|
|
Mkoa wa Kagera
unapatikana kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao makuu ya
mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es
Salaam, mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa kaskazini, Rwanda na
Burundi kwa upande wa magharibi mkoa wa Kigoma, Mwanza kwa upande wa
kusini na ziwa Victoria kwa upande wa mashariki. Vile vile mkoa wa
Kagera uko kusini mwa ikweta kati ya 1 “00” na 2”45” latitudi. Kwa
Iongitudo uko katika nyuzi 30”25” na 32”40” Mashariki mwa ‘greenwich'.
Mkoa wa Kagera ulijulikana kama “Ziwa
Magharibi” jina hili lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya
uhuru mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda.
Mkoa ulipata jina hili kutokana na mto
Kagera ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na
kumwaga maji yake katika ziwa Victoria.
Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la
kilomita za mraba 39,168 kati ya hizo kilometa za mraba 28,513 ni eneo
la nchi kavu za kilomita 10,655 ni eneo la maji. Ukiacha mbali wilaya za
Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare sehemu kubwa ya mkoa ni yenye
milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande
wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera
ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.
|
Hali ya hewa
Hali ya hewa ya mkoa
wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua
zinanyesha kwa wastani wa milimita 800-1,100 kwa mwaka kati ya mwezi
Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo
zinazowezesha kuwepo kwauoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya
mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika
ambazo ni muhium kwa shughuli za kilimo na ufugaji.
|
|
|
Wakati tunapata UHURU, mkoa wa Kagera
ulikuwa na jumla ya wilaya nne (4), wilaya hizo ni Ngara ambayo
ilianzishwa mwaka 1947, Biharamulo, Bukoba, na Karagwe mwaka 1958 ambayo
ilizinduliwa rasmi na gavana wa kiingereza Sir Richard Turnbul. Aidha,
mwaka 1975 wilaya mpya ya Muleba ilianzishwa kutoka kwenye wilaya ya
Bukoba na mwaka 2007 wilaya ya Chato na Missenyi zilianzishwa na kuunda
jumla ya wilaya 7 za mkoa wa Kagera.
Kwa sasa mkoa wa Kagera una jumla ya
wilaya saba (7) na halmashauri 8. Wilaya hizo ni Bukoba, Muleba,
Biharamulo, Ngara, Chato, Karagwe, Missenyi na Ngara. Halmashauri ni
Bukoba Manispaa, halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Muleba, Biharamulo,
Ngara, Chato, Karagwe na Missenyi.
Kisiasa mkoa una jumla ya majimbo 10 ya
uchaguzi (Muleba 2, Karagwe 2, Ngara 1, Biharamulo 1, Missenyi 1,
Bukoba Manispaa 1, Bukoba Vijijini 1 na Chato jimbo 1).
|
IDADI YA WATU
|
|
Kwa mujibu wa
sensa ya watu na makazi ya mwaka 1967 mkoa ulikuwa na watu 658,712,
mwaka 1978 watu 1,009,379, mwaka 1988 mkoa ulikuwa na watu 1,326,183 na
mwaka 2002 watu 2,033,888. Ongezeko la idadi ya watu lilikuwa kwa
wastani wa asilimia 2.7. Aidha, mwaka 2011 kwa mujibu wa sensa ya watu
na makazi ya mwaka 2002 mkoa unakadiriwa kuwa na idadi ya watu
2,746,058.
|
|
Halmashauri Ya Wilaya
|
Idadi ya Watu
|
|
1978
|
1988
|
2002
|
MAOTEO 2011 |
Missenyi |
-
|
-
|
-
|
174,889
|
|
Bukoba (V)
|
296,462
|
343,950
|
395,130
|
467,129
|
|
Bukoba (M)
|
36,914
|
47,009
|
81,221
|
153,016
|
|
Muleba
|
217,493
|
274,447
|
386,328
|
492,404
|
|
Chato |
-
|
-
|
-
|
383,162
|
|
Biharamulo
|
165,580
|
209,524
|
410,794
|
252,218
|
|
Karagwe
|
185,013
|
292,589
|
425,476
|
542,517
|
|
Ngara
|
107,917
|
158,658
|
334,939
|
422,044
|
|
JUMLA
|
1,000,379
|
1,326,183
|
2,033,888
|
2,746,058
|
|
Chanzo: Ofisi Kuu ya Takwimu Taifa (NBS) , 2011
|
HISTORIA YA MKOA WA KAGERA
Mkoa huu haukuitwa Kagera bali ulikuwa
moja ya maeneo yaliounda jimbo lililoitwa Lake Province. Jimbo hili
lilijumuisha Wilaya ya Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baadaye
ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region' (Ziwa Magharibi) na
kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba.
Kabla na baada ya kuja kwa wakoloni
mkoa wa Kagera ulikuwa na utawala wa Kimila (Chiefdoms) uliogawanyika
katika himaya 8. Himaya hizo ni pamoja na Kyamutwara, Kihanja (Kanazi),
Kiziba, Ihangiro, Bugabo, Karagwe, Biharamulo (Rusubi) na Maruku
(Bukara).
Baadhi ya Watemi waliotawala himaya
hizo ni pamoja na Emmanuel Rukamba (Kyamtwara), Rumanyika (Karagwe),
Kasusura (Biharamulo), Lugomola (Bukara), Rutinwa (Kiziba), Kayoza
(Bugabo), Kahigi (Kihanja) na Nyarubamba (Ihangiro). Kila mtemi alikuwa
na walinzi wake walioitwa Warugaruga.
Wakazi wa asili ya Kagera ni wabantu na
wengi wao wana asili ya Bunyoro. Wanaongea lugha sawa na ile ya
Wanyoro, Wanyankole, Watoro na Wakiga. Busubi na Bugufi wana lugha na
desturi sawa na Watusi, Wahutu na Waha. Lakini makabila hayo ni ya
Wabantu wa Ziwa (Interlacustrine Bantu) na yanafanana mila na desturi.
Makundi hayo yaligawanyika kati ya wachungaji (Bahima) ambao walitawala
na wakulima (Bairu) ambao walitawaliwa na mara nyingi kudharauliwa.
Bahima (Balangira) walikuwa na koo chache zipatazo 20 na walitawaliwa na
Wahinda, Wabito na Wankango.
Bairu walikuwa na Koo kama 130 zenye
mashina 24 ambayo kiasili walikuwa Bairu lakini kwa kuoa katika Bahima
au kufanya kazi kwa Watemi walipandishwa hadhi na kuwa Bahima (Batware).
Kila ukoo uliitwa jina la Baba mwanzilishi wake na kina ukoo ulikuwa na
kitu walichokatazwa kula (Omuziro) na mnyama walioshirikishwa nae
(Ekyerumono).
Mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa
Kagera mwaka 1979 baada ya vita ya Tanzania na Uganda. Chini ya uongozi
wa Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo wakati huo Capt. Peter Kafanabo jina la
Kagera lilipendekezwa kwa sababu ya mto Kagera unaogusa sehemu kubwa ya
Wilaya zote zinazounda Mkoa wa Kagera.
Uchumi wa wenyeji wa Kagera ulijikita
katika mashamba ya migomba. Chakula chao kikuu ni ndizi katika aina zake
mbalimbali. Katika mashamba yao hulima mazao mengine kufuatana na
msimu. Mazao hayo ni pamoja na maharage, mihogo, mahindi na mboga. Baada
ya kuja kwa wazungu waliongeza ulimaji wa kahawa kama zao la biashara
lililowasaidia kujiongea kipato.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
MAJIMBO YA UCHAGUZI
|
Mkoa unayo
majimbo ya Uchaguzi 10 na wapo Wabunge 9 wa kuchaguliwa na Wabunge 3 wa
viti maalum. Jumla ya Wabunge 11 wanatoka chama cha Mapinduzi (CCM) na
Mbunge 1 anatoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Majina ya
waheshimiwa wabunge na majimbo wanayowakilisha pamoja na wale wa viti
maalumu ni kama ifuatavyo:-
|
|
|
Na
|
Jina La Mbunge
|
Jimbo
|
Chama
|
Wilaya
|
1.
|
Mhe. Hamis Sued Kagasheki
|
Bukoba Mjini
|
CCM
|
Bukoba
|
2.
|
Mhe. Jason Samson Rweikiza
|
Bukoba Vijijini
|
CCM
|
Bukoba
|
3.
|
Mhe. John Pombe Magufuli
|
Chato
|
CCM
|
Chato
|
4.
|
Mh.
Dk Antony Mbasa
|
B'mulo Magharibi
|
CHADEMA |
Biharamulo |
5.
|
Mhe. Begumisa Gosbert Blandes
|
Karagwe
|
CCM
|
Karagwe
|
6.
|
Mhe. Eustace Katagira
|
Kyerwa
|
CCM
|
Karagwe
|
7.
|
Mhe. Anna Tibaijuka
|
Muleba Kusini
|
CCM
|
Muleba
|
8.
|
Mhe. Charles Mwijage
|
Muleba Kaskazini
|
CCM
|
Muleba
|
9.
|
Mhe.Asumpta Nshunju Mushama
|
Nkenge
|
CCM
|
Missenyi
|
10.
|
Mhe. Deogratius Ntukamazina
|
Ngara
|
CCM
|
Ngara
|
11.
|
Mhe. Bernadetha Mushashu
|
Viti Maalumu
|
CCM
|
|
12.
|
Mhe. Elizabeth Batenga
|
Viti Maalum
|
CCM
|
|
13.
|
Mhe. Conjester Rwamulaza
|
Viti Maalum
|
CHADEMA
|
|
|
|
Vyama
vya siasa vinavyoendesha shuguli zake vizuri hapa mkoani ni pamoja na
CCM, TLP, NCCR - Mageuzi, CUF, UMD, UDP, na CHADEMA. Hatuna matukio ya
kukiukwa kwa sheria na utaratibu kwa vyama vya siasa.
|
HALI YA UCHUMI NA MAENDELEO YA MKOA
Uchumi wa mkoa
unategemea zaidi kilimo ambapo zaidi ya asilimia 70 ya watu
wanajishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula na biashara. Shughuli
za uvuvi, mifugo,viwanda na madini zinachangia pia katika uchumi wa
mkoa.
Kwa
kuzingatia malengo ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
(MKUKUTA) , Dira ya Taifa ya mwaka 2025 na malengo ya Milenia, Mkoa wa
Kagera unaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na umepiga
hatua katika sekta za uchumi, miundo mbinu na huduma za jamii. Hata
hivyo pamoja na hatua hizi zilizopigwa, juhudi za wananchi mkoani za
kujiletea maendeleo zinakumbana na matatizo na vikwazo mbalimbali
ambavyo vimeendelea kupatiwa ufumbuzi kwenye mipango ya maendeleo ya
Mkoa.
|
KANDA ZA IKOLOJIA (ECOLOGICAL ZONES) :
Mkoa wa Kagera umetenganishwa katika
Kanda tano za kilimo kuzingatia mwinuko wa maeneo hayo kutoka usawa wa
bahari na kiwango cha unyeshaji wa mvua.
|
|
•Ukanda wa kwanza :
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya mashariki ya wilaya ya Bukoba na
Muleba yanayoambaa kandokando ya ziwa victoria na uko katika mwinuko wa
mita 1,300 mpaka 1,500 kutoka usawa wa bahari. Mvua zinanyesha kwa
wastani wa milimita 800 - 1,750 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi
katika eneo hili ni kilimo cha ndizi, maharagwe, mahindi na kahawa. Eneo
la ukanda huu ni asilimia 17 ya eneo la Mkoa.
|
|
|
|
Ukanda wa pili :
Huu ni ukanda wa juu ulioko kwenye mwinuko wa mita 1,400 mpaka 1,800
kutoka usawa wa bahari. Ukanda huu unajumuisha maeneo ya juu ya wilaya
ya Karagwe na Ngara na mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800-1,000
kwa mwaka. Mazao yanayolimwa kwenye ukanda huu ni ndizi, maharagwe,
mahindi na kahawa. Eneo la ukanda huu ni asilimia 19 ya eneo la mkoa.
|
|
•Ukanda wa Tatu :
Ukanda huu uko katika mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari na
unajumuisha wilaya ya Ngara ,Biharamulo na Chato.Mvua zinanyesha kwa
wastani wa milimita 750-800 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi ni
uzalishaji wa mazao ya mahindi, mihogo, mpunga, mtama, karanga na pamba.
Eneo la ukanda huu ni asilimia 27 ya eneo la mkoa.
|
Ukanda wa Nne :
Ukanda huu upo kwenye mwinuko wa mita 1,000 kutoa usawa wa bahari na
unajumuisha maeneo ya mashariki ya wilaya ya Karagwe,wilaya ya Misenyi
na maeneo ya magharibi ya wilaya ya Bukoba. Mvua zinanyesha kwa wastani
wa milimita 800-1,000 kwa mwaka. Shughuli kuu za kiuchumi ni kilimo cha
mazao ya mahindi,maharagwe na ufugaji. Eneo la ukanda huu ni asilimia 10
ya eneo la mkoa.
Ukanda wa Tano :Ukanda
huu unajumuisha maeneo ya kaskazini ya wilaya ya Karagwe na Misenyi na
uko kwenye mwinuko wa mita 1,000 kutoka usawa wa bahari .Ukanda huu
unapata mvua za wastani wa milimita 750-800 kwa mwaka.Sehemu kubwa ya
ukanda huu ni misitu ya hifadhi na mapori ya akiba. Eneo la ukanda huu
ni asilimia 27 ya eneo la mkoa.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|