SAKATA LA MWANAFUNZI ALIFIA HOTEL YA SOUTHERN RESORT LAZUA MASWALI MENGI....!
Ndugu na jamaa wa marehemu Jackline Musa Matiko, wakitoa mwili wa ndugu yao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
------
Akizungumza na uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, baba wa marehemu, Mussa Matiku alisema
baada ya kuikuta maiti ya mtoto wake kando ya bwawa katika hoteli hiyo
na kuichunguza shingo yake aliiona imelegea na tumbo lake halikujaa
maji kama watu wanaokufa kwa maji wanavyokuwa. Alisema kwa vigezo hivyo ni wazi kwamba mwanaye hakufa maji na amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliomuua kikatili binti yake.
Naye mjomba wa marehemu ambaye alikuwa na Jackline kabla ya kifo chake aliyejitambulisha kwa jina moja la Abdul, alisema binti huyo alitoka nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Mazizini Ukonga kwenda Gongo la Mboto kwa bibi yake kusherehekea Sikukuu ya Mwaka Mpya.
Jackline Musa Matiko (15) enzi za uahi wake.
-------
“Baada
ya kufika pale na kupata chakula cha mchana pamoja na ndugu zake,
Ilipangwa kwenda kutembea kokote walikohitaji ambapo walichagua
kwenda Quality Centre.Aliongeza kuwa walipofika huko waliamua kwenda Southern Beach Resort Kigamboni ambako ndiko waliposherehekea siku hiyo ya mwaka mpya.
Akadai kuwa wakati wakiwa huko walikuwa wakinywa vinywaji laini, kucheza muziki pamoja na kuogelea lakini akawapa tahadhari kuwa kila anayetoka kwenda sehemu yoyote ahakikishe anarejea walipokuwepo wenzake.
Akaongeza: “Ilipofika saa moja usiku Jackline hakuonekana ndipo nikawa na hofu na kuanza kumtafuta huku nikiwa nimewaambia wenzake wasitoke eneo nililowaacha.
“Kutafuta kwangu hakukuzaa matunda nikaenda kwa uongozi wa bichi kueleza kuhusiana na tukio hilo nao pia wakatangaza kwa kutumia kipaza sauti kuwa mtoto amepotea huku akiwa anatajwa jina lake pia hapakuwa na mafanikio.”
Baada ya kuona jitihada za kumpata Jack hazikuzaa matunda walikwenda kutoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Vijibweni kisha wakarudi nyumbani.
---------------
Abdul
aliongeza kuwa anachohisi uongozi ulishajua kuwa tukio hilo lilitokea
lakini waliamua kumficha kwa kuhofia kama wangesema ukumbi
ungefungwa na biashara ingekuwa ndiyo mwisho kwa siku hiyo.Aliongeza kuwa asubuhi walipigiwa simu na polisi wakielezwa kuwa kuna mtoto aliokotwa akiwa amekufa na walipokwenda kuhakikisha wakakuta ni Jackline.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Engelbert Kiondo alipohojiwa alisema upelelezi wa tukio hilo ulisubiri ripoti ya madaktari ili kujua kama mtoto huyo alikufa maji au aliuawa kisha kutupwa karibu na bwawa la hoteli hiyo.
Marehemu Jackline alizikwa Januari 3, mwaka huu eneo la Moshi Bar Ukonga.
No comments:
Post a Comment