo
Mwigulu Nchemba akaanza kubembeeza kwa hadaa kwamba ametumwa na Rais
Kikwete kumuomba Eng Mpinga ajitoe Chadema na atapatiwa cheo au kazi
yeyeote ikiwemo ukuu wa Wilaya.Mzee Mpinga akamchomolea Mwigulu katakata
na Mwigulu akaondoka na kusema "Kaa ujifikirie, ukipata jibu
nijulishe... Sisi (CCM) ndio tuna Serikali tunaweza kufanya chochote..)
Picha iliyowekwa Facebook na mtumishi wa Mwigulu ilipigwa kwa siri
kwasababu Eng Mpinga anasema hakukuwa na tukio la wazi la kupiga picha.
Katibu wa Kanda awashukia Polisi
18. Nae Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa
amelitaka Jeshi la Polisi kutumia kiherehere kile kile walichokitumia
kumkamata Mh Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kile alichoandika Facebook kuwa
waziri mkuu ni -------- kuagiza wananchi wapigwe tu, basi wa wamkamate
pia aliyesambaza picha na maelezo ya uongo huko Facebook na Jmii Forums
kuwa mgombea wa Chadema amejitoa ilhali wanajua kampeni zimepigwa
marufuku na Tume na taarifa yake sio ya kweli..
Safari ya Nassari kuelekea Arumeru
19. Baada ya kikao na waandishi wa habari Nassari na msafara wake wa
gari mbili walondoka ofisini hapo kuelekea Arumeru. Defenda za Polisi
zikawaunganishia tena kukaba msafara. Ilikuwa ni kama vile gaidi osama
analindwa asitoroke.
20. Msafara ulikatiza Kilombero, Desemba,
Seliani na hadi unafika mataa ya Mianzini tayari kundi kubwa la magari,
boda boda n.k waliunga msafara na Polisi wasijue la kufanya. Wananchi
waliokuwa pembezoni mwa barabara walishangilia sana kwa miluzi na
makelele kila mahali Nassari alikopita pamoja na kukabwa na askari
polisi.
21. Baadhi ya magari binafsi yaliyounga msafara
kilazima yalianza kujiachia mojamojakuanzia Philips yakabaki magari kama
manne hivi ambayo yalikuwa ni kutoka Arumeru. Polisi nao wakiwa nyuma,
msafara ukikimbia nao wanakimbia..
22. Gari ya Polisi kutoka
Arusha ilipokelewa na gari nyingine iliyokuwa imejiandaa kwa kazi hiyo,
ya Arusha ikaishia maeneo ya Tengeru.
23. Maeneo ya Makumira
kulikuwa na gari jingine landcruiser lenye askari walio tayari kwa
mapambano na mabomu yao wametega mahali pembeni ya njia.
24.
Nassari na watu wake wakafika Leganga Usa River na kushukia njia ya
vumbi kulia kufuata ilikokuwa gari ya matangazo ya Chadema maeneo ya
Ngaresero iliyokuwa ikiwatangazia watu kuwa mkutano wake umeahiriswa
hadi watakapotangaziwa tena.
25. Hapo Leganga askari Polisi
walikuwa wameziba kabisa njia inayoingia uwanja wa Shule ya Msingi
Leganga, baada ya kuona Nassari ameingia njia ya vumbi nao
wakaunganishia kwa nyuma kumfuata.. Baade kidogo landcruiser 2
zilizosheheni askari na silaha zao wakaunga msafara tena kumfukuzia
Nassari.
26. Askari wengine kwenye Landcruiser na silaha
waliziba njia ya kuingilia uwanja mwingine wa Ngarasero pale Usa River,
wananchi wakiwa wametanda barabarani washangaa..
