Bashir na Kiir wakutana Addis Ababa |
Matukio Duniani |
Kundi la Fatah laandaa mkutano wa hadhara katika Ukanda wa Gaza |
Mamia ya Maelfu ya wafuasi chama cha rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina, Mahmud Abbas, Fatah, leo wamefanya mkutano wao wa kwanza wa hadhara katika Ukanda wa Gaza, tangu kundi la Hamas lilipochukua udhibiti wa eneo hilo mwaka wa 2007. |
Ndege za kivita za Syria zaendelea kuwashambulia waasi |
Ndege za kivita za Syria na wanajeshi leo wameendeleza mashambulizi dhidi ya waasi karibu na mji mkuu Damascus, siku moja baada ya bomu la kutegwa ndani ya gari kuwauwa watu 11 kaskazini ya mji huo. |
Wafungwa 80 wa Taliban waachiwa huru na serikali ya Afghanistan |
Takribani wafungwa 80 wa Taliban ambao wakati mmoja waliwahi kuzuiwa katika gezera la Bagram jeshi la Marekani, leo wamewachiwa huru na serikali ya Afghanistan huku kukiwa na matarajio kwamba hatua hiyo huenda ikasaidia katika juhudi za maridhiano. |
Msichana wa Pakistan aliyeshambuliwa na Taliban aondoka hospitalini |
Mtetezi wa haki ya elimu nchini Pakistan, Malala Yousafzai, ambaye alishambuliwa na wanamgambo wa Taliban karibu miezi mitatu iliyopita, ameruhusiwa kuondoka hospitalini Uingereza. |
Rais wa Venezuela Chavez yuko katika hali dhaifu |
Serikali ya Venezuela imesema kwamba rais Hugo Chavez anatibiwa kutokana na matatizo ya kupumua baada ya kukumbwa na maambukizi ya mapafu. |
EU yasema tarehe ya mazungumzo ya nyuklia na Iran bado haijajulikana |
Umoja wa Ulaya umesema kwamba hakuna tarehe iliyowekwa kwa mazungumzo zaidi kuhusu mpango wa Iran wa nishati ya nyuklia, huku ukitaraji kwamba tarehe hiyo itatangazwa hivi karibuni. |
UNICEF: Watoto wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kujiunga na waasi |
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia watoto, UNICEF, limesema lina wasiwasi kuhusu idadi inayoongezeka ya watoto wanaosajiliwa kujiunga na makundi yenye silaha katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, huku rais wa nchi hiyo Francois Bozize akikabiliwa na uasi katika upande wa Kaskazini. |
No comments:
Post a Comment