* Atoweka nyumbani kwa siku mbili
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ihanga Kata ya Ilomba Emanuel Mwasibata akiwa amesimamia kikao cha usuruhishi
Dereva
wa daladala Aswile Mwalukoba aliyeshika fimbo baada ya kurejea nyumbani
na kuhudhuria kikao cha usuruishi ambapo alikili kuzaa na mwanafunzi
huyo na kukubali kuzika .
Daladala iliyobeba mwili wa Marehemu kutoka Uyole.
Wakazi wa Uyole wakiwa wameshikwa na butwaa baada yakumkosa mwenyeji wao
Mwili wa mtoto ukiwa umefunkwa na kitenge na kutelekezwa kwenye kiti
Kulia
ni Carolina Kyando akiwa na dada yake baada ya kuleta mwili wa mtoto
nyumbani kwa Mwalukoba eneo la Mama John jijini Mbeya
Majirani pande zote mbili wakingojea kujua hatma ya mazungumzo yanayo endelea baada ya Mwalukoba kurejea
******************
Vitendo vya ukatili dhidi
ya watoto na wanawake jijini mbeya vimeendelea chukua sura mpya baada ya dereva wa daladala jijini humo
kumzalisha mwanafunzi Masomo ya jioni kituo cha Juhudi kilichopo Ilomba.
.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni eneo la mama John Mtaa wa Ihanga Kata ya
Ilomba ambapo dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Aswile Mwalukoba (45
) kutelekezewa wa miezi saba ambaye alikwisha fariki baada ya kuugua kwa muda
mfupi.
Akizungumzia tukio hilo
Mwenyekiti Mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata amesema kuwa mgogoro huo umetokana na dereva huyo kugoma kuuzika mwili huo
kwakile alicho dai kuwa hivi sasa haishi na binti huyo kwa muda mrefu sasa.
Kwa upande wake binti huyo
aliyefahamika kwa jina la Calorina Kyando amedai kuwa kitendo cha yeye
kuuchukua mwili wa mtoto huyo hadi kwa baba yake unatokana kutelekezwa na bwana huyo kisha kupigwa
marakwa mara na kusababishiwa ulemavu wa sikio la kushoto baada ya kung’atwa na
mwanaume huyo.
Mwanamke huyo amefafanua kuwa
mara baada ya mtoto huyo kufariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya
Igawilo jijini humo aliamua kumpigia simu mzazi mwenzie kwa lengo la kumpa
taarifa za msiba huo.
Amesema mara baada ya kutoa
taarifa hiyo mwanaume huyo alikubali na kumueleza mwanamke huyo kuwa yuko
tayari kwa ajili ya mazikoya mtoto huyo ambapo anafanya taratibu za kuwasiliana
na ndugu zake walioko Tukuyu Wilayani Rungwe.
Amesema katika siku iliyofuata
mwanaume huyo hakupatikana kwa simu ya kiganjani na wala hakuwepo nyumbani
kwake anapo ishi eneo la Mama John hali iliyo plelekea baadhi ya majirani na
mwanamke huyo kutoka Uyole kusaidiana na kuutoa mwili huo Hospitalini hapo kwa
lengo la kufanya taratibu nyingine .
Aidha majirani hao waliamua
kuchukua mwili huo hadi nyumbani kwa Mwalukoba ambapo waliuweka kwenye kiti
ndani ya nyumba yake huku wakiendelea kumsubiri mwalukoba arudi aliko ambapo baadaye alirudi nyumbani hapo
akisindikiazwa na Mdogo wake aliyefahamika kwa jina Gabriel Mwalukoba hadi
nyumbani hapo.
Kitendo hicho cha kurejea kwa
mwanaume huyo kilifanya mwenyekiti wa mtaa huo Ndugu Emanuel Mwasibata kuhoji
juu ya kutoweka kwa nyumbani kwakwe kwa
muda wa siku mbili huku kukiwa hakuna mawasiliano yoyote.
Baada ya kikao cha muda mrefu kati ya pande
zote mbili mwanaume huyo alikubali kuupokea mwili huo na hivyo kuanza kufanya
taratibu za mazishi ambapo mazishi hayo yalifanyika katika makaburi ya Iyela
mida saa 12 jioni na kuhudhuriwa na familia zote mbili pamoja na majirani wengine
kutoka Uyole na Mama John.
No comments:
Post a Comment