27. Nassari
akiwa kwenye gari ya wazi alikutana na barrier ya Polisi baada ya kuvuka
daraja Fulani kama mita 150 hivi kabla ya kuingia Usa River halisi
kupitia Old Moshi road (sasa Mandela Road). Barrier hii iliongozwa na
Mkuu wa Kituo cha Polisi Usa River ..kama sijakosea ni Mussa Sindi Huya
28. Kufikia hapo hali ilianza kuwa mbaya, Polisi walikomaa Nassari
waondoke nae bila mtu mwingine yeyote. Nassari nae hataki. Mabishano
yakawa makali sana kiasi cha askari wote kushuka kwenye magari yao na
kuwazingia Chadema huku silaha zao zikiwa tayari tayari kwa lolote.
Punde kidogo gari 2nyingine 2 za Polisi zikaongezeka na kupaki mwanzo wa
daraja, Nassari na Chadema wake wakawa wamewekwa Kati huku mabishano
yanaendelea. Watu wa Chadema waliokuwa nje ya magari ni reed brigade
peke waliokuwa kwenye gari ya wazi..wengine walikuwa ndani ya magari yao
kama matatu wakisubiri hatma ya hali ile.
29. Wakati Mkuu wa
Kituo yuko bize kuwasiliana na Nassari nae alikuwa busy pia kuwasiliana
na wote wakimaliza kila mmoja anadai ameelekezwa hivi na ndicho kilicho
sahihi. Kiongozi huyo wa Polisi alionekana kama anapokea maagizo fulani
kila anapoambiwa taarifa mpya na Nassari kutoka mahali Fulani..
30. Nassari akawaambia kama ni vipi aende mwenyewe kwa mguu hadi
Ofisini kwake na hao wenzake warudi. Polisi wakakataa, wanataka waondoke
nae wao.
31. Baada ya mzozo kutokuwa na muafaka na dalili ya
hali kuchafuka zaidi, magari yote yaliamriwa kugeuza kurudi yalikotoka.
Madereva wakatii na kugeuza lakini kusogelea darajani wakakuta gari za
Polisi zimeziba, wao wako kati na dalili ya Polisi kukinukisha iko
wazi..
32. Nassari akapanda boda boda na kuondoka eneo hilo,
hatua hiyo ikawalazimu Polisi kuwasha landcruiser zao na kuanza
kumfukuzia na hapo kutoa mwanya kwa gari zilizokuwa ziimewekwa kati
kugeuza tena kwa kasi ya ajabu na kupenya huku nyingine zikikatiza
kwenye mahindi ya watu na kutimka lakini wakakutana na kizuizi kingine
cha Polisi inapotokea Mandela road kuunga na barabara kuu ya Moshi
Arusha.
33. Nassari alifika mahali huku anafukuzziwa na askari
Polisi akaacha ile bodaboda akaingia kwenye Suzuki iliyokuwa na Katibu
wake, Toti Ndonde akiwa na watu wengine wawili. Wale watu wengine
walishatawanyika kila mtu na njia yake.
34. Askari Polisi
waliendelea kuifukuzia Suzuki hiyo hadi ikafikia mahali Nassari akashuka
na kuwaluliza wanamfuatilia nini hivyo? Askari wale wakajibu yeye
aendelee na shuguli zake wao wanayao. Nassari akarudi garini safari
ikaendelea. Sasa alikuwa anaelekea shambani kwake anakojenga nyumba
yake. Polisi bado wanamfukuzia.
35. Nassari akafika restaurant fulani akaamua kushuka kwenye gari aende chooni kujisaidia, Polisi bado wamekaba.
36. Nassari akaenda hadi kwenye nyumba yake anayojenga, akakagua
mambomambo hapo.. Polisi bado wamekaba na landcruiser lao. Kha!
37. Baada ya kutoka maendeleo ya kazi ya ujenzi na kuona hali ya
kufuatwa inaendelea, ikabidi dereva akaimbize gari na kuwapotezea
vichochoroni.HII NDIO KAZI YA JESHI LA POLISI KWA SASA… WAKATI WAHALIFU
WANAKULA RAHA WAO WANAHANGAIKA NA WATU WEMA TENA VIONGOZI WAKUBWA
KABISA!!
source:CHADEMA IN BLOOD
No comments:
Post a Comment