Kwa
siku nzima nimekuwa nakusanya mawazo, kutoka kwa wapenzi mbali mbali
ambao walikuwa wananisaidia uchunguzi wangu juu ya namna wanavyoshiriki
tendo la ndoa na kulidhika.
Wengi
kati ya hao kwa kiwango tofauti cha kuanzia mara tatu na kuendelea
waliniambia kuwa hawatosheki na viwango hivyo na kuliacha swali kubaki
kuwa wapenzi wakutane mara ngapi kwa wiki ili watosheke?
Jibu la swali hili linapatikana baada ya kutambua kitu kimoja muhimu, nacho ni chanzo cha kutosheka hasa nini?
Katika
hali ya kawaida kutosheka kupo zaidi akilini na wala si mwilini, hii
ina maana kwamba watu wanaodhani kuupa mwili mahitaji zaidi kadiri
unavyodai ni njia ya kuutosheleza wanajidanganya, kwa sababu tamaa ya
mwili haitoki mwilini bali kwenye akili ya mtu.
Kwa
msingi huo mtu akitaka kutosheka na penzi la mpenzi wake, ni lazima
kwanza aitosheleze akili yake na kile anachopata, zoezi ambalo
atalifikia kwa kutathimini uwezo wake wa kufanya mapenzi na wa mpenzi
wake. Wengi kati ya watu wanaodai hawatosheki kimapenzi ni wale
wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia
uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Ukiyaendesha
mawazo yako kufanya mapenzi mara kwa mara, hutatosheka hata ukipewa
kila saa, kwa sababu fikra zako unazijenga zaidi ya unachopata.
Uchunguzi
unaonesha kuwa watu ambao akili zao zimejaa mawazo ya ngono, hawawezi
kulala bila kufanya mapenzi, lakini watu hao hao, ukiwapa matatizo
yatakayochukua sehemu kubwa ya mawazo yao kwa mfano, kuwafunga jela,
kuwafukuza kazi, kupata msiba, utashangaa wanaweza kukata wiki bila
kusumbuliwa na tamaa ya ngono.
Hii ina maana kwamba unavyowaza ndivyo unavyotenda. Kitaalamu
kinachofanya mapenzi ni mawazo, ndiyo maana wapo wanaojichua wenyewe
kwa kutumia mawazo yao na kupata raha. Kila mmoja akijenga heshima juu
ya fikra zake na kujali hisia zaidi tutakuwa na watu wengi wanaofurahia
tendo la ndoa bila kujali wanalipata mara ngapi kwa wiki.
Uchunguzi
wangu umebaini kuwa watu wengi hasa wapenzi wa siku nyingi na
wanandoa, wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa
pamoja, lakini si kwa kuheshimu fikra na hisia zao, jambo ambalo husababisha ladha ya mapenzi kuwa ya asilimia ndogo, ukilinganisha na mahitaji halisi ya mawazo yao.
Upo
ushahidi wa kutosha kwa wanandoa wengi kupata msisimko mdogo wanapokuwa
na waume/wake zao katika tendo la ndoa tofauti na wanapopata wasaa wa
kusaliti ndoa kwa hawara zao.
Watu wa
aina hii wasiseme kuwa hawatosheki na tendo la ndoa kwa sababu
wanakutana na wapenzi wao mara chache zaidi, bali wanakutana katika
mhemko wa chini usioweza kulifanya tendo hilo kuwa na raha ya kutosha.
Labda msomaji wangu utaniuliza, tatizo la kupata msisimko mdogo kwa mtu unayemzoea linachangiwa na nini? Jibu litakuwa ni MAWAZO ya mtu mwenyewe.
Ukichunguza utagundua kuwa, wapenzi wengi hasa wazoefu huwa hawapeani nafasi katika mawazo, kama wanavyotoa nafasi kwa wapenzi wa pembeni,
hili ndilo tatizo linalopunguza msisimko wa kimapenzi na kuondoa hali
ya kutosheka na penzi. Kama mtu anataka mpenzi wake amtosheleze, basi
hana budi kumkuzia mwenza wake hisia kiasi cha kumtamani.
Niulize
swali, hivi ni mara ngapi wewe unayesema hutosheki na penzi ulishakaa
peke yako ukamvutia taswira mpenzi wao kabla hajarudi nyumbani kiasi
cha kupata msisimko wa kutana naye kimwili?
Wengi wetu
hatufanyi hivyo, hatuna vitu vinavyotuvutia kwa wake/waume zetu, jambo
ambalo hutufanya tukikutana nao kimwili kwa kutimiza desturi tu na
kubaki na kiu zetu za penzi.
Lakini
uweli unabaki kuwa wapenzi wakikutana kipindi cha msisimko mkubwa na
kupeana mahaba kwa usahihi hata ikiwa ni mara moja kwa wiki watatosheka.
No comments:
Post a Comment