Sunday, October 27, 2013

UCHAGUZI UNAOENDELEA WA TFF HALI TETE WAANDISHI WA HABARI WAFUKUZWA UKUMBINI,WASEMA HAWATAANDIKA CHOCHOTE


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA),Juma Pinto akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Water Front,kunakofanyika Uchaguzi wa Rais na viongozi mbali mbali wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ambapo hadi sasa hakuna Mwandishi yeyote alieruhusiwa kuingia kwenye Ukumbi huo kwa madai kwamba Waandishi hawausiki na Uchaguzi huo,kwani waandishi jukumu lao ni kusubiria kupewa matokeo tu ya uchaguzi huo,kauli iliyotolea na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi,Ndg. Hamidu Mbwezeleni.Jambo hilo liezua tafrani kidogo kwenye Eneo hilo hasa pale Watu wa Usalama (Polisi) walipowataka Waandishi kuondoka kwenye Eneo hilo la Uchaguzi.Mwenyekiti wa TASWA,Juma Pinto amewataka Waandishi wa Habari kuachana na Uchaguzi huo na kutoripoti chochote,kwani kilichoonyeshwa ni dharau kubwa kwa waandishi wa Habari na watanzania wote nchini wanaopenda Michezo.CHANZO MICHUZI JR BLOG

No comments: