Friday, February 22, 2013

DIAMOND: NIMLOGE Q-CHILLAH ILI NITEMBELEE NYOTA YAKE IPI? YA KULA UNGA?

Written By Nicolaus Trac on Thursday, February 21, 2013 | 8:42 AM



MWIMBAJI supa staa wa kizazi kipya, Naseeb Abdul “Diamond” amefunguka kuwa hajawahi kusafiria nyota ya msanii mwenzake Q-Chillah.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds FM jana mchana, Diamond alisema ameshangazwa na maneno ya Q-Chillah kuwa yeye (Diamond) anamloga na kusafiria nyota yake.
“Hivi nimloge au kusafiria nyota yake ipi hiyo? …hii ya kula unga? Alihoji kwa hasira Diamond.
“Mimi najituma, nafanya kazi kwa bidii, yeye anahangaika na mastarehe yake hayo halafu anasema nasafiria nyota yake, kwa kipi haswa? Kwanza wakati mimi naingia kwenye game Q-Chillah alishapotea,” aliongeza.

Diamond ndani ya studio za Clouds FM, jana mchana
Siku kadhaa zilizopita, kupitia kipindi hicho hicho cha XXL, Q-Chillah alimshambulia Diamond kuwa anamloga na kusafiria nyota yake.


Hata hivyo Diamond aliendelea kusisitiza kuwa bado ataendelea kumsheshimu Q-Chilllah kama msanii aliyemtangulia kwenye fani.
Diamond pia alipuuza madai ya mtu anayepita kwenye vyombo vya habari kutangaza kuwa ni mganga wake na kumtaka kama ni mganga kweli basi amshushe kisanii.
Akizungumzia madai ya kukosa watu kwenye show zake za Zanzibar na Mwanza, Diamond alisema hizo ni fitna za wapinzani wake ambao huchukua picha za mapema kabla show haijaanza na kuzitumia kama kilelezo cha kuanguka kwa show zake.

No comments: