Wednesday, September 18, 2013

Historia ya kuacha kunywa pombe na kulewa


Nilipokuwa mnywaji niliamini kuwa siwezi kuacha pombe kwa kuwa kabila langu linadai mwanaume wa ukweli lazima anywe na pombe ni sehemu muhimu ya utamaduni wetu. then mijini tunaambiwa kuwa wajanja ni wale wanaokunywa.

nilipokuwa naelekea kulewa, nilijiona naeda kufanya jambo la busara, wakati nalewa nilijiuliza uko wapi utamu na faida za pombe? ebwana utamu wa bia baridi uko pale kwenye kuimeza pale kwenye koo wakati inakaribia kushuka tumboni, basi! kilchobaki ni mzigo

then wakati nimelewa nilijiuliza sasa ninafaida gani? mbona nashindwa kutembea, naongea hovyo, kila mwanamke ni mzuri, nanuka pombe nk?

ngoma kesho yake sasa, mning'inio (hangover), mateso mpaka ugonjwa, walevi wenzangu walinishauri kunywa tena eti nazimua! kuna siku nilikunywa matapu matapu yale yatokayo arusha na siku nyingine nikanywa gongo ya kihaya (kaliiinya), nililewa siku mbili na ugonjwa juu!

nilijiona siwezi kuacha pombe, nakumbuka rafiki yangu mmoja wa kipare aliniambia kuwa ninaweza na akanihakikishia kuwa naweza akasema kama nabishi, basi nijaribu kuacha pombe! nikajaribu siku hiyo (maana nilikuwa nakunywa kila siku), ikapita, wiki, then mwezi.

nikajisemea kuwa kumbe nikijidhibiti itakuwa poa kwa hiyo ninywe kidogo kidogo, baadae nikaona kama bado ni utumwa maana mbele ya pombe, maji, soda na juice, nilichakua pombe, nikaona bado innanitesa, nikasema sasa basi kwenda mbali.

changamoto ni maneno ya watu wanaoisifia pombe na kutudharau tusiokunywa, eti inakuletea marafiki, inapunguza mawazo, sijui vinywaji vingine ni vya watoto wadogo etc. kwa ufupi pombe ni addiction ndio maana matangazo yote ya vilevi hayakwambii kunywa bali yanakwambia onja, wanajua ukionja hutorudi nyuma ila kuacha inawezekana kabsi utakapo acha kuitukuza!

No comments: