KIMWANA WA TWANGA IPO PALE PALE, MAIMATHA ATUPWA NJE

Mmoja wa
viongozi wa Aset, Hassan Rehani ameiambia Saluti5 kuwa tofauti na uvumi
uliozagaa kuwa mchuano huo umeyeyuka, ni kwamba Kimwana wa Twanga
itaendelea kuwepo kila mwaka.
Rehani
amesema badiliko pekee ni kwamba aliyekuwa mratibu wa Kimwana wa
Twanga, Maimatha wa Jesse (pichani chini) hatakuwepo tena katika mchuano
huo kwa vile hakidhi tena vigezo vinavyohitajika.

Hivi
karibuni Maimatha alitangaza kuanzisha kinyang’anyiro kingine
kitakachojulikana kama Kigoli kwa kushirikiana na Extra Bongo na Hassan
Rehani ameitaja hali hiyo kama moja ya vitu vinavyomuondolea Maimatha
vigezo vya kuratibu Kimwana wa Twanga.
Kwa
mujibu wa Hassan mchuano huo ambao hushirikisha mabinti wenye vipaji
vya kunengua mitindo mbali mbali ya Twanga Pepeta, utafanyika baada ya
mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Via saluti5
No comments:
Post a Comment