Wednesday, August 14, 2013

MWANAFUNZI ATEKWA NA KUFANYISHWA NGONO

KWA SIKU NNE

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Marangu inayomilikiwa na kanisa Katoliki jimbo la Moshi, (jina limehifadhiwa) alitekwa na kukufungiwa kwenye hoteli moja ya kitalii mjini hapa na kufanyiwa vitendo vya ngono kwa muda wa siku nne mfululizo.
Mwanafunzi huyo anadaiwa kutekwa Agosti 6 mwaka huu na kijana mmoja (jina linahifadhiwa) mfanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi (Airtel) mjini Dodoma.
Akizungumza jana na Tanzania Daima Jumatano, kaka wa mwanafunzi huyo, Joseph Temba, alidai mdogo wake alitekwa na mtu huyo na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa.
Alisema walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Agosti 10, mwaka huu, katika baa moja akiwa na mdogo wake baada ya raia wema kutoa taarifa za kuonekana kwake.
Kwa mujibu wa kaka wa mwanfunzi huyo siku ya tukio alipokea simu kutoka kwa mwangalizi wa wanafunzi (matroni) akimjulisha kutokuwapo bwenini kwa mdogo wake na ndipo walipoanza kufuatilia na kutoa taarifa kituo kikuu cha polisi mjini Moshi na kupewa namba Mos/RB/9196/2013.
Alisema siku iliyofuata ya Agosti saba jioni walipokea simu kutoka kwa watu wa karibu wakiwataarifu kuwapo katika hoteli hiyo mdogo wake lakini baada ya kufika walinyimwa kuona kitabu cha wageni ili kuangalia orodha ya majina ya wageni waliofikia hapo ili kujiridhisha kama mtuhumiwa huyo alikuwapo mahali hapo.
Hata hivyo alisema jioni ya Agosti 10 walipokea taarifa za kuonekana kwenye baa hiyo mtuhumiwa akiwa na mdogo wake na kuwajulisha polisi na hatimaye kufanikiwa kumtia mbaroni ambapo hadi sasa bado anahojiwa na jeshi la polisi.
Chanzo cha kutekwa kwa mwanafunzi huyo ni mawasiliano ya simu baina ya mtekaji na mwanafunzi huyo ambapo inadaiwa mtuhumiwa huyo alimrubuni mwafunzi huyo kuacha masomo na kwamba angemtafutia nafasi kwenye shule kubwa za kimataifa.
Inadaiwa kwamba mwanfunzi huyo alikubaliana na propaganda hiyo na kutoka shuleni jioni ya Agosti 6 na kumfuata mtuhumiwa kwenye gari lake na kwenda naye hadi Moshi mjini umbali wa kilomteta 50 kutoka shule ya sekondari Marangu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema hana taarifa za kutekwa kwa mwanafunzi huyo kwa kile alichodai alikuwa ametingwa na majukumu ya kikazi mjini Arusha na kuahidi kulifuatilia baadaye.
Tanzania daima

No comments: