Dr Wiliam Mgimwa |
KUELEKEA
uchaguzi mkuu mwaka 2015 mbunge
wa jimbo la kalenga na waziri fedha na uchumi Dr Wiliam Mgimwa ameanza
kuingia na hofu ya kupata upinzani mkali katika jimbo lake la
uchaguzi na kuwataka wapiga kura kuwapuuze wadau wa maendeleo
wanaofika kusaidia kutatua kero za wananchi.
Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ,John Adam na Sarah Sanga wakazi wa kata ya Nzihi walisema kuwa hawakutarajia kusikia mbunge wao akionyesha kuwabeza watoto wao wanaofika katika vijiji vyao walivyozaliwa kusaidia matatizo ya wananchi.
Alisema Adam kuwa ni vema wabunge na madiwani kuendelea kuwa na mshikamano wa kweli kwa wadau mbali mbali wa maendeleo wanaofika kusaidia shughuli za maendeleo katika maeneo yao badala ya kuendelea kuingizwa misaada hiyo katika sura ya kisiasa .
Kwani alisema kuwa hatua ya mbunge Dr Mgimwa kuwataka wananchi wa jimbo hilo la Kalenga kuwapuuza watu mbali mbali wanaofika kusaidia shughuli za kimaendeleo katika jimbo hilo ni kauli isiyo na faida kwa maendeleo ya wana kalenga .
" Hivi kweli siasa itugawe wananchi na familia zetu ...leo mtoto wetu anapokuja kutusaidia misaada ya kimaendeleo tukatae kwa sasa mbunge wetu hapendi watu hao kutusaidia sasa nini maana ya maendeleo"
Huku Bi Sanga akimtaka mbunge Dr Mgimwa kuachana na hofu ya kisiasa na kuwa wanaoweza kufanya mabadiliko ya mbunge ama chama kipi kitawale jimbo la Kalenga ni wananchi ambao mwisho wa siku wanapima kazi iliyofanywa na mbunge ama diwani husika na kama hakuna jipya hawataangalia mtu wala chama wanatoa hukumu .
Mbunge Mgimwa katika moja kati ya mikutano yake aliyoifanya katika jimbo la Kalenga alipata kutoa kauli iliyonukuliwa na gazeti la Majira la Jumamosi tarehe 28/9/2013 kauli inayoonyesha wazi kuwa ameanza kupata hofu ya kisiasa jimboni baada ya kutamka wazi kuwa wapo watu wanazunguka kutoa misaada vikiwemo vitanda katika Hospital ya Ipamba .huku zikiwa ni siku chache kupita toka mkazi wa Nyamihuu Jackson Kiswaga kukabidhi msaada huo wa vitanda katika Hospital hiyo kama fadhila yake kwa Hospital kutokana na kulazwa hapo na kuhudumiwa vema ,msaada ambao hata hivyo mbunge huyo anadaiwa kuwa na taarifa nao.
No comments:
Post a Comment