ARSENAL 3-1 NA BAYERN, SASA YASUBIRI MIUJIZA MECHI YA MARUDIANO
Bayern waliwasambaratisha vijana wachovu wa Wenger kupitia mabao ya Toni Kroos, Thomas Muller na Mario Mandzukic.
 Shangwe za mashabiki wa Bayern
Hata
 pale Podolski alipoipunguzia Arsenal bao dakika ya 55 na kuwa 2-1 bado 
ilionekana Arsenal wana mlima mrefu wa kupanda ili kushinda mechi ya 
marudiano ugenini.
Podolski akiifungia Arsenal bao pekee
Vijana
 wa Wenger walibakiwa na tumaini pekee katika ligi ya mabingwa baada ya 
kutolewa na Blackburn kwenye kombe la FA Jumamosi iliyopita.
Walianza kupumbazwa dakika ya nane pale Kroos alipoujaza mpira wavuni kupitia krosi ya Thomas Muller.
| 
Kroos (kushoto) baada ya kufunga bao la kwanza  
Dakika
 ya 21 mambo yakawa mabaya zaidi baada ya mpira wa kona wa Daniel Van 
Buyten kutemwa na kipa Szczesny na kumkuta Muller aliyeujaza wavuni na 
kuandika bao la pili. | 
| 
Muller akiipatia Bayern bao la pili 
Bayern
 Munich ikapigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Arsenal dakika ya 
77 baada ya Mandzukic kumalizia mpira wa krosi ya Arjen Robben 
aliyetokea benchi. 
Katika mchezo mwingine, Porto iliifunga Malaga 1-0 | 
 
 
No comments:
Post a Comment