Saturday, January 5, 2013

MABINTI WA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI WAIKIMBIA CCM NA KUJIUNGA NA CHADEMA

MABINTI WA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI WAIKIMBIA CCM NA KUJIUNGA NA CHADEMA



Esther Wassira
Watoto wa kike wa waziri wa nchi ofisi ya Rais Mheshimiwa Stephen Wassira, wameamua kutokuwa wanafiki kwa kuamini chama tawala cha baba yao na kuchukua kadi za uanachama wa CHADEMA.

Mabinti hao ni pamoja na muimbaji aliyewahi kutamba na wimbo wake ‘Sheila’ Esther Wassira na dada yake Lilian Wassira.

“Imefikia wakati tunahitaji kuona mabadiliko Tanzania kwasababu haitoshi kukaa na kusikia vilio vya watanzania kila siku, ukipita kote wanasema maisha magumu, serikali haifanya chochote, migomo maandamano yamekuwa yakizidi,” alisema Esther ambaye ni mwanasheria wakati wa kupokea kadi hizo mbele ya katibu mkuu wa chama hicho Dr. Wilbrod Slaa.


“Katika sehemu kama hiyo tuliyofikia watanzania wanachohitaji ama mahali popote katika nchi kinachohitajika ni mabadiliko almost katika kila sekta. Kwahiyo mabadiliko hayo kutokea hayawezi kutokea kama tutabaki na malengo yale yale, sera zile zile, mifumo ile ile , uongozi ule ule, tunahitaji vitu vipya.”

Naye Lilian alisema, “Mienendo ya hiki chama nimeifuatlia na nina imani nao, nimesikiliza sera zao na nimezielewa. 

Sifuati ukongwe wa chama na hiki chama kina mizizi ya akina nani. Nafuata chama kwasababu kwanza mwamko walionao, sera zao za movement for change na jinsi nilivyoona hawaongei tu lakini tumeona wazi.

 Tunaona yaani wanavyopambana, tunaona na tunajua kwanini ilikuwa vile, sisi si wajinga. Sasa kwasababu tunaona,na sisi tumeamua tuwe sehemu ya CHADEMA.

No comments: