Kahaba
mmoja alijikuta akiambulia kichapo kikali toka kwa vijana wa kiislamu
baada ya kunaswa akijiuza karibu na msikiti wao..
Wakati
mwanamke huyo akicharazwa bakora, nguo ya ndani ilimvuka huku akipiga
kelele kuwa hatarudia kufanya hivyo na kama akirudia basi akatwe kichwa.
Kutokana
na kukerwa na vitendo hivyo, vijana hao wanaofanya ibada katika msikiti
huo, waliamua kuwatafuta vijana wa ulinzi shirikishi na kuwapa kazi
hiyo ya kuwakamata na kuwacharaza bakora kisha kuwapeleka katika kituo
hicho cha polisi.
“Tumeamua
kuwakamata na kuwacharaza bakora, hawana ustaarabu wala busara hawa,
wanakojoa na kutupa kondomu hovyo, “ alisikika mmoja wa vijana hao.
Mmoja
wa vijana hao aliyekuwa akisimamia kwa karibu zoezi hilo, aliwaambia
waandishi wetu kuwa wameamua kufanya hivyo na litakuwa zoezi endelevu
kutokana na wanawake hao kutokuwa wasikivu kwani kila wanapoambiwa juu
ya kukaa mbali na nyumba hiyo ya ibada hawasikii.
Alisema
kuwa siku moja wanawake hao walimtoa udhu muumini mmoja ambaye alikuwa
akienda kuswali alfajiri baada ya kumshika na kusababisha akose
kuhudhuria swala siku hiyo.
Hata
hivyo, wakati mahojiano yanaendelea, mmoja wa askari waliokuwa zamu
aliamuru mwanamke huyo aingizwe lokapu kusubiri kesho yake aunganishwe
na wenzake kisha wapelekwe mahakamani.
Habari
zilizotufikia ni kwamba baada ya kufikishwa mahakamani na kukutwa na
kosa la uzururaji, wakahukumiwa kifungo cha miezi sita jela au faini ya
shilingi elfu hamsini ambapo walilipa kiasi hicho na bado wanaendelea na
biashara hiyo maeneo hayo.
GPL