Monday, March 25, 2013

Walemavu wasubiri huruma ya Rais Kikwete kuunda Baraza lao


 Gidion Mandes ambaye ni mlemavu wa kutoona na wakili wa kujitegemea
ambaye ni Mtanzania wa Kwanza mwenye ulemavu wa aina hiyo kufika Chuo
Kikuu.Mwaka 2010 aligombea Ubunge Jimbo la Muleba Kusini na kushindwa
katika kura za maoni za CCM dhidi ya Profesa Anna Tibaijuka.

WATU wenye ulemavu wamemuomba rais Jakaya Kikwete kumteua Mwenyekiti ili
kuharakisha uanzishaji  wa Baraza la Ushauri la Taifa la watu wenye ulemavu
kama inavyotamkwa na sheria.

Hayo yameelezwa wakati wa kikao cha kujadili masuala ya haki za watoto
wenye ulemavu na uanzishwaji wa Baraza lao kilichoandaliwa na Kanisa la
Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT)na kufanyika mjini Bukoba.

Kwa mujibu wa Mkurugezni Mtendaji wa Shirika la walemavu linaloshughulikia
sheria,maendeleo ya jamii na uchumi(Dolased)Gidion Mandesi alisema mchakato
wa uundaji wa Baraza hilo hauwezi kuunza kwani rais hajamteua Mwenyekiti.

Alisema sheria iliyotungwa mwaka 2010 inasema baada ya rais kumteua
mwenyekiti Waziri atateua Baraza la Ushauri la Taifa ambalo litasaidia
uundawaji wa mabaraza ya ushauri ya walemavu katika ngazi za Mikoa na
Wilaya.

“Hakuna utawala bora kwa walemavu na rais anatuangusha sheria ilitungwa
zamani na walengwa tupo kitu kinachokosekana ni utashi wa viongozi wetu wa
kisiasa”alisema Mandesi

Gidion MandesI ni mlemavu wa kutoona ambaye alikuwa Mtanzania wa kwanza
mwenye ulemavu wa aina hiyo kufika Chuo Kikuu ambapo hivi sasa ni wakili wa
kujitegemea aliyebobea katika masuala ya sheria.
 Nyingine ni picha mbalimbali wakati na baada ya  kikao cha wadau  wa
masuala ya watoto wenye ulemavu kilichojadili haki ya kuanzishwa kwa Baraza
la watoto wenye ulemavu Mkoani Kagera.
Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwa na wadau wa masuala ya watoto wenye ulemavu

 Na Phinias Bashaya,
Bukoba.

No comments: