Saturday, January 5, 2013

HABARI MOTOMOTO



DRC: Baraza la usalama lawaekea vikwazo Waasi wa M23


Waasi wa M23 huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamesema vikwazo vilivyowekwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa havitateteresha jitihada zao za mazungumzo ya amani kwa upande wao.

Matukio ya Kisiasa


Hali ya rais Hugo Chavez iko imara, asema makamu wa urais Venezuela


Makamu wa rais nchini Venezuela Nicolas Maduro amesema rais wa nchi hiyo Hugo Chavez amepata fahamu na kutambua kinachoendelea baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na rais huyo kuugua saratani


Masoko ya fedha yashusha pumzi


Masoko ya fedha yameimarika kote duniani kufuatia hatua ya makubaliano ya bajeti nchini Marekani na kuepusha ongezeko la kodi kwa wananchi. Wadadisi wa masuala ya kiuchumi wanasema balaa kubwa limeepukwa.


Seleka Wako Tayari Kuzungumza


Waasi wa Seleka wametangaza kusitisha mashambulio kuelekea mji mkuu Bangui na kutuma ujumbe katika mazungumzo ya Libreville nchini Gabon.

Matukio Duniani

Katuni za Mtume zachapishwa tena Ufaransa

Gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa leo limechapisha tena katuni za kiongozi wa Waislamu, Mtume Muhammad, hivi leo, ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kitendo kama hicho kuzusha ghasia ulimwenguni.

Watu 30 wauawa Syria

Watu wapatao 30 wameuawa nchini Syria hivi leo, baada ya ndege za kijeshi kukishambulia kituo kimoja cha mafuta kwenye kiunga Muleiha, karibu na mji mkuu Damascus.

Watu watano wauawa Iraq

Watu watano wameuawa katika mkururo wa mashambulizi nchini Iraq hivi leo.

Israel yawahamisha Mabedui wa Kipalestina

Jeshi la Israel limezihamisha kwa nguvu familia kadhaa za Mabedui wa Kipalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi, wakati jeshi hilo likifanya mazoezi yake.

Thamani ya hisa yaimarika duniani

Bei ya hisa kwenye masoko ya fedha duniani imepanda juu ghafla, baada ya Bunge la Marekani kuunga mkono mpango wa kuiepusha nchi hiyo na mserereko wa kiuchumi.

Maduro asema Chavez anaendelea vyema

Makamu wa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, amekanusha uvumi kuhusiana na kuzorota kwa afya ya Rais Hugo Chavez, aliye matibabuni nchini Cuba.

Iran kujenga eneo lisilopitisha mwangaza

Iran imedhamiria kuweka eneo la kwanza la nchi hiyo kutokuruhusiwa kufikwa na mwangaza katika kisiwa chake cha Qeshem.

Rais wa Cyprus aukataa ubinafsishaji

Rais Dimitris Christofias wa Cyprus, amesema atakataa maombi yoyote kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa, ya kutaka kuuza mashirika yanayomilikiwa na serikali, kama mpango wa kuhitimisha makubaliano ya kupata fedha za kuikoa nchi hiyo inayotumbukia kwenye mgogoro wa kiuchumi.

No comments: