NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA VITEGAUCHUMI VYA VYA PSPF JIJINI DAR
SIKU
MOJA baada ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
kuwatembezea wadau na wanachama wake katika nyumba za mradi wa nyumba za
makazi ambazo zimejengwa na Shirika hilo eneo la Buyuni kata ya Majohe
Chanika Wilayani Ilala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene nae ametembelea na kujionea nyumba
hizo na kuumwagia sifa Mfuko huo kwa ubunifu na kuwajali wananchama
wake.
Mbene pia alitembelea Ujenzi wa jingo la Kitegauchumi la Ghorofa 35 linalojengwa na Mfuko huo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Bwana Adam Mayingu akimpa maelezo Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo
Mbene juu ya muundo kamili wa Jengo hilo la ghorofa 35 ambalo linajengwa
na PSPF jijini Dar es Salaam na litakuwa na maduka, makazi na Ofisi.
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo la PSPF Tower, Ghazi Al Shamali (kushoto)
akitoa maelezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu juu ya hatua zilizofikiwa
hadi sasa katika ujenzi huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akiangalia thamani za ndani
katika moja ya vyumba katika nyumba zilizopo ndani ya jengo hilo la PSPF
Tower ambalo ujenzi wake bado unaendelea na pindi zitakapo kamilika
zitauzwa kwa watumishi wa Serikali pamoja na Wanachama wa Mfuko huo.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), Bwana Adam Mayingu
wakiongozana kuteremka ngazi zilizopo katika moja ya nyumba (apartment)
zilizopo katika jingo hilo la PSPF Tower ambalo linaendelea kujengwa.
Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene akitembezwa ndani ya jengo hilo
na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma
(PSPF), Bwana Adam Mayingu.
Watumishi wa PSPF wakizungumza jambo ndani ya Jengo hilo.
Awali
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Zebedayo Mbene alipata fursa ya kutembelea
mradi wa ujenzi wa nyumba 491 za Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa
Umma (PSPF) zinazojengwa Buyuni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na
ambazo zimekamilika ujenzi wake na kuanza kuuzwa kwa Wanachama wa mfukjo
huo. Pichani mbele kutoka kushoto ni Gabriel Silayo, Mkurugenzi wa
Uwekezaji wa PSPF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Mbene na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha
Mshomba wakimtembeza Kiongozi huyo katika nyumba hizo.
Nyumba hizo zikiwa zimekamilika ujenzi wake na kusubiri wateja tu.
Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene akiwa na Mkurugenzi wa Fedha wa PSPF, Masha Mshomba akimtembeza ndani ya moja ya nyumba hizo.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri
wa Fedha, Janet Mbene nje ya moja ya nyumba ambazo zimejengwa na PSPF,
kwaajili ya kuwauzia wanachama wake kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment