RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII- UDOM ATIWA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 15.6
RAISI
WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA
DODOMA(UDOM) IDD MOHAMED NA WAZIRI WAKE WA FEDHA IBRAHIM MATATA
WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI
6,MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA
LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
TAARIFA TOKA KWA MDAU JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG ZINASEMA KUWA
RAISI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII, SANAA NA LUGHA AMBAYE PIA NI
MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU ANAYESOMA BCOM ACCOUNTING ANAYEFAHAMIKA KWA
JINA LA IDD MOHAMED ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KITUO CHA POLISI
UDOM KWA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI
6.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA JANA SIKU
YA ALHAMISI AKIWA NA MWENZAKE AMBAYE PIA ALIKUWA WAZIRI WA FEDHA WA
KITIVO HIKO IBRAHIM MATATA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU
BCOM ACCOUNTING NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO HIKO CHA POLISI.
MARA BAADA
YA KUKAMATWA WALIKUTWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 7 LAKI 2 NA 24
ELFU.(Shilingi 7,224,000 ZA Kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa kwenye
account ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na
Lugha na kupelekwa katika Akaunti ya Mtu Binafsi ambaye ni Waziri wa
Fedha wa Kitivo hiko Ndugu Ibrahim Matata.
Chanzo hicho
kiliendelea Kujuza kuwa Awali Raisi Huyo Anahusika na kosa la kuomba
Rushwa ya Shilingi Milioni 1 na laki 1 katika Duka lililopo Katika Bweni
namba 13 (Block 13 ).
Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa
Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari
kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa ili kuweza Kufikishwa
mahakamani
Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka
katika Vyanzo vya habari Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri
wake Wa fedha watafikishwa Mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa
Shilingi Milioni 15 na laki 6 ambapo waliweza kuzitoa na kuweka katika
akaunti ya Waziri Wa Fedha Ibrahim Matata na kufanikiwa kuchukua Sh
Milioni 7 laki 2 na Ishirini na Nne elfu ambazo ndio walikamatwa nazo
Mkononi.
Hatimaye Bunge la Serikali ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha
Sayansi ya Jamii ,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma linatarajiwa
kukaa leo Saa 10 Jioni ili kuweza kutoa uamuzi wa Kumvua madaraka na
kufikisha baadhi ya Ushaidi wa Sauti wakati Raisi huyo akiomba Rushwa
katika Duka lililopo Block 13.
No comments:
Post a Comment