Friday, January 11, 2013

Sakata na mapenzi ya jinsia moja yaandama chuo kikuu cha Victoria 10 Januari, 2013 - Saa 12:43 GMT Facebook Twitter Tuma kwa rafiki yako Chapisha Tangazo katika gazeti la Uganda linalohimiza mswada huo kufutiliwa mbali Chuo kimoja kikuu nchini Uingereza, kimesitisha uhusiano wake na chuo kikuuu kimoja nchini Uganda , kupinga uamuzi wa wabunge wa nchi hiyo wa kuidhinisha mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja. Chuo kikuu cha wa Buckingham kisema kimesikitishwa na mswada huo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, kikisema kuwa kinakandamizi juhudi za kuafikiwa kwa uhuru wa kujieleza na ushirikiano. Chuo hicho sasa kimestangaza kuwa kimesitisha ushirikiano wake na chuo kikuu cha Victoria. Hata hivyo chuo hicho cha Buckingham, kimesema wanafunzi wanaoendelea na masomo yao kwa sasa hawataadhiriwa na uamuzi huo. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chuo hichi cha kibinfasi, uamuzi huo umeafikiwa baada ya mazungumzo na shirika la Edulink, lililo na makao yake mjini Dubai, ambalo ni mmiliki wa chuo hicho cha Victoria. Taarifa hiyo imesema kuwa chuo hicho kimeshindwa kutekeleza na kutimiza sheria za Uganda na Uingereza inayozuia ubaguzi. Chuo cha Victoria hakitafungwa Chuo kikuu cha Buckingham Wasimamizi wa chuo hicho sasa wanesena kuwa ushirikiano wao na chuo kikuuu cha Burkingham umesitishwa rasmi. Kufuatia tangazo hilo, chuo kikuu cha Victoria kitasitisha kutoa shahada katika masomo ya usimamizi wa biashara, uhasibu, uandishi wa habari na masomo ya teknolojia ya komputa hatua ambayo itawaadhiri takriban wanafunzi mia mbili. Kaimu naibu wa Chansella wa chuo cha Victoria, David Young, chuo hicho kitaendelea kutoa mafunzo ya masomo mengine ikiwa na pamoja na sayansi ya utabibu na afya ya jamii ambayo shahada zake hazitolewi na chuo cha Burkingham. Chuo kikuu cha Victoria, kilifunguliwa mwaka wa 2011, na rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na Chansela wa chuo hicho ni aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Apolo Nsibambi.

Sakata na mapenzi ya jinsia moja yaandama chuo kikuu cha Victoria

 
Tangazo katika gazeti la Uganda linalohimiza mswada huo kufutiliwa mbali
Chuo kimoja kikuu nchini Uingereza, kimesitisha uhusiano wake na chuo kikuuu kimoja nchini Uganda , kupinga uamuzi wa wabunge wa nchi hiyo wa kuidhinisha mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja.
Chuo kikuu cha wa Buckingham kisema kimesikitishwa na mswada huo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, kikisema kuwa kinakandamizi juhudi za kuafikiwa kwa uhuru wa kujieleza na ushirikiano.
Chuo hicho sasa kimestangaza kuwa kimesitisha ushirikiano wake na chuo kikuu cha Victoria.
Hata hivyo chuo hicho cha Buckingham, kimesema wanafunzi wanaoendelea na masomo yao kwa sasa hawataadhiriwa na uamuzi huo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chuo hichi cha kibinfasi, uamuzi huo umeafikiwa baada ya mazungumzo na shirika la Edulink, lililo na makao yake mjini Dubai, ambalo ni mmiliki wa chuo hicho cha Victoria.
Taarifa hiyo imesema kuwa chuo hicho kimeshindwa kutekeleza na kutimiza sheria za Uganda na Uingereza inayozuia ubaguzi.

Chuo cha Victoria hakitafungwa

Chuo kikuu cha Buckingham
Wasimamizi wa chuo hicho sasa wanesena kuwa ushirikiano wao na chuo kikuuu cha Burkingham umesitishwa rasmi.
Kufuatia tangazo hilo, chuo kikuu cha Victoria kitasitisha kutoa shahada katika masomo ya usimamizi wa biashara, uhasibu, uandishi wa habari na masomo ya teknolojia ya komputa hatua ambayo itawaadhiri takriban wanafunzi mia mbili.
Kaimu naibu wa Chansella wa chuo cha Victoria, David Young, chuo hicho kitaendelea kutoa mafunzo ya masomo mengine ikiwa na pamoja na sayansi ya utabibu na afya ya jamii ambayo shahada zake hazitolewi na chuo cha Burkingham.
Chuo kikuu cha Victoria, kilifunguliwa mwaka wa 2011, na rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na Chansela wa chuo hicho ni aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Apolo Nsibambi.

No comments